“Kazi ya sanaa ni kuelimisha na kuburudisha lakini ubunifu nao usivuke mipaka”

Iliyochapishwa

Emmanuel Simwenga kwa jina marufu Izzo Bizzines ni mwanamuziki wa kizazi kipya nchini Tanzania ambaye amekuwa akifanya shughuli za muziki tangu mwaka 2009 alipoachia kibao chake cha kwanza.

Akizungumza na BBC Izzo amesema Tanzania iko mbioni kuzindua mdundo wa taifa ambao utakuwa alama ya muziki wa Tanzania kimataifa. Sanaa ya muziki wa kipya ni moja kati ya sekta zinazoendelea kutoa ajira kwa vijana nchini humo kutokana na kuendelea kukua kila siku baada ya jamii kubadili mtazamo juu ya Sanaa hiyo na wasanii na kuitambua kama kazi rasmi.