Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 23.03.2024
Real Madrid inaongeza shauku ya kumnunua beki wa kulia wa Liverpool na England Trent Alexander-Arnold, huku kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 huko Anfield ikikamilika mwaka ujao. (Relevo )
Meneja wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso atajiunga na Bayern Munich badala ya Liverpool ikiwa atahamia popote msimu huu wa joto. ( Sky Sports News)
Chelsea wako kwenye mazungumzo ya juu na Lyon kuhusu kumteua Sonia Bompastor, kiungo wa kati wa zamani wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 43, kuchukua mikoba ya Emma Hayes katika klabu ya WSL. (ESPN)
Chelsea waliongoza mbio za kumnasa mshambuliaji wa Brazil Endrick lakini wasiwasi kuhusu ada hiyo uliwaruhusu Real Madrid kuwashinda hadi kumsajili kinda huyo wa miaka 17 kutoka Palmeiras. (Telegraph )
Manchester United wako tayari kumnunua mlinzi wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 Gleison Bremer, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 43 katika mkataba wake na Juventus. (Mirror)
Aston Villa huenda ikalazimika kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Jacob Ramsey, 22, ili kusaidia kuepuka kukiuka sheria za faida na uendelevu. (Football Insider)
Newcastle United huenda ikalazimika kumuuza mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 24, msimu wa joto ili kuzingatia kanuni za uchezaji haki za kifedha. (Football Insider)
Winga wa Sunderland Jack Clarke, 23, hatatia saini kandarasi mpya katika klabu hiyo ya Championship, ambayo inaweza kuibua shauku mpya kwa Muingereza huyo kutoka West Ham na Lazio. (I)
Aliyekuwa mkuu wa uajiri wa Arsenal Sven Mislintat anaweza kurejea Borussia Dortmund kama mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo. (Sky Sports German)