Jeff Bezos: Mtindo wa uhisani wa Marekani unafanana na ule wa Uingereza?
Na Stephen Smith, BBC

Chanzo cha picha, Getty Images
Uhisani ama ufadhili, unaozidi kuwapatia hadhi watu matajiri na mashuhuru duniani, ni jambo linalogonga vichwa habari kwa sasa.
Lakini uhisani unamaanisha nini kwa sasa hasa kwa mwaka 2022? Na je, unafanana na unavyofanyika nchini Marekani kama inavyofanya nchini Uingereza, anauliza Stephen Smith.
Mfanyabiashara maarufu wa bitcoin wa Marekani Sam Bankman-Fried alikuwa mmoja wa watu wanaoangaziwa zaidi katika harakati mpya ya kutoa misaada inayojulikana kama "Effective Altruism" (EA).
Badala ya kuhangaika sana na masuala ya misaada, badala yake wafuasi wa EA wanapendelea kuwekeza kwenye fedha na teknolojia, na kisha kuzitoa kwa wahisani.
Lakini biashara ya Bankman-Fried mwenye umri wa miaka 30, ya fedha za mtandaoni, FTX, ilifilisika mapema mwezi huu.
Utajiri wake ulipururuka mara moja - ulikuwa na thamani ya $10.5bn (£8.68bn). Kuhusu wadai wake, mbali na kujipongeza kwa ufanisi wa kujitolea kwao, sasa wamepata hasara ya karibu kiasi cha $8bn.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati huo huo, mwanzilishi wa Amazon, Jeff Bezos alitangaza nia yake ya kutoa "sehemu kubwa ya mali zangu nyingi" katika maisha yake, ishara ya ukarimu kwa mtu huyo ambaye ana utajiri wa thamani ya $117.5bn kwa mujibu wa Forbes.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Tayari ametoa $2.4bn katika maisha yake ya kazi, kinasema chanzo hicho hicho.
Haijulikani ni jinsi gani Bezos anatarajia kutekeleza ahadi yake. Hajatia saini 'Giving Pledge', mpango uliozinduliwa na Bill Gates na Warren Buffet ili kuwashawishi matajiri wenzao kwamba wanapaswa kutoa mali zao nyingi kwa mashirika ya misaada.
Na wakosoaji wameeleza kuwa utajiri mkubwa wa Bezos hauhusiani na rekodi ya kampuni yake kuhusu kodi. Nchini Uingereza, Amazon inalipa kodi kkutokana na faida yake lakini si kwa mauzo yake, ikikabidhi £492m kama ushuru wa moja kwa moja kwa Forodha, huku mapato yake mwaka jana yakifikia £20.63bn.
Kampuni hiyo imeshutumiwa kwa kulipa mishahara ya chini na mazingira duni ya kufanya kazi, na wafanyakazi wa Amazon katika maeneo kote ulimwenguni walifanya matembezi kwenye Black Friday, abayo ni siku inayuofuata badaa ya siku ya mapumziko ya shukrani ya Marekani.
Katika miaka ya hivi karibuni, aina mpya ya uhisani imeibuka nchini Uingereza - ikihusisha mwanaharakati nyota wa michezo au wanamuziki. Mchezaji kandanda Marcus Rashfordwa Manchester United, aliongoza Orodha ya Sunday Times kwa wanaojitolea kwa mwaka 2021, kupitia kampeni yake dhidi ya umaskini wa chakula na wafadhili wakuu wa mwaka huu ni pamoja na dereva wa mbio za magari Lewis Hamilton, mwanasoka Mo Salah na rapa Stormzy.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hata hivyo, utamaduni - na suala la kodi - hutofautisha mitazamo ya uhisani kati ya Uingereza na Marekani. Wamarekani walitoa $484.85bn kwa mifuko ya hisani mwaka wa 2021, kwa ujibu wa National Philanthropic Trust (NPT) nchini Marekani.
Waingereza walichangia £10.7bn, linasema shirika la Charities Aid Foundation. Marekani ina takribani mara tano ya idadi ya watu wa Uingereza lakini Wamarekani wanatoa mara 45 zaidi ya fedha hiyo.
"Watu matajiri nchini Marekani wana matarajio kwamba wale ambao wamefanikiwa kifedha watatoa (watasaidia)- sana - au kiasi fulani," anasema Dk Beth Breeze, mkurugenzi wa Kituo cha Uhisani katika Chuo Kikuu cha Kent.
Anasema "mafanikio" nchini Marekani hayangaliwi tu kwa kiasi gani watu anatengeneza fedha lakini pia kwa jinsi wanavyotoa (kusaidia) kwa uwazi.
Bezos anaishi katika muktadha wa kitamaduni ambao unatarajia watu kama yeye watoe, anaongeza Breeze kusema, na mke wake wa zamani MacKenzie Scott ndiye mhisani anayependwa zaidi wa kisasa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wahisani wakubwa wa Uingereza kwa mwaka 2021
- Meneja wa Hedge fund, Sir Chris Hohn anayetoa mamilioni ya kwa ajili ya mazingira na afya za watoto
- Mfanyabiashara Alan Parker pia amejielekeza kusaidia kwa ajili ya mazingira na usalama wa watoto
- Mwekezaji Sir Paul Marshall - elimu na usawa wa kijamii
- Mjasirimali Lord Edmistonaliyeanzisha Christian charity
- Mwendesha magari Lewis Hamilton alichangia mamilioni ya fesha kusaidia kuboresha fursa kwa vijana.
Orodha hii ni kwa mujibu wa Sunday Times Giving List














