Kutana na Mwanamke anayetumia picha kuonyesha thamani ya miili ya wanaume

Pix

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Wanaume sita wako kwenye chumba kimoja. Mmoja anawarushia maua ya waridi. Kuna mwanamke kando anawatazama kupitia kamera na kuwaambia wanaume hao wabadilishe pozi. Wanaume wote hao wako bila nguo.

Zoezi la upigaji picha linaendelea. Lakini kuna tofauti kubwa. Wanaume wote wako bila nguo wanapigwa picha na mwanamke mmoja pekee ambaye yeye amevaa nguo.

Jina la mpiga picha ni Yushi Lee. Alizaliwa nchini China. Sasa anaishi London.

Anataka kuleta mabadiliko katika uwanja wa upigaji picha na haswa katika picha za mapambo akitumia wanaume.

Yushi Lee anasema sanaa yake ya upigaji picha inahusu mambo matatu; jinsia, mvuto na hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

Anasema kuwa miili ya wanaume ndio kitovu muhimu cha mvuto katika mambo hayo matatu.

"Wanawake daima huchukuliwa kuwa warembo au wanapaswa kuwa warembo. Kwa hiyo tunafikiri kwamba miili ya wanawake tu ndio mizuri na muhimu. Tunathamini miili ya wanawake kuliko miili ya wanaume,” anasema Lee.

"Lakini tukiangalia wanyama, wanyama madume ndio wenye mvuto zaidi.,kwa mfano Simba na Tausi. Mwili wa kiume hauthaminiwi katika uwanja wa upigaji picha za mapambo. Ninahisi kutokuwa na usawa ndani yake. Miili ya wanaume haipewi umuhimu mkubwa,” anaongeza.

Miili ya wanaume ina thamani kubwa na kitovu cha mvuto.

Kwa mujibu wa Lee, anataka kubadilisha hali hii. Wapiga picha wa kiume na wachoraji wengi wamekuwa wakitumia miili ya wanawake kwa maelfu ya karne, anasema.

“Sasa nina kamera mkononi mwangu. Ninapiga picha ninavyohisi.”

Wanaume wengine wamechapisha picha zao kwenye mitandao ya kutafuta wenza na wapenzi kama Tinder. Lakini Lee anasema hawamvutii sana. “Wanaume hawafikirii sana kujitengeneza kuvutia,” asema.

Hata sasa, wanamitindo wa kiume hawajui jinsi ya kupiga picha za kuvutia. “Mwanaume hajifikirii sana. "anaongeza.

men

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Inaelezwa wanaume hawaoni kama miili yao ina thamani na wengi wahafikirii sana kuipamba na kuipendezesha ivutie

Anadai kuwa uzuri wa asili wa wanaume unaweza kuonekana kwenye picha anazopiga. "Nadhani picha ninazopiga ni kielelezo ya kile ninachotamani," Lee anasema.

Katika baadhi ya picha, Yushi Lee huenda peke yake. Anasema hili ni jaribio la kufanya uhusiano kati ya picha na hadhira kuwa maalum.

Yushi Lee anatoka China. Katika nchi za Magharibi, wanawake wa Asia wanachukuliwa kuwa wa kuvutia ingawa ni wafupi. Anasema majibu yake ni mchakato wa kujibu mtazamo huu.

Wanaume wanaopigwa picha hizi wanafikiria nini kuhusu mtazamo wa Lee?

Mtazamo wa Lee ni kwamba anataka kubadilisha dhana ya kwamba wenye mvuto kwenye picha ni wanawake tu. Yeye anaamini hata wanaume wanamuonekano mzuri kwenye picha na wanaweza kutumika kuvutia biashara mablimbali. Picha za namna yoyote ile.

Kinachokosekana ni mpiga picha mzuri wa kufanya picha zitoke vizuri zivutie na ziwe na faida kibiashara. Kwa sasa ameanza kubadilisha mtazamo huo ili picha za wanaume ziwe kwenye majarida makubwa, mitandao na bidhaa mbalimbali. Lakini wanaovutiwa zaidi ni wanawake ambao ni wanunuzi zaidi wa bidhaa. Huu ndio mtazamo wa Lee kuliko sasa, zinatumika picha za wanawake zaidi.

Hata hivyo Wanawake wanapowauliza wanaume kuhusu kutuma picha zao, wanaume hawajui nini cha kutarajia, anasema mwanamitindo Ulster Graham.

"Wanawake wanapowauliza wanaume kutuma picha, wanaume hutuma picha za utupu. Nini kitatokea nitakapotuma picha ya viungo vyangu?” Wanauliza swali hili.

Adenye

Immunel Adenye ni mwanamitindo. Anasema hata hakufikiria kuwa kuna uzuri wowote katika mwili wake. "Sikuzote nimehisi kwamba kazi ya mwili ni muhimu zaidi kuliko mwonekano wa mwili," anasema.

"Ningependelea kuwa injini ya gari kuliko kuiangalia tu. Sijawahi kuona mwili wa mwanaume kama njia ya kufurahisha. Sasa nmeona manufaa yake,” anasema Adenye.

Je! miili ya wanaume inaonekana kama bidhaa ama vitu?

Picha za Yushi Lee ni tofauti na video za kawaida za muziki wa kufokafoka kwa mfano. Video za kufoka huangazia wanawake wenye mvuto na wakati mwengine wakiwa nusu utupu wakicheza karibu na waimbaji wa kiume. Adenye anasema anachofanya kwakwe ni tofauti kabisa. Ni kiyume chake.

Lakini swali pia liliibuka ikiwa wanaume kwenye picha za Lee wanatumika kama kama vitu ama bidhaa. Wanamitindo hao wa kiume walisema kwamba haya yote yalikuwa yakifanyika kwa idhini yao na kwamba Lee aliwapa heshima hata kwenye wakati ambao walipaswa kuondoa nguo zao zote ama baadhi ama wakati wa kubadilisha nguo.