Darya Trepova: Tunachojua kuhusu mtuhumiwa wa mauaji ya mwanablogu wa Urusi Vladlen Tatarsky

th

Chanzo cha picha, JJ.OOOEE/VK

Iliyochapishwa

Kuzuiliwa kwa Darya Trepova kwa mauaji ya mwanablogu wa Urusi anayeunga mkono vita Vladlen Tatarsky kumeibua maswali kuhusu historia na siasa za mwanadada huyo.

Ripoti za vyombo vya habari vya Urusi zinasema Bi Trepova, 26, alimkabidhi Tatarsky sanamu ambayo iliaminika kuwa na vilipuzi vilivyomuua. Baadaye katika video iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Urusi, anaonekana akikubali hili .

Walakini, kuna uwezekano mkubwa kwamba taarifa yake ilipatikana kwa kulazimishwa, na hasemi ikiwa alijua kuhusu vilipuzi.

Maafisa wa Urusi wanasema mauaji hayo yalipangwa na idara za usalama za Ukraine kwa usaidizi wa Taasisi ya Kupambana na Ufisadi (RBK), inayoongozwa na kiongozi wa upinzani wa Urusi aliyefungwa jela Alexey Navalny, ambayo wanasema Bi Trepova ni mfuasi wake.

Lakini marafiki na familia wanasema kwamba alipokuwa mwanaharakati wa kupinga vita - aliripotiwa kuzuiliwa kwenye maandamano mwanzoni mwa vita - maoni yake hayakuwa ya itikadi kali na hakuwa na uwezo wa kuua.

Mumewe Dmitry Rylov anapendekeza kwamba labda alidanganywa.

Kwa hivyo tunajua nini kumhusu Darya Trepova?

Mtu anayemfahamu aliiambia BBC kwamba alienda shule katika mji wa Pushkin nje ya St Petersburg, akiongeza kuwa "hakuonekana kuwa na maoni yoyote ya kisiasa wakati huo".

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Vyanzo vingine vinasema baadaye alijiunga na chuo kikuu cha jimbo la St Petersburg, ingawa haijulikani ni kitivo gani, na haaminiki kuwa alimaliza kozi yake.

Kulingana na rafiki yake mwingine, alifanya kazi kwa muda mrefu katika duka la nguo jijini, lakini aliacha kazi yake mwezi mmoja uliopita na kuhamia Moscow.

Haijabainika ni muda gani ameolewa na Bw Rylov.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Agentstvo, marafiki wa Bi Trepova walisema kwamba ndoa yao ilikuwa "mzaha" na walikuwa marafiki tu.

Lakini baadhi ya ripoti zinasema wawili hao wote walikamatwa katika maandamano ya kupinga vita tarehe 24 Februari mwaka jana, mwanzoni mwa uvamizi wa Ukraine.

Bi Trepova alizuiliwa kwa siku 10, inaonekana kwa kupuuza maombi ya polisi kwa umati kutawanyika.

Bw Rylov anasemekana kuwa mwanachama wa kundi dogo la upinzani liitwalo Libertarian Party, ambalo lilihusika katika maandamano hayo. Chama kilisema alikuwa amehama.

Pia iliambia kituo cha Telegram cha SOTA kwamba Bi Trepova hakuwa na uhusiano na chama hicho, na kwamba ililaani mauaji ya Tatarsky.

Baadhi ya ripoti zinasema Bw Rylov pia anasakwa kuhusiana na mauaji hayo.

Aliiambia SVTV News kwamba hangeweza kufanya mauaji kwa hiari. "Ninaamini kuwa mke wangu alidanganywa," alisema.

“Ndiyo, ni kweli kwamba hakuna hata mmoja wetu anayeunga mkono vita vya Ukraine, lakini tunaamini kuwa vitendo hivyo haviruhusiwi.

"Nina uhakika 100% kwamba hangekubali jambo kama hili kama angelijua kuhusu hilo."

Ripoti zinasema wachunguzi wa Urusi hawajafutilia mbali uwezekano kwamba Bi Trepova hakujua ni nini kilikuwa kwenye sanamu hiyo.

Pia, chanzo cha RBK kilisema msichana huyo alikuwa akiwasiliana na Tatarsky - mwathirika wa mlipuko wa mkahawa - na alihudhuria hafla za hapo awali alizohusika nazo

th

Chanzo cha picha, MVD.RU

Maelezo ya picha, Maelezo ya Darya Trepova yaliongezwa kwenye orodha ya watu wanaotafutwa na wizara ya mambo ya ndani saa chache kabla ya kuzuiliwa