Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
COP27: Uchafuzi unaosababishwa na mafuta nchini Misri unatishia ustawi wa miamba ya matumbawe adimu duniani
Wakati Misri ikiwa mwenyeji wa viongozi wa dunia kujadili hatua kuhusu mabadiliko ya hali ya tabia nchi, kituo cha mafuta kinamwaga maji machafu yenye sumu kwenye pwani ya Bahari Nyekundu nchini humo, uchunguzi wa BBC idhaa ya kiarabu umegundua.
Aina adimu ya matumbawe, ambayo hutoa tumaini la kuhifadhi viumbe vya baharini kadiri sayari inavyopata joto, inaweza kuwa hatari. Nyaraka zilizovuja zilizopatikana na BBC na kundi la wanahabari wasio wa faida ya Source Material zinaonesha kuwa "maji yanayozalishwa" kutoka kituo cha mafuta cha Ras Shukeir nchini Misri yanamwagwa kwenye Bahari Nyekundu kila siku.
Maji machafu ambayo huletwa ardhini wakati wa kuchimba mafuta na gesi - yana viwango vya juu vya sumu, mafuta na grisi. Nyaraka hizo, ambazo zilitolewa na Kampuni ya Ghuba ya Suez Petroleum (Gupco) mwaka 2019 ili kujaribu kuajiri kampuni ya kutibu maji hayo, zinasema viwango vya uchafuzi wa mazingira "havizingatii" sheria na kanuni za mazingira za Misri.
Kila siku, mita za ujazo 40,000 za maji haya yenye sumu - sawa na mabwawa 16 ya kuogelea yenye ukubwa wa mabwawa ya Olimpiki - yanaingia kwenye Bahari Nyekundu, nyaraka zinasema.
Dkt. Greg Asner, mwanaikolojia katika Chuo Kikuu cha Arizona State, anasema habari hiyo "ni ya kutisha sana", inayoonesha uchafuzi wa madini ya risasi, cadmium, shaba, nikeli na metali nyingine nzito. "Sio lazima uwe mtaalamu kujua kuwa kuna jambo haliko sawa hapa," anasema.
Nyaraka zilizovuja zinaonesha kuwa serikali ya Misri inafahamu kuhusu tatizo la maji machafu tangu mwaka 2019, baada ya kampuni ya mafuta ya Uingereza BP kuuza hisa zake 50% katika kiwanda hicho kwa kampuni ya Falme za Kiarabu, Dragon Oil.
Asilimia 50 nyingine inamilikiwa na kampuni ya mafuta ya serikali ya Misri.
Uuzaji wa BP ulikuwa sehemu ya uamuzi wa kuondoa mali ya kampuni yenye thamani ya $10bn (£8bn wakati huo), iliyoonekana na wachambuzi wengi kama mpango wa kusaidia kufikia malengo ya hali ya hewa.
Caroline Lucas, Mbunge wa Uingereza wa Chama cha Kijani, anasema: "Haishangazi kwamba BP na wengine wangependelea kuuza mali zao chafu zaidi, zinazoharibu mazingira, kuliko kuzisafisha wenyewe."
BP iliiambia BBC uuzaji wa sehemu yake ya Gupco ulikuwa kwa sababu za kifedha, sio kama sehemu ya mpango wowote wa kufikia malengo ya hali ya hewa.
Ilirejelea maswali kuhusu maji machafu kwa Gupco. Gupco na wizara ya mazingira ya Misri hawakujibu ombi la BBC la kutoa maoni yao.
Ufikiaji wa Ras Shukeir ni mdogo kwa wafanyikazi wa mafuta na wakaguzi wa serikali. Hata hivyo, BBC iliweza kutumia picha za satelaiti kuchunguza kiwango cha uchafuzi wa maji.
Uchambuzi wa picha za satelaiti zenye mwonekano wa juu unaonesha maji mengi ya kijani kibichi yanayotiririka baharini, yakisafiri hadi kilomita 20 (maili 12) kusini katika maeneo yanayohifadhi viumbe vya baharini.
Kampuni ya kuchanganua satelaiti ya Soar.Earth ilitumia mbinu za ufuatiliaji wa ubora wa maji kwa mbali kuchunguza bomba.
Mtaalamu wa kampuni ya kutambua kwa mbali, Sergio Volkmer, anasema "haijatengenezwa kwa maua ya mwani" lakini kutoka kwa kitu kilicho chini ya uso, kama vile mchanga au kioevu kinachotolewa ndani ya nchi.
Bomba hilo hilo la kijani kibichi linaonekana kwenye picha ya kwanza kabisa ya setilaiti ambayo BBC inaweza kuipata, kuanzia 1985, ikionesha kwamba kituo cha mafuta kinaweza kuwa kimekuwa kikimwaga "maji yaliyotengenezwa" kwenye Bahari Nyekundu kwa miongo kadhaa. Bado inaonekana kwenye picha ya hivi karibuni ya kituo, kuanzia Septemba 2022.
Dkt. Asner, mwanaikolojia wa Chuo Kikuu cha Jimbo la Arizona, pia alichunguza eneo hilo kwa kutumia Allen Coral Atlas, zana ya satelaiti wa ambayo inachunguza miamba ya matumbawe.
Anasema ingawa kuna dalili za mfumo wa ikolojia unaostawi katika kila upande wa eneo lililoathiriwa, "ghafla unaweza kuona ni vigumu kuona kupitia maji" kwa sababu ya "kitu juu ya uso wa maji ambacho kinaonekana kama uchafuzi wa mazingira".
Dkt. Gera Troisi, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Brunel London ambaye anachunguza athari za sumu kwa viumbe, anasema viambata vilivyo katika "maji yanayozalishwa" vinaweza kukabiliana na maji ya bahari, kunyonya oksijeni, na kutosheleza hata viumbe vya baharini vinavyostahimili zaidi.
"Tunawakosesha hewa na kuwakinga kutokana na mwanga kwa sababu ya haya yote ," anasema.
Umoja wa Mataifa umeonya kwamba ikiwa wastani wa joto duniani utaongezeka kwa 1.5C, 90% ya matumbawe ya dunia yataangamizwa.
Lakini licha ya joto la bahari kupanda kwa kasi katika Bahari Nyekundu kuliko kiwango cha wastani cha kimataifa, "matumbawe makubwa" ya eneo hilo hadi sasa yameonekana kustahimili athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Wanasayansi wengine wanaamini matumbawe ya Bahari Nyekundu yanaweza kushikilia siri ya kuokoa matumbawe kote ulimwenguni.
Mmoja wao, mtaalamu wa masuala ya bahari Sylvia Earle, anasema utafiti zaidi unahitajika ili kujua ni nini kinachofanya matumbawe haya kuwa katika hatari. Lakini anasema ni "umuhimu mkubwa kwa jumuiya ya kimataifa kwa sababu ya uwezekano wa kupandikiza matumbawe kutoka Bahari ya Shamu ili kurekebisha miamba iliyoharibiwa katika sehemu nyingine za dunia, kama vile Great Barrier Reef".
Licha ya kufunika 0.1% tu ya bahari, miamba ya matumbawe ni nyumbani kwa 30% ya viumbe hai vya baharini.
Katika Bahari Nyekundu, wao ni tegemeo kwa viumbe walio hatarini kutoweka kama vile kobe wa hawksbill, pamoja na kusaidia uvuvi, kilimo cha baharini na utalii - ambao hutoa mapato kwa mamilioni ya Wamisri.
Wanasayansi, nchini Misri na kimataifa, wamependekeza eneo ambalo Gupco inafanya kazi lijumuishwe katika eneo jipya la ulinzi wa baharini katika Bahari Nyekundu, ili kujumuisha eneo lote linalojulikana kama Great Fringing Reef.
Hivi sasa takriban 50% ya miamba iko kwenye eneo hilo. Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) zilitarajia nyongeza hiyo itatangazwa na wizara ya mazingira ya Misri katika COP27.
Lakini hadi sasa hakuna tangazo lililotolewa. Kampuni za mafuta, Shell na Chevron, zimefanya uchunguzi wa hivi majuzi wa visima vipya vya mafuta na gesi umbali wa kilomita 30 kutoka sehemu zilizohifadhiwa za Great Fringing Reef, (miamba ambayo hukua karibu sana na ufuo )