Tetesi kubwa tano za soka Ulaya jioni hii

Chanzo cha picha, Getty Images
Klabu za Leeds United na Westham zinamuania kiungo wa Manchester City Kalvin Phillips. Phillips alijiunha na City toka Leeds msimu uliopita lakini amekosa namba Ettihad (Daily star).

Chanzo cha picha, Getty Images
Alex Telles, mlinzi wa Manchester United atarejea Old Trafford mwishoni mwa msimu kwa kuwa hakuna kipengele cha kumnunua moja kwa moja kwenye mkataba wake wa mkopo huko Sevilla aliko kaka (Romano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa pembeni wa Chelsea, Mykhailo Mudryk anapaswa kupewa muda na kumtathmini baada ya muda wake Chelsea sio wakati huu mfupi aliojiunga Stamford Bridge akitokea Shakhtar, anasema mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Andriy Shevchenko.

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool wanahusishwa na kiungo mhispania Gabri Veiga na wako tayari kumnunua mwishoni mwa msimu akitokea Celta Vigo (Thisisanfield).

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United inasaka mshambuliaji msimu ujao, huku jina la kinda wa Atalanta Rasmus Hojlund likiwavutia mashetani hao wekundu..Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 alifunga mabao matatu akiichezea Denmark kwa mara ya kwanza wiki hii. (Ekstra Bladet)








