'Muujiza' wa Qatar: Mabadiliko yaliyoifanya nchi hii kuwa moja ya mataifa tajiri zaidi duniani  

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,  Majengo marefu mjini  Doha pamoja na picha za Kombe la Dunia  
Iliyochapishwa

Sio kipindi kirefu kilichopita, Doha, mji mkuu wa Qatar, haukua mji wa baadaye na mbali na mji wa picha za kuvutia zinazoonekana mwaka huu 2022, siku chache baada ya kupokea Kombe la dunia la Soka. 

Karne moja iliyopita, katika 1922, taifa hili dogo la Ghuba lenye wakazi milioni tatu na chini ya kilomita za mraba 12,000 km²  ilikuwa ni ardhi ambayo haikuwa na wakazi, makazi duni ya wavuvi na wakusanyaji wa lulu ambapo wengi wa wakazi walikuwa ni wa kuhamahama waliotoka katika majangwa ya mbali ya mlango bahari ya Arabia.

 Ni watu wachache tu wenye umri wa miaka 90 ambao wanaweza kukumbuka leo hali ngumu ya uchumi waliyoishi katika miaka ya 1930 na miaka 1940, baada ya uvumbuzi wa Lulu wa Wajapan, waliitengeneza kwa wingi na kuangusha uchumi wa Qatar.  

Katika karne ile, Qatar ilipoteza hadi 30% ya wakazi wake walioondoka kutafuta fursa katika nchi za ng’ambo. Miaka kumi baadaye, katika mwaka 1950, haikuwa na watu zaidi ya 24,000 wakazi wake kulingana Umoja wa Mataifa.    

Lakini wakati huo uchumi wa Qatar ulikuwa katika kipindi cha mageuzi. Ilipata muujiza: moja ya hifadhi kubwa zaidi za mafuta duniani. 

Sasa Qatar ina majengo marefu na makubwa, ya kifahari, na visiwa bandia na viwanja vya mpira vya kisasa. Katika BBC BBC tunachambua mabadiliko matatu

ambayo yalisababisha mabadiliko ya nchi na kuwa moja ya nchi tajiri zaidi duniani. 

1.    Uvumbuzi wa mafuta

Wakati Qatar ilipogundua dhahabu yake nyeusi, ilikuwa bado haijawa taifa  na ilikuwa ni mikononi mwa Uingereza, ambayo ilichukua udhibiti wa eneo mwaka 1916.

Baada ya miaka kadhaa ya uvumbuzi, hifadhi za kwanza za mafuta zilibainika katika eneo la  Dukhan mwaka 1939, kwenye mwambao wa magharibi mwa nchi kilometa 80 kutoka Doha.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uchumi wa Qatari ulianza  kubadilika haraka mwaka 1939, kwa uvumbuzi wa kwanza wa hifadhi za mafuta katika eneo la Dukha, magharibi mwa nchi

Kwa kuvutiwa na kushamiri kwa sekta ya viwanda, wahamiaji na wawekezaji walianza kuwasili Qatar, na idadi ya watu ikaanza kuongezeka.

Mwaka 1950 Qatar  ilikuwa na wakazi chini ya 25,000 lakini  kufikia mwaka 1970 ilikuwa na zaidi ya wakazi 100,000.

Kutoka nchi ya wavuvi na wakusanyaji wa lulu, katika mwaka 1970 Qatar tayari ilikuwa na pato la ndani ya nchi (GDP)  ya zaidi ya dola milioni  300 za Marekani. 

Mwaka mmoja baadaye , Qatar ilitangazwa kama taifa huru baada ya kuondoka kwa Uingereza. Enzi mpya ambayo pia ilikuja na uvumbuzi wa pili ulioleta utajiri.

Ugunduzi wa gesi asilia 

Wakati wa uvumbuzi katika mwaka 1971 wahandisi walivumbua  hifadhi ya gesi katika North Field, kwenye mwambao wa Qatar, ni wachache waliotambua umuhimu wake.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Kampuni ya Qatargas, ambayo huzalisha gesi ya kimiminika duniani – kukua kwa sekta hii ni miongoni mwa mambo makuu yaliyochangia katika ukuaji wa uchumi wa Qatar.   ​​​

Lakini sawa a mafuta, faida kubwa iliyotokana na mauazo ya gesi ilikuwa ikiongezeka taratibu.

Mapinduzi ya 1995  katika Ufalme

Ukuaji wa uchumi wa Qatari ulishamiri kwa kuingia kwa karne ya 21.

Ni kati yam waka 2003 na  2004, Pato la ndani ya nchi (GDP) lilipanda kutoka  3.7% hadi  19.2%.

Miaka miwili baadaye, katika mwaka 2006, uchumi upipanuka kwa 26.2%. 

Ukuaji huu wa GDP umekuwa msingi wa uthabiti wa  Qatar kwa miaka kadhaa.

G

"Mageuzi haya ya kiuchumi yalifanyika  baada ya  Hamad bin Khalifa al Thani ,baba yake emir wa sasa wa Tamim bin Hamad Al Thani,  kuchukua madaraka mwaka 1995, ambalo lilikuwa ni tukio tata kwa baadhi kwasababu namana yalivyofanyika ,"  

 Pato la ndani ya nchi nchini  Qatar lilikuwa ni $61,276 mwaka 202. Iwapo pia tutazingatia suala la uwezo wa ununuzi, kiwango hicho kinapanda hadi kufikia  $93,521 kulingana na Benki ya dunia, kiwango ambacho ni cha juu  zaidi duniani. 

Aidha taifa la  Qatari hutoa ujira wa juu zaidi, na pia kutoa elimu  bora kwa umma na mifumo yake ya afya imeimarika.   

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wataalamu wanaelezea kuwa  kupanda kwa njia   utata mamalakani  Hamad bin Khalifa al Thani kama mojawapo ya sababu za mageuzi ya kuvutia ya ukuaji wa uchumi wa Qatari baina ya mwishoni mwa karne ya 20 na mwanzoni mwa karne ya 21.   

Changamoto ya uchumi wa  Qatari  

Hatahivyo, ukuaji wa kuvutia wa uchumi wa Qatari umekumbwa na vikwazo na kusababisha kupungua kwa kazi ya ukuaji huo katika miaka ya hivi karibuni.

Pia inaonyesha changamoto zinazoikabili kwa siku zijazo, ikiwa ni pamoja na suala la nishati ya mafuta yatokanayo na fossil , ambayo yanachunguzwa kwa athari zake kwa mabadiliko ya tabia nchi.  

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, The Shard, ni jengo refu zaidi mjini London, ambalo ni sehemu ya uwekezaji wa mfuko wa    utajiri wa Qatari  

 Zaidi ya hayo vikwazo ilivyowekewa Qatari  kati ya mwaka 2017 na  2021 na Saudi Arabia, Milki za Kiarab , Bahrain na Misri baada ya mzozo wa kidiploamasi na Doha, vilichagiza ustahimilivu wa uchumi wa Qatari.   

 Mfano wa jaribio hili ni uwepo wa mamlaka ya uwekezaji ya Qatar, hali ya mfuko wa taifa, na mali za nchi hii zinazofahamika katika miji kama  London au  New York.

 Utajiri wa kiuchumi wa Qatar umekuwa ukionekana katika zaidi ya  dolama milioni $200,000 ambazo imewekeza katika Kombe la Dunia, ambalo ndio ghali zaidi katika historia- ujenzi wa viwanja vinane vya michezo, uwanja mpya wa ndege  na leri mpya, hiyo ikiwani baadhi tu ya miundo mbinu michache iliyojengwa  kwa ajili ya tukio hilo.

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Qatari imekua ikijiandaa kwa  Kombe la dunia ghali zaidi katika historia ya miaka 12  

Sehemu kubwa ya maswali ambayo wengi duniani wanajiuliza  ni jinsi ambavyo  tukio hilo limekuwa likiandaliwa, huku kukiwa na na malalamiko kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu kuhusu hali za wafanyakazi wanaohusika na ujenzi, wengi wao wakitoka  katika nchi kama vile Nepal, India na  Bangladesh.

 Zaidi ya hayo kuna madai ya ufisadi na hongo dhidi ya  Qatar na shirikisho la kimataifa la mpira wa miguu (FIFA) wakati iliposaini kupokea mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2010.

 Mbali na shutuma hizo, ni wazi kwamba hii ni zaidi ya Kombe la Dunia kwa nchi ndogo ambayo imekua tajiri katika kipindi kifupi na sasa inataka kujiweka kama nchi muhimu kijiografia kwa kuwa  kisasa zaidi na inayoendelea.