Jinsi vipimo vya mkojo vilitumika zaidi ya miaka 4,000 iliyopita kubaini ujauzito

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Leo, kujua ikiwa una mjamzito ni rahisi sana: unatumia kifaa kidogo(kwenye picha hapo juu) ambacho kimebuniwa mahasusi kuonyesha kama umepata ujauzito- michirizi miwili ionekane.

Vipimo vya nyumbani vya ujauzito vilitumika kwa mara ya kwanza katika miaka ya 1960.

Vinafanya kazi kwa kugundua homoni ya gonadotropini ya chorionic (hCG) ya binadamu kwenye mkojo, ambayo hutolewa hasa na seli kwenye tumbo la uzazi wakati wa ujauzito.

Vipimo vya damu vinaweza kukupa jibu ndani ya siku 11 tu baada ya kupata ujauzito na vipimo vya mkojo siku chache baadaye.

Matokeo chanya mara nyingi huonekana kama mwanzo wa safari ya kuwa mzazi.

Lakini mambo yalikuwa tofauti sana zamani. Dalili dhahiri kama vile kukosa hedhi au hamu ya kula zinaweza kumaanisha ujauzito.

Lakini, hadi baadaye sana katika ujauzito hakukuwa na njia ya kujua ikiwa ishara hizi hazikutokana na ugonjwa au kukoma kwa hedhi.

Kutafuta mbinu

Tangu zama za Ugiriki ya kale, iliaminika kuwa wanawake wangejua ikiwa ni wajawazito kwa sababu wangehisi kizazi kiko karibu baada ya kujamiiana hali ambayo bila shaka haliwezekani.

Hasa ikizingatiwa kwamba ni mapema sana katika hatua hiyo ya awali kubaini kama mimba ilipachikwa moja kwa moja kutokana na kitendo cha kujamiano

Lakini hii haikuwazuia watu kutafuta mbinu ya kubainisha dhana hiyo kwa uhakika zaidi.

Jarida la matibabu la Hippocratic ya karne ya 4 KK. C. "Aphorisms" ilipendekeza kunywa mchanganyiko wa divai, maji na asali kabla ya kwenda kulala. Ikiwa mwanamke angepata ujauzito, mchanganyiko huo ungesababisha maumivu na tumbo lake kunguruma.

Kim Phillips, Mhadhiri wa somo la historia katika Chuo Kikuu cha Auckland, alisomea "Siri za Wanawake," utafiti wa matibabu ya karne ya 13 ambayo yaliwafahamisha wasomaji wake kwamba ikiwa matiti ya msichana yanaelekea chini, inamaanisha alikuwa mjamzito.

Iliaminika kuwa hii ilikuwa hivyo kwa sababu "wakati mimba inapojitungwa kawenye kizazi, damu ambayo ingetoka kwa njia ya hedhi huelekezwa kwenye matiti."

Jukumu la mkojo

Leo hii, mkojo ndio chanzo halisi cha kupata jibu thabiti iwapo mwanamke amepata ujauzito.

Na ingawa inaweza kuonekana kama njia ya kisasa, mbinu hii ilianza kutumika kitambo. Kwa kweli, maandiko ya wanazuoni wa Misri ya kale yanaonyesha kwamba mkojo ulitumiwa kubaini ujauzito kwa miaka 4,500.

Maandiko hayo yalieleza kwamba mwanamke angeweza kujua ikiwa amepata ujauzito, akikojolea ngano na shayiri kwa siku kadhaa.

Wamisri wa kale walifanya vipimo vya ujauzito kwa kutumia mkojo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wamisri wa kale walifanya vipimo vya ujauzito kwa kutumia mkojo.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ikiwa shayiri iliota ya kwanza mtoto alitarajiwa kuwa mvulana, lakini ikiwa ngano itaota ya kwa basi mto alitarajiwa kuwa wa kike. Ikiwa hakuna mbegu iliyoota, basi mwanamke huyo hakuwa na mimba.

Katika karne ya 16, neno sindano lilitafsiriwa vibaya, ambalo kwa Kiingereza linaitwa niddle na lilitafsiriwa visivya na kuitwa nettle, na hii ilizua dhana kwamba mwanamke alilazimika kuacha nettle kwenye mkojo wake usiku kucha ili kuona ikiwa ina michirizi yekundu kwenye mkojo wakati wa asubuhi, kwani hii ilikuwa dalili kwamba alikuwa mjamzito.

Vipimo hivi viliweza kufanywa bila uangalizi wa daktari. Tangu kuanzishwa kwake mnamo 1518, Chuo cha Kifalme cha Madaktari huko London kimepiga marufuku waganga wa kike kufanya udaktari.

Mwanzoni mwa karne ya 17, mwanamke aliyejulikana kama "Bi. Phillips" - pengine mkunga - alipelekwa mahakamani kwa kutumia uroscope kugundua ujauzito.

Catherine Chaire, mwanamke ambaye alisomea udaktari kinyume cha sheria huko London katika miaka ya 1590, alikuwa na mbinu yake mwenyewe: Alisema angeweza "kutambua ujauzito kwa kufua nguo kwa sabuni na maji ya zafarani nyekundu."

Mbinu za kisasa

Kuzingatia mkojo katika vipimo vingi ni mwendelezo wa kile tunachojua leo.

Wamisri wa kale waliwafanya wanawake kukojolea mbegu za ngano na shayiri ili kujua kama walikuwa wajawazito.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wamisri wa kale waliwafanya wanawake kukojolea mbegu za ngano na shayiri ili kujua kama walikuwa wajawazito.

Na tofauti za vipimo vya msingi wa mkojo imejirudia katika maandishi ya matibabu hadi karne ya 17.

Mkojo wa mwanamke ulipokwa kwenye chombo kilichofungwa kwa siku chache, "viumbe fulani vilivyo hai" vilionekana, kulingana na kitabu cha 1656 "Complete Practice for Midwives."

Utaratibu mwingine ulikuwa kuchemsha mkojo (ikiwa mistari nyeupe ilionekana, mwanamke alikuwa mjamzito).

Ilikuwa katika tafiti za miaka ya 1930 ambapo mapendekezo ya utafiti wa kwanza wa vipimo vya mbegu, vilivyoelezewa katika tafiti za Misri ya kale kama muujiza, haipaswi kupuuzwa.

Utafiti uliopima nadharia uligundua kuwa 70% ya wakati, mkojo wa wanawake wajawazito ulikuza mbegu, ingawa hakukuwa na uhusiano wowote na jinsia ya mtoto.

Wakati mkojo wa wanaume au wanawake ambao hawakuwa na mimba ulitumiwa, haikuwa na athari.

Kwa hakika, kulikuwa na dutu ya pekee katika mkojo wa wale wa wanawake wajawazito.

Utafiti wa karne ya 20 ulionyesha kwamba majaribio haya yote ya kihistoria - iwe kwa mbegu au sindano - yalikuwa na matokeo ya kitu cha kuaminika zaidi kuliko mchanganyiko maalum, kuosha nguo kwa maji ya zafarani, au kuangalia matiti.

Panya, sungura na vyura

Njia nyingine ya kutumia mkojo kubaini ujauzito iliibuka katika miaka ya 1920 na 1930.

Kwanza, panya au sungura walidungwa mkojo kutoka kwa mwanamke mjamzito, na kisha waliuawa ili kuona ikiwa ovari zao zimebadilika.

Baadaye, chura hai walitumiwa katika majaribuo hayo. Ikiwa mwanamke alikuwa mjamzito, chura angetoa mayai.

Utafiti juu ya mada hiyo uliendelea hadi miaka ya 1950. Lakini njia hizi zote zilikuwa ghali na sio sahihi kwa ailimia 100. Pia hazikuwa nzuri kwa panya au chura.

Na katika miaka ya 1960, kazi mpya ya kingamwili ilisababisha majaribio tunayojua leo.

Mimba daima imekuwa na jukumu muhimu katika historia ya wanawake.

Kupata mimba ilikuwa muhimu katika masuala ya mirathi na urithi. Na historia ya vipimo vya ujauzito inaonyesha kwamba watu walikuwa wakiangalia katika mwelekeo sahihi, hata kabla ya kuwa na zana za kuwa na uhakika wa matokeo.