Tetesi za soka Ulaya Jumatano 11.10.2023

Chanzo cha picha, Getty Images
Mjumbe wa bodi ya Real Madrid anasema anatumai mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe atachagua kujiunga na klabu hiyo ya Uhispania wakati mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 na Paris St-Germain utakapokamilika msimu ujao wa joto. (AS, kupitia Remontada Blanca – In Spanish)
Manchester City wana nia ya kumpa fowadi wao wa Norway Erling Haaland, 23, kandarasi mpya ambayo itaondoa kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 173 na kupunguza hofu kwamba Real Madrid au Barcelona wanaweza kumchukua. Haaland ana mabao 44 katika mechi 43 za Premier League. (Gazzetta dello Sport)
Manchester United wamemuongeza mlinzi wa Sporting Lisbon na Ureno Goncalo Inacio, 22, kwenye orodha ya wachezaji wanaolengwa huku wakipania kuimarisha safu yao ya ulinzi msimu ujao. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Manchester City Kalvin Phillips anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo mwezi Januari, huku Newcastle United na Everton zikiwa miongoni mwa wanaomtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27. (Subscription Required)
Arsenal imekuwa ikifanya kazi ya kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney kutoka Brentford na mazungumzo yamefanyika kati ya klabu hizo mbili, huku Chelsea pia wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (TeamTalks)
Jamaica inaweza kumpa mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood, 22, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Getafe ya Uhispania fursa ya kurejea katika soka ya kimataifa - miaka mitatu baada ya kucheza soka la juu Uingereza. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumnunua winga wa Borussia Dortmund na England mwenye umri wa miaka 19 Jamie Bynoe-Gittens. (Bild – In Deutsch)
Manchester City wanavutiwa na kiungo wa kati wa Ujerumani Joshua Kimmich na Bayern Munich huenda wakalazimika kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ikiwa hataongeza mkataba wake zaidi ya 2025. (90 Min).
Winga wa Manchester United na England Jadon Sancho, 23, yuko tayari kuhama mwezi Januari huku Juventus na Borussia Dortmund - klabu yake ya zamani - zote zikivutiwa. (Subscription Required)

Chanzo cha picha, PA Media
Inter Milan wamekataa uhamisho wa Januari wa kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Albania Armando Broja, 22. (Fabrizio Romano)
Meneja wa zamani wa Chelsea na Tottenham Antonio Conte yuko tayari kuchukua nafasi ya meneja wa Napoli ikiwa mabingwa hao wa Serie A watamfukuza Rudi Garcia. (Calciomercato – In Itali )
West Ham wanapanga kufanya mazungumzo kuhusu mkataba mpya na mlinzi wa Ufaransa Kurt Zouma, 28, ambaye mkataba wake unakamilika 2025. (Teamtalk).












