AFCON 2023: Msimamo na muelekeo ukoje kuelekea mechi za kufuzu wiki hii?

Iliyochapishwa

Mechi za mzunguko wa tatu na nne za kuwania kufuzu kwa Fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2023) zitapigwa kwa muda wa siku nane zijazo huku mataifa 45 yakijaribu kufuzu fainali zijazo za michuano hiyo zitakazofanyika nchini Ivory Coast kuanzia Januari mwakani.

Nchi tano zimeshinda michezo yao yote miwili ya ufunguzi, ikiwa ni pamoja na Morocco waliofuzu nusu fainali Kombe la Dunia na mabingwa watetezi Senegal.

Timu mbili za juu kutoka katika makundi 12 ya timu nne nne zitatinga fainali - isipokuwa katika Kundi H ambapo wenyeji Ivory Coast wanafuzu moja kwa moja na timu nyingine tatu zinacheza kuwania nafasi moja.

Makundi mawili pia yamepunguzwa hadi timu tatu kwa sababu ya Shirikisho la soka duniani, FIFA kuzipiga marufuku kujishughulisha na soka nchi za Kenya na Zimbabwe.

BBC Sport Africa inaangalia namna mzunguko wa makundi unavyoendelea.

Kundi A

Nigeria iliichapa Sierra Leone 2-1 nyumbani na kisha kuizaba Sao Tome 10-0. Mshambulizi wa Super Eagles, Victor Osimhen ndiye mfungaji bora wa michuano hiyo mpaka sas akiwa amefunga mabao matano.

Majirani wa Nigeria kutoka Afrika Magharibi Guinea-Bissau pia wameanza vyema kampeni zao kwa kushinda nyumbani dhidi ya Sao Tome na kutoka sare ya 2-2 ugenini dhidi ya Sierra Leone.

Hapo jana Sierra Leone na Sao Tome zilienda sare ya 2-2

Machi 24: Nigeria v Guinea-Bissau

Machi 26: Sao Tome na Principe v Sierra Leone

Machi 27: Guinea-Bissau v Nigeria

Kundi B

Burkina Faso, ambao walifika fainali mwaka 2013, waliibuka na ushindi dhidi ya Cape Verde na kisha kutoka nyuma na kuifunga Eswatini.

Cape Verde ilitinga hatua ya 16 bora ya Afcon iliyopita nchini Cameroon kabla ya kuchapwa na Senegal ambao walikuwa mabingwa. Baade waliwachapa Togo.

Mechi zijazo:

Machi 24: Burkina Faso v Togo / Cape Verde v Eswatini

Machi 28: Togo v Burkina Faso / Eswatini v Cape Verde

Kundi C

Timu tatu katika Kundi C zinachuana kuwania nafasi mbili baada ya Kenya kuondolewa kufuatia kusimamishwa kwao na Fifa kwa sababu ya serikali kuingilia masuala ya michezo.

Washindi mara tano Cameroon, chini ya kocha Rigobert Song, walichukua usukani wa kundi hilo kwa ushindi wa 1-0 nchini Burundi katika mhcezo wao pekee hadi sasa.

Machi 23: Cameroon v Namibia

Machi 28: Namibia v Cameroon

Kundi D

Hili ndilo kundi linaloonekana kuwa na mshuano mklai zaidi kati ya makundi 12 kwani timu zote nne zina alama tatu baada ya raundi mbili za mwanzo.

Timu bora katika orodha ya Fifa duniani Misri, wako mkiani kwa tofauti ya mabao baada ya ushindi wao dhidi ya Guinea na kuchapwa 2-0 ugenini na vinara Ethiopia, ambao walishiriki katika AFCON ya kwanza mwaka 1957 lakini wamefuzu mara mbili tu tangu 1982.

Kwingineko, Malawi iliishinda Ethiopia lakini ikachapwa na Guinea, na kuacha kundi likiwa gumu zaidi kutabirika.

Machi 24: Guinea v Ethiopia / Misri v Malawi

Machi 28: Ethiopia v Guinea / Malawi v Misri

Kundi E

Mechi za kwanza kwa kocha mpya wa Ghana Chris Hughton zitakuwa mbili dhidi ya Angola iliyo nafasi ya pili.

Black Stars walitoka suluhu na Madagascar katika mchezo wao wa ufunguzi lakini wakatoka sare ugenini dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Madagascar ilitinga robo fainali ya AFCON 2019 - michuano pekee kufuzu kufikia sasa - na watakuwa na matumaini ya kufuzu tena kupitia michezo yao miwili dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Machi 23: Madagascar v Jamhuri ya Afrika ya Kati / Ghana v Angola

Machi 27: Jamhuri ya Afrika ya Kati v Madagascar / Angola v Ghana

Kundi F

Algeria wanawania kufuzu fainali za AFCON kwa mara ya ishirini na mabingwa hao wa mwaka 2019 bado hawajaruhusu bao katika mechi za ushindi nyumbani dhidi ya Uganda na ugenini nchini Tanzania.

Niger pia hawajafungwa lakini wametoka sare katika michezo yao yote miwili na kuwafanya Uganda na Tanzania kuwa katika wakati mgumu wakijiandaa kukabiliana na Algeria.

Tanzania sasa iko chini ya kocha mpya, baada ya kumteua Malgeria Adel Amrouche ambaye pia amewahi kuzifundisha Kenya, Burundi, Libya na Botswana.

Machi 23: Algeria v Niger

Machi 24: Uganda v Tanzania

Machi 27: Niger v Algeria

Machi 28: Tanzania dhidi ya Uganda

Kundi H

Uamuzi wa kuwajumuisha wenyeji Ivory Coast katika hatua ya makundi ulifanywa ili kuwapa mazoezi ili wasiingie kwenye michuano hiyo kwa hasara bila kucheza soka la ushindani.

Kati ya nchi nyingine zinazopigania nafasi moja ya wazi ya kufuzu katika Kundi H, mabingwa wa mwaka 2012, Zambia wako katika nafasi nzuri zaidi baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Comoro, shukrani kwa bao la dakika za lala salama kutoka kwa kiungo Kings Kangwa.

Zambia imemteua kocha wa zamani wa Chelsea na Ghana Avram Grant

Machi 23: Zambia v Lesotho

Machi 24: Ivory Coast v Comoro

Machi 26: Lesotho v Zambia

Machi 28: Comoro v Ivory Coast

Kundi I

Vinara wa kundi hilo Mauritania bado hawajaruhusu bao huku wakijaribu kufuzu AFCON kwa mara ya tatu.

Gabon pia wana ushindi mmoja na sare moja katika mechi za mbili za kwa kwanza ugenini.

Matokeo ya kusikitisha ya DR Congo hadi sasa yanamaanisha kuwa Leopards wanapaswa kukaza buti baada ya kupoteza michezo yao miwili ya kwanza ambapo wamefunga bao moja pekee.

Machi 23: Gabon v Sudan

Machi 24: DR Congo v Mauritania

Machi 27: Sudan v Gabon

Machi 29: Mauritania v DR Congo

Kundi J

Vinara wa Kundi Tunisia, ambao wameshinda kombe hilo mara moja pekee, walipokuwa wenyeji mwaka wa 2004, walianza vyema kwa ushindi wa 4-0 nyumbani dhidi ya Equatorial Guinea lakini wakatoka sare tasa na Botswana.

Libya, ambayo hivi karibuni imebadilisha kocha wao, pia ilipata ugumu wa kucheza dhidi ya Zebra lakini ilishinda mchezo huo kwa bao moja, na baadaye kufungwa ugenini dhidi ya Equatorial Guinea.

Machi 24: Equatorial Guinea v Botswana / Tunisia v Libya

Machi 28: Botswana v Equatorial Guinea / Libya v Tunisia

Kundi K

Morocco, wakiwa na uwanda mpana wa kujiamini baada ya ubabe wao kwenye fainali za Kombe la Dunia, wameshinda michezo yao yote miwili na wanaongoza kundi hilo. Katika mzunguko wa sasa hawana mchezo wa mchujo, wana mechi ya kirafiki dhidi ya Brazil.

Michezo mawili wiki hii inayowakutanisha Afrika Kusini na Liberia itaamua nani atashika nafasi ya pili.

Kama Kenya, Zimbabwe pia inatumikia adhabu ya Fifa na imeondolewa.

Machi 24: Afrika Kusini v Liberia

Machi 28: Liberia v Afrika Kusini

Kundi L

Mabingwa watetezi Senegal wanaoongoza kundi hili, huku Sadio Mane akifunga mabao manne, wanakabiliana na mpinzani wake wa karibu Msumbiji katika michjezo miwili ya nyumbani na ugenini.

Benin, ambayo hivi majuzi ilimteua kocha wa zamani wa Nigeria, Gabon, Niger na Burkina Faso Gernot Rohr, ilifika robo fainali mwaka wa 2019 lakini wamepoteza michezo yote miwili hadi sasa. Pia wameachana na jina la utani la "Squirrels".

Mechi dhidi ya Rwanda ambao wamepoteza mmoja na kutoka sare mmoja ni muhimu kwa timu hiyo ambayo sasa inajulikana kwa jina la "The Cheetahs".

Machi 22: Benin v Rwanda

Machi 24: Senegal v Msumbiji

Machi 27: Rwanda v Benin

Machi 28: Msumbiji v Senegal