Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Chef Ali: Mpishi aliyejizolea umaarufu mitandaoni kutokana na upishi wake
Iliyochapishwa
Ali Said Mandhry amejizolea umaarufu katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari katika tasnia ya upishi kutokana na utofauti wake.
Chef Ali kama anavyofahamika kwa umaarufu hupika vyakula vya asili kama vya Uswahilini, Kiafrika, Kiarabu, Kireno, Kihindi, Kizungu, na vya kichina.
Chef Ali amezungumza na mwanahabari wa BBC Roncliffe Odit kuhusu safari yake, ufanisi wake, ujumbe alionao kwa wanaotazamia kubobea na kuwa kama yeye au hata zaidi.