Nini kinachosababisha mabinti wadogo kukoma hedhi mapema?

Hebu fikiria ukiwa katika ujana wako au umri wa miaka ishirini unapogundua kuwa unakaribia kukoma hedhi... Emma, So-Myat Noh na Elspeth hawakuweza kupiga picha ya kukua kwao (kubalehe).
Huu ulikuwa mwanzo wa safari kuelekea tukio muhimu maishani, na pia kupitia upweke ndani yake. Jambo linalotokea katika maisha ya kila mwanamke, lakini halijajadiliwa sana.
Ilikuwa asubuhi mnamo Agosti 2013. Daktari alipokagua faili ya Emma Delaney na kusema kwamba alikuwa amekoma hedhi akiwa na umri wa miaka 25. Emma alikaa kimya kwenye kiti cha hospitali. Kila alichokuwa anakisema daktari, mawazo yake yalikuwa yakienda huku na huko akilini mwake.
Hakuwa anapata hedhi na pengine hatapata tena. Hakukuwa na nafasi ya yeye kupata mimba kawaida.
"Nilipigwa na butwaa. Daktari aliniambia kuwa sitaweza kupata watoto," alisema. Emma ni mmoja wa wanakikundi cha wanawake walio na ugonjwa unaoitwa Primary Ovarian Insufficiency (POI).
Upungufu wa uwezo wa Ovari kwa mwanamke (POI)
Kukoma hedhi yoyote ambayo hutokea kabla ya umri wa miaka 40 inahusishwa na hali hii ya kupungua uwezo wa ovari za mwanamke. Mara nyingi hakuna sababu maalum ya hii. Wanawake walio na POI hawapati dalili za kukoma hedhi hadi wafikishe miaka hamsini.
Takriban mwanamke mmoja kati ya 100 nchini Uingereza wanakabiliana na aina hii ya hali ya kiafya. Kulingana na wataalamu, idadi hii inaweza kuwa kubwa zaidi. Lakini hili ni suala ambalo halijajadiliwa vya kutosha.

"Kuna mijadala michache sana kuhusu kukoma hedhi kwa vijana wenye umri mdogo," anasema daktari na nyota wa TikTok na mtaalamu wa masuala ya hedhi Dk. Nihat Arif.
"Kwa ujumla tunafikiria tu kuhusu wanawake wenye umri mkubwa na wenye mvi, lakini sio hivyo ilivyo," Arif anasema. '
'Ilikuwa ndoto yangu kuwa na watoto wawili'
Kwa upande wa wanawake wengine kama Emma, haijulikani kwa nini ovari zao hazifanyi kazi. Hata hivyo, POI pia inaweza kusababishwa na kingamwili, matatizo ya kromosomu, au upasuaji wa tumbo na ovari.
Pamoja na athari za kimwili za aina hii ya ugonjwa, athari za akili pia zinaweza kuwa hatari sana. Baada ya daktari wa Emma kumweleza jambo hilo, alikaa kwenye gari lake akilia kwa muda wa saa moja hivi.
Emma anafanya kazi katika saluni yenye shughuli nyingi jijini Manchester, Uingereza. Hawakujua lolote kuhusu kukoma hedhi zaidi ya kile walichokisikia kutoka kwa vikongwe waliokuwa wakifika hapo. Ndoto waliyokuwa nayo ya maisha ya baadaye wakiwa na watoto wawili iliiishia hapo.

Kwa miezi michache iliyofuata, Emma alitakiwa apate tiba ya kupandikizwa homoni (HRT). Waligundua kuwa ovari zake zimeacha kufanya kazi. Pia, mwili wake haukuweza kuzalisha homoni za estrojeni na progesterone za kutosha.
Homoni hizi hudhibiti mzunguko wa hedhi katika mwili. Upungufu wa homoni hizi ulikuwa ukiathiri mwili wake kwa miaka.
'Athari za pombe na ngono mwilini'
Hakuwa sawa, alisikia joto mwili mzima. Pia, kutoweza kulala usiku hakutokana na usingizi, lakini haya yote zilikuwa dalili za matatizo ya homoni au homon inbalance.
Mama Emma alikuwa na miaka arobaini. Lakini hakuwa amefikia kukoma hedhi, lakini mwanae akiwa na miaka 25 tayari amekoma hedhi. Lakini haingejalisha sana.
Marafiki zao walikuwa wametulia na walikuwa na watoto wao wenyewe. Nilihisi hakuna mtu angenielewa," alisema.
Emma aliamua kujikita zaidi kazini na kukwepa kuzungumzia jambo hilo. Akaanza kutoka usiku na marafiki zake wa kike na wakiume.
Walitaka kuishi maisha tofauti sana na marafiki na wenzi wao na watoto. Anasema "Nilikuwa nikiukatili mwili wangu kwa pombe na ngono...sikutambua umuhimu wa kuzungumza na mtu kuhusu hilo," alisema.
Kukabiliana na kukoma kwa hedhi
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kukabiliana na kukoma kwa hedhi kabla ya wakati au mapema kunaweza kuwa jambo gumu sana.
Idadi kubwa ya wanawake, hugunduliwa kuwa na tatizo hili baada ya kuanza matibabu ugonjwa mwingine mkubwa. So-Myat Noh, mwanafunzi wa ubunifu wa picha huko London, alikabiliwa na kukoma kwa hedhi kama athari isiyotarajiwa ya matibabu ya saratani.
Katika umri wa miaka 23 tu, aligunduliwa na saratani ya koloni ya hatua ya III. Mionzi ya tumbo ilikuwa imeharibu ovari zake, lakini wakati huo hakuelewa maana halisi ya hii.
"Wote (madaktari, wauguzi) walijiegemeza kabisa kutibu saratani yangu. Sikumbuki mtu yeyote alisema chochote kuhusu kukoma kwa hedhi," alisema Myat.
Dalili zake zilionekana ghafla na zilikuwa kali sana. Hizi ni pamoja na mzio masikioni, hofu na uchovu.
Somyat anasema alipokuwa akikua, mazungomzo kuhusu hedhi, uzazi na kukoma hedhi haikuwa mada ya kawaida kwake. Kwa hiyo hawakujua mengi kuhusu hilo. Marafiki zao katika chuo kikuu walikuwa na wasiwasi kila wakati kuhusu IUD na tembe za kupanga uzazi, lakini uzoefu wa So-Myat ulikuwa tofauti.

"Kwa sababu ya kila kitu kilichokuwa kikitokea kwangu, siku zote nilikuwa nikiungana na watu wazima. Nilihisi kukosa kitu katika maisha yangu."
Akaunti ya mtandao wa kijamii ya Dkt. Nihat Arif imejaa ujumbe kutoka kwa wanawake ambao wamekuwa wakipitia tatizo hilo. Anatoa wito "Jadili suala hili na wanawake katika maisha yako ... jadili na mama yako, nyanya, shangazi, shangazi, dada au rafiki bora. Hakuna kitu cha kuonea aibu. Jaribu kujifunza kutokana na uzoefu wao."
Kupungua kwa hamu ya mahusiano ya kimapenzi
Wanawake wengi wanagunduliwa na tatizo hili la kukoma hedhi kutokana na kuongezeka kwa ufahamu wa dalili, lakini bado kuna safari ndefu, anasema Dk Arif anasema.
Ikiwa halijatibiwa kwa muda mrefu, inaweza kuwa na athari za muda mrefu kwa mifupa, moyo na akili ya mwanake. "Baadhi ya wagonjwa wamehuzunishwa sana na hili. Wanaweza kuwa walitaka watoto. Inaweza kuuua ndoto zao za maisha au matamanio," aliongeza.
Katika upasuaji wake, Dk. Arif pia alipata athari zingine nadra na ambazo hazijajadiliwa sana. Hizi ni pamoja na maumivu wakati wa ngono, kupoteza hamu ya tendo.

Elspeth Wilson mwenye umri wa miaka 23 anafahamu veyama kuhusu hali hii. Aligundulika na tatizo hili (POI) akiwa na umri wa miaka 15 tu. Kutokana na hili, anasema alikumbana na ugumu wakati wa kushiriki mapenzi yeye na mpenzi wake.
"Unapokuwa kwenye uhusiano na mtu unataka kumuonyesha kuwa unampenda. Lakini mwili wako usipokubali hali hiyo na mambo yanakuwa ya ajabu, na magumu sana," alisema.

Alijisikia vizuri kujadili katika kikundi cha WhatsApp cha wanawake wengine ambao walikuwa wanakabiliwa na hali kama hiyo. Hakuna kikomo cha mzungumzo katika kundi hilo.
"Pia inatia moyo sana kuuliza maswali kuhusu hilo. Ni rahisi zaidi ikiwa una uwezo wa kuzungumza yanayokusibu bila kuona aibu yoyote."
Kwa upande wa So-Myat, ambaye alishiriki katika kikundi cha usaidizi cha mtandaoni kwa mabinti wanaokabiliwa na kukoma kwa hedhi kutokana na saratani, alikubali kueleza.
Emma pia alijifunza na baada ya muda alikubali kuzungumza kwa uwazi zaidi juu ya uzoefu wake. Alianza kwa kumwambia mshauri kila kitu kilichokuwa akilini mwake.
Miaka michache iliyopita Emma alikutana na mwenzi wake ambaye alikuwa anajua matatizo yake ya afya ya kimwili. Wote wawili wanaishi pamoja sasa.

Emma, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 34, pia anatarajia kupata watoto katika siku zijazo kwanjia ya kuasili.
Pia, ameamua kuvaa fulana nyeusi kwenye saluni hiyo. Kauli mbiu kama "Make Menopause Matter" imeandikwa juu yake. Kauli mbiu hii kwenye t-shirt yake imefunikwa kwa kiasi fulani kutokana na madoa ya kupauka.
Mteja wake anaposema kuwa Emma ni mdogo sana kuweza kukabiliana na kukoma hedhi, anaeleza hali yake yote ya kiafya alipokuwa akifanya kazi kwenye saluni.
Wanawake huniambia kwamba baada ya dakika 30 walipata habari zaidi kuhusu kukoma hedhi kuliko walivyopata katika maisha yao yote. "Ninajivunia kwamba ninasema jambo ambalo ni muhimu kwa kila mwanamke."












