Njia 7 za kuishi maisha kwa ukamilifu: Wanawake wawili 'waliofufuka' wazungumza

Chanzo cha picha, Getty Images
Iwapo utaonyeshwa maisha yako yote kama filamu halisi machoni mwako, je utakachokishuhudia kitakufurahisha? Je kuna wakati tunahisi kujuta?
Mwandishi wa BBC Emma Barnett amezungumza na wanawake wawili waandishi wa vitabu ambao wamepitia uzoefu wa kukaribia kifo na kuwauliza iwapo mtazamo wao kuhusu maisha umebadilika.
Georgina Scull na Tanya Shadrick wanasema kwamba kipindi cha mpito kuelekea "maisha yao ya pili" sio cha haraka sana, walitathimini kwa subira na kwa uvasiri maisha yao na kujaribu kufanya maamuzi mapya.
Hadithi ya Georgina
Tanya alipatwa na tatizo la kuvuja damu kupindukia baada ya kujifungua akiwa na umri wa miaka 33.
Baada ya kutoka kwenye kipindi cha kupoteza fahamu (coma) Tanya aliamua kwamba anataka kuishi ‘’maisha ya pili’’ kwa njia tofauti.
''Ilitokea ghafla sana. Kuvuja damu kulianza mara moja. Nilifahamu kuwa ninakwenda kufa, ilitisha sana," Tanya anaongeza kuwa: Nilijutia uoga wangu katika ‘’Maisha ya kwanza’’. Kwenye karatasi, nilionekana mwenye mafanikio, lakini katika uhalisia nilikuwa ninayakimbia maisha."
"Katika maisha, mambo yanayobadilisha maisha yako huwa ya ghafla, hasa katika hali kama hizo mbaya. Inachukua muda kutambua umuhimu wa miito hii kwa njia iliyobora."
Georgina na Tanya wanashirikisha njia 7 za kuishi maisha kwa ukamilifu
1. Uwe mkweli hukusu kile unachokitaka

Chanzo cha picha, Getty Images
Georgina anasema kuwa maisha yetu yameundwa na sehemu tofauti kama vile marafiki, familia, kazi, na matamainio yetu katika kubadili maisha yetu katika nyakati tofauti.
Alitathmini maeneo mengi ya maisha kutoka nyakati tofauti na kutushauri kuachana na mambo ambayo hayatufurahishi advises , na kuzingatia zaidi vitu vingi ambavyo vinatufurahisha.
Tanya anasema kwamba wakati hatuhisi kuwa huru kwa sababu tofauti, ni kawaida sana kuhisi kujuta au kutaka kuanza mambo mapya.
Kuhusu hilo, Tanya anasisitizia kuhusu umuhimu wa kusikiliza sauti yetu ya ndani au hisia zetu za ndan, kujiamini na kuwa wenye subira.
Georgina nusura afariki akiwa na umri wa miaka 37 wakati mirija yake ya uzazi (fallopian tube) ilipopasuka kutokana na mimba iliyotungwa katika mirija hiyo nje ya kizazi.

2: Usiache kufanya kile ambacho unataka kukifanya
Georgina anaelezea kuwa kila mtu maisha huwa na mipango kwa ajili ya maisha yake ya baadaye, lakini wakati mwingine tunapoangazia sana hali ya usoni, kile kilichofanyika au ni nini kinaweza huwa kinasahaulika.
Georgina anasema: "Nenda kwenye hiyo safari ambayo umekuwa ukitamani kwenda, kutana na marafiki ambao umekuwa ukitaka kukutana nao, anza upya kufanya mambo unayoyapendelea. Furahia wakati ulionao sasa."
"Sio lazima kila wakati uwe na malengo fulani maishani mwako, lakini kila muda wa maisha yako unafaa kuuishi vyema. Kuwa wazi kwa uzoefu mpya ," anasema Tanya.
3. Usijaribu kubadili yaliyopita
Georgina anasema baadhi ya maamuzi tunayoyafanya maishani ni jaribio la kubadili maisha yetu ya nyuma.
Georgina anatumia kujieleza huku: "Iwapo ulikulia katika familia yenye uwezo wa chini kifedha, kipaumbele chako maishani huenda kikawa kupata pesa. Kama hukukulia katika familia yenye upendo wakati wote utakuwa unatafuta upendo.
Lakini kumbuka kuwa haiwezekani kubadilisha kipindi chako kilichopita. Kile tunachoweza kufanya ni kuishi sasa maisha kamilifu na jinsi ".
3. Usijiwekee ukomo wa muda
Tanya anasema, "Jamii yetu inaangalia utatuzi wa haraka wa kila tatizo. Tuna malengo kama jisi gani ninaweza kupunguza kilo 10 za mwili au ni jinsi gani ninaweza kukimbia kilomita 5 katika wiki sita. Ukweli ni kwamba, wakati tunapojipatia malengo ya muda mrefu, mamo mazuri zaidi huweza kutokea ."
Anaendelea kusema kuwa: "Uanafunzi nchini Uingereza kwa ujumla huchukua miaka 7. Kwanini tusitumie muda mwingi zaidi katika kufanya mambo tunayotaka kuyafanya? Unaweza kujiuliza binafsi maswali haya, iwapo unaweza kuhakikishiwa kuwa katika ajira katika somo moja kati ya miaka 10 au 20, ni somo gani ungelichagua?"
4. Endelea kutafuta vitu vipya
Georgina anasema: "Ni rahisi sana kukwama katika shuguli zisizo badilika. Jaribu kubadilisha kule unakokwenda na kile unachokifanya. Kutana na watu wapya. Kama hufanyi vitu hivi, dunia yako itasinyaa."
Na Tanya anashauri : "Ni vipi unaweza kufurahi kuhusu maisha? Unaweza kuangalia orodha ya vitu 100 unavyovipenda, kwa mfano. Fanya haya kwa siku au wiki. Mwisho wa muda ule utagundua mambo ambayo yanaweza kukusisimua na kukufurahisha."

Chanzo cha picha, Getty Images
6. Tambua upendo
"...Na sizungumzii tu kuhusu mahaba. Tambua upendo wa rafiki zako, familia, upendo wako binafsi, ya kazi," Georgina anaendelea kusema kuwa ‘’Mara nyingine hatujui thamani ya upendo ulio mbele yetu.
Lakini moja ya vitu vyenye ufanisi zaidi tunavyoweza kuvifanya vichangie furaha katika maisha yetu ni kutambua na kushukuru upendo katika maisha yetu."
7. Sahau kile watu wanachokifikiria kukuhusu
"Jaribu kutozingatia ni kwa jinsi gani watu wangapi wanapenda jumbe unazozituma kwenye mitandao yako ya kijamii au ni nini watu wanachokizungumzia kuhusu mambo uliyoyachagua wewe kuyafanya’’, anasema Tanya.
Tanya anaendelea kusema: "Badiliko kubwa unaloweza kulifanya maishani mwako ni kusema ndio kwa uzoefu mwingi, kwenda kwenye mikutano, kutojificha maisha .
Vitu ambavyo tunavifanya vigumu zaidi na baadaye haviji kutufaya tujute baadaye maishani." " Zinatia kuonyesha ujasiri kwa kile unachokithamini".















