Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 04.01.2024

Iliyochapishwa

Manchester United inapanga kuanza mazungumzo juu ya mkataba mpya na beki wa Uingereza, Aaron Wan-Bissaka mwenye umri wa miaka 26 mwishoni mwa msimu huu. (Mail)

Mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 31, anakaribia kuongezewa mkataba mpya katika klabu ya Liverpool licha ya kutakiwa na Saudi Pro League. (Football Transfers na Anfield Watch)

Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia (PIF) umefufua nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Manchester City na Ubelgiji, Kevin de Bruyne, mwenye umri wa miaka 32. (Rudy Galetti)

Borussia Dortmund wanataka kumsajili beki wa kushoto wa Chelsea, Ian Maatsen, 21, kwa mkopo au kwa mkataba wa kudumu. (Telegraph)

Dortmund wanataka winga wa Manchester United, Muingereza, Jadon Sancho, 23, ajiunge na timu hiyo kwa mkopo katika kambi yao ya mazoezi ya Marbella wiki ijayo. (Sky Sports)

Manchester United wana nia ya kumfanya winga wa Crystal Palace Michael Olise, 22, kuwa mmoja wa wachezaji wa kwanza kusajiliwa huko Old Trafford. (Standard)

Crystal Palace wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Uingereza, Eddie Nketiah lakini Arsenal hawatamuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 mwezi Januari - ikiwa hawatapata mbadala wake. (Ben Jacobs)

Meneja wa Girona, Michel Sanchez ameibuka kama mbadala wa meneja wa Newcastle United Eddie Howe. (Marca)

Klabu ya Ligue 1 ya Ufaransa, Lyon inataka kumsajili winga wa West Ham na Algeria, Said Benrahma, huku Wolves na Fulham pia wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Footmercato)

Mshambuliaji wa Ujerumani, Timo Werner, 27, amekuwa shabaha ya Manchester United, huku RB Leipzig ikitarajiwa kuruhusu mkataba wa mkopo. (Mirror)

Everton wanatafuta kumuuza kiungo wa kati Mreno, Andre Gomes kwa sababu ya mshahara mkubwa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Football Transfers)

Monaco wako kwenye mazungumzo na West Ham kuhusu uhamisho wa mkopo, wakitaka kumchukua beki wa Ujerumani Thilo Kehrer, 27. (Fabrizio Romano)

Sheffield United wanakaribia kumsaini mshambuliaji wa Villarreal na Chile, Ben Brereton Diaz, 24, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Fabrizio Romano)

Wolves wako kwenye mazungumzo ya kumsajili kwa mkopo kutoka Paris St-Germain - kiungo wa kati wa Gabon mwenye umri wa miaka 18 Noha Lemina, kaka yake Mario Lemina, . (Talksport)

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Esther Namuhisa