Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
'Nijitavunja mkono, mguu wangu... Nitafanya lolote kuepuka kwenda vitani Ukraine'
Kwa wanaume wengi wa Urusi, uamuzi wa Kremlin wa kuwajumuishi wanajeshi 300,000 waliohifadhiwa kwa ajili ya vita nchini Ukraine ulikuja kuwa mshtuko.
Katika majiji makubwa, vita vya miezi saba vya Urusi dhidi ya jirani yake vimeonekana kuwa mbali sana. Lakini punde tu hotuba ya Rais Vladmir Putin ilipokwisha, iligonga mwamba. Kutumwa kwenye vita kulikuwa karibu zaidi kuliko mtu yeyote angeweza kufikiria.
Gumzo la ujumbe wa ofisini lililipuka na mijadala yenye wasiwasi kuhusu kitakachofuata. Mipango ilifanywa jinsi ya kuepuka kupelekwa mstari wa mbele.
"Ilikuwa kama filamu ya sci-fi kutoka miaka ya 1980. Inatisha kidogo kuwa mkweli kwako," anasema Dmitry, 28, ambaye anafanya kazi katika ofisi huko St Petersburg. Wafanyikazi hawakuweza kuanza siku yao ya kazi, walishikilia hotuba kwenye skrini zao za runinga, kompyuta na simu za rununu.
Alijiondoa ofisini baada ya chakula cha mchana na kwenda kubadilisha rubles kwa dola kwenye benki iliyo karibu.
Dmitry alihama baada ya kutembelewa na polisi kwa kushiriki katika maandamano ya kupinga vita - akiamini kuwa itakuwa vigumu kwa mamlaka kumpata.
"Sina hakika cha kufanya baadaye: ibiri ndege inayofuata kwenda nje ya nchi au ubaki Urusi kwa muda mrefu kukabiliana na polisi kwenye maandamano kadhaa ya kupinga vita."
Sergei -sio jina lake halisi - tayari ameitwa kujiunga na wanajeshi wa ziada.
Mwanafunzi wa PhD mwenye umri wa miaka 26 na mhadhiri katika chuo kikuu maarufu cha Urusi, alikuwa akitarajia kuletewa mboga usiku kabla ya hotuba ya Putin wakati kengele ya mlango ililia. Badala yake, alikabiliwa na wanaume wawili waliovalia kiraia ambao walimpa karatasi za kijeshi na kumtaka atie sahihi.
BBC ina nakala ya karatasi hizi, kumuomba akiunge na kituo cha usajili siku ya Alhamisi.
Ikulu ya Kremlin ilisema ni watu ambao wamefanya kazi yao ya kijeshi na walikuwa na ujuzi maalum na uzoefu wa mapigano ndio watakaoitwa. Lakini Sergei hana uzoefu wa kijeshi na baba yake wa kambo ana wasiwasi, kwani kukwepa wito jeshini ni kosa la jinai nchini Urusi.
Baba yake wa kambo anafanya kazi katika kampuni ya mafuta ya serikali na saa kadhaa baadaye aliombwa kutoa orodha ya wafanyakazi ambao walikuwa na msamaha wa kisheria kutoka kwa utumishi wa kijeshi.
Wanaume wengi wa Urusi hawafanyi hivyo, wengi wamekuwa wakitafuta njia za kuepuka wito.
Huko Moscow, Vyacheslav anasema yeye na marafiki zake walianza kutafuta miunganisho ya matibabu ili kusaidia.
"Afya ya akili au matibabu ya uraibu wa madawa ya kulevya yanaonekana kuwa mazuri, ya bei nafuu au labda chaguzi za bure," alisema.
"Iwapo utapigwa mawe na kukamatwa unapoendesha gari, tunatumai utanyang'anywa leseni yako na itabidi upate matibabu. Huwezi kuwa na uhakika lakini tunatumai hii itatosha kuepuka kuchukuliwa [jeshi]."
Shemeji yake alikwepa rasimu hiyo kwa sababu hakuwa nyumbani wakati maafisa walikuja kupiga simu. Mamake aliona hati hizo, ambazo zilimtaka aripoti kazini kati ya 19 na 23 Septemba.
"Sasa amejifungia katika chumba kimoja na kukataa kutoka," anasema Vyacheslav. "Ana watoto wawili wadogo wenye umri wa miaka mitatu na mmoja: anapaswa kufanya nini?"
Mwanaume mwingine, kutoka Kaliningrad, aliiambia BBC kuwa atafanya lolote ili kuepuka kuandikishwa jeshini: "Nitavunjika mkono wangu, mguu wangu, nitaenda gerezani, chochote ili kuepuka jambo hili zima."
Maelfu ya Warusi walihudhuria maandamano ya kupinga vita katika miji kote Urusi Jumatano usiku. Wengi walisema walikabidhiwa karatasi za wito ama barabarani au baadaye katika kizuizi cha polisi.
Shirika la kutetea haki za binadamu la OVD-Info liliorodhesha hadi vituo 10 vya polisi mjini Moscow pekee ambapo waandamanaji walipewa karatasi zao. Angalau mtu mmoja katika wilaya ya Vernadsky ya Moscow alikataa kutia saini na kutishiwa kwa kesi ya jinai.
Mwanamke mmoja aliambia tovuti huru ya Mediazona kwamba mumewe alikamatwa katika maandamano ya kupinga vita huko Arbat katikati mwa Moscow. Alifikishwa kituo cha polisi, akakabidhiwa karatasi za kujiunga jeshini na kuzisaini huku akichukuliwa video na polisi. Aliambiwa ajitokeze kuandikishwa siku ya Alhamisi.
Mikhail, mwenye umri wa miaka 25, alikuwa ameondoka Urusi kuelekea nchi jirani ya Georgia mwanzoni mwa vita na alirudi tu katika mji wake mdogo wa Urals kwa siku chache. Alikuwa amepanga kurejea lakini sasa ana wasiwasi na tishio la silaha za nyuklia la Rais Putin na atasalia nchini Urusi, karibu na familia yake.
"Tuko katika hali ya hofu. Katika mji wangu sehemu kubwa ya watu tayari wamepokea karatasi za wito lakini sijasajiliwa kuishi hapa kwa hivyo sitazipata."
Hivi karibuni alikuwa amepata kazi nzuri huko Tbilisi lakini sasa anaona kuwa haina maana kwa sababu ya kuongezeka kwa oparesheni ya kijeshi ya Vladimir Putin.
"Sijali tena, naishi kwa leo tu."