Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 14.09.2024
Wakala wa mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 32, ameongeza uvumi kuhusu hatma yake katika klabu ya Liverpool baada ya kutuma kauli ya hasira kwenye mitandao ya kijamii. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ameamua kwamba hatohamia Newcastle United kwa sababu anataka kucheza soka la Ulaya. (Football Insider)
Everton wamedhamiria kusimama na Sean Dyche kwa angalau msimu mzima huku kukiwa na shinikizo kubwa kwa meneja huyo ambaye yuko mkiani mwa Ligi Kuu ya Uingereza. (Telegraph - subscription required)
Mkufunzi wa Newcastle Eddie Howe amedai kuwa baadhi ya wapinzani wao walijaribu kuongeza bei maradufu kwa malengo fulani katika miaka ya mapema baada ya klabu hiyo kunyakua klabu hiyo ikiungwa mkono na Saudi Arabia. (Chronicle Live)
Howe pia alitetea rekodi yake ya uhamisho kama meneja wa Newcastle United katika jibu kali kwa kukosolewa na mkurugenzi mpya wa michezo Paul Mitchell kwamba muundo wa kuajiri wa klabu "haufai kwa madhumuni".(Telegraph - subscription required)
Arsenal na Chelsea zinatarajiwa kumjumuisha mshambuliaji wa Sporting Lisbon na Uswidi Viktor Gyokeres, 26, kwenye orodha yao ya wachezaji watakaowanunua dirisha la usajili la majira ya joto litakapofunguliwa. (Football Insider)
Mkurugenzi wa zamani wa ufundi wa Stoke City,. Ricky Martin yuko kwenye sura ya kuwa mkurugenzi mpya wa michezo wa Carlisle United . (Teamtalk, external)
Chelsea na Tottenham bado wanavutiwa na mlinzi wa Lecce wa Denmark Patrick Dorgu, 19, ambaye thamani yake ni takriban euro 40m (£33.8m). (La Gazzetta dello Sport kupitia SportWitness)
Leeds United walikuwa na ofa ya pauni milioni 8.5 ili kumsaini mchezaji wa kimataifa wa Hungary Roland Sallai lakini winga wa wakati huo wa Freiburg , 27, hakushawishika kuhusu uhamisho wa msimu wa joto na kujiunga na miamba ya Uturuki Galatasaray . (HITC)
Beki wa Chelsea Muingereza Ben Chilwell anatumai kujumuishwa katika kikosi cha wachezaji 25 cha klabu hiyo kinachoshiriki Ligi ya Premia, kwakuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 hatarajiwi kuhamia Uturuki kwa mkopo. (Telegraph - Subscription required)
Mtendaji mkuu wa Liverpool Michael Edwards anaongoza harakati za klabu hiyo za kumtafuta kiungo mpya wa kati. (Football Insider)
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi