Tetesi za soka Ulaya Jumanne tarehe 11.04.2023

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kalvin Phillips
Iliyochapishwa

Aston Villa wana nia kubwa ya kusaini ni mkataba na kiungo wa kati wa England Kalvin Phillips, 27, kutoka Manchester City. (Football Insider)

Kiungo wa England Ben Chilwell, 26, yuko tayari kusaini mkataba mpya wa miaka minne katika klabu ya Chelsea. (Athletic - subscription required)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Baba yake Lionel Messi na wakala wake Jorge walikutana na Barcelona lakini hakuna pendekezo la uhamisho lililotolewa kwa ajili ya mshambuliaji huyo Muagerntina mwenye umri wa miaka 35. (Cadena Ser, via Mirror)

Wing'a wa Ujerumani Marco Reus, 33, yuko tayari kusaini mkataba mpya na Borussia Dortmund – lakini mshahara wake utakatwa ili aendelee kubakia katika klabu hiyo . (Bild - in German)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wan-Bissaka

West Ham wanamfuatilia kwa karibu mchezaji wa safu ya kati-nyuma Muingereza Wan-Bissaka, 25, wakiwa na mpango wa kumhamisha msimu ujao wa joto. (Football Insider)

Arsenal wako huru kumuuza mshambuliaji wa kikosi cha England Folarin Balogun katika msimu ujao. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 kwa sasa yuko katika klabu ya Reims kwa mkataba wa mkopo. (Times - subscription required)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ridle Baku

Arsenal na Chelsea ni miongoni mwa vilabu kadhaa vinavyotaka kumchukua kiungo huyo wa Wolfsburg na Ujerumani Ridle Baku, 25. (Bild - in German)

Chelsea ina matumaini ya kuendela kuwa na Joao Felix msimu ujao. The Blues walisaini mkataba wa mkopo na mshambuliaji huyu Mreno mwenye umri wa miaka 23 kutoka klabu ya Atletico Madrid mwezi Januari. (Fabrizio Romano)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ridle Baku

Newcastle United inataka kusaini mkataba na mshambuliaji Mbrazili Joao Pedro, 21, kutoka Watford katika msimu ujao wa kiangazi. (Football Insider)

Brighton wana matumaini ya kuafikia mkataba mpya na kiungo wa safu ya mashambulizi Evan Ferguson, licha Manchester United na Tottenham kuwa na nia ya kumsajili (Mail)