Daktari wa 'mchongo' agunduliwa baada ya miaka 43

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Tunapokuwa na shida au ugonjwa wowote katika mwili wetu, tunatafuta daktari mara moja. Tunaamini na kufuata maagizo yaliyowekwa na madaktari.
Je, itakuwaje ikiwa daktari aliyetibu maelfu ya wagonjwa - atabainika sio daktari wa kweli? Kesi hiyo imetokea huko Ahmedabad, Gujarat. Mahakama imemtia hatiani mtu aliyejifanya daktari.
Kujiunga na Chuo

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Katika jimbo la Gujarat, Julai 1980. Utpal Ambubai Patel mwenye umri wa miaka 17 alikuwa amewasilisha maombi mawili ya kujiunga na kozi ya udaktari katika chuo cha matibabu.
Katika moja ya maombi, Utpal aliambatanisha cheti cha masomo chenye alama 48%.
Lakini ombi lake lilikataliwa na usimamizi wa chuo cha kitabibu. Kwa mujibu wa sheria zilizokuwepo wakati huo, kiwango cha chini cha alama 55% kilihitajika ili kuingia kwenye kozi ya matibabu.
Siku chache baada ya ombi la kwanza kukataliwa, Utpal aliwasilisha ombi jingine. Cheti kipya na daraja lake limeongezeka.
Cheti kipya cha alama kilionyesha kuwa Utpal amepata asilimia 68% ya ufauli. Kwa sababu hiyo aliitwa kwa ajili ya usaili na kupewa nafasi katika kozi ya matibabu.
Alijiunga na mwaka wa kwanza wa kozi ya shahada ya kwanza ya udaktari.
Baada ya miaka 43

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Hata baada ya kuandikishwa, Utpal alikumbana na changamoto kadhaa. Kwa vile cheti alichotumia kuomba kujiunga na chuo ilikuwa na mashaka, mkuu wa chuo wakati huo alimtumia notisi akitaka maelezo.
Utpal Patel alimaliza masomo yake ya chuo na kuanza kufanya kazi ya udaktari huku uchunguzi ukiendelea.
Uchunguzi uliofanywa na wasimamizi wa chuo ulibaini kuwa cheti cha kilichotolewa na Utpal kwa ajili ya kujiunga na kozi hiyo kilikuwa ghushi na cheti chake cha kweli alikuwa amepata alama ya chini.
Baadaye, malalamiko yaliwasilishwa kwa polisi dhidi ya Utpal kwa niaba ya uongozi wa chuo mwaka 1991; kwa kujiandikisha katika masomo ya matibabu kwa kutoa hati bandia na kesi ilisajiliwa chini ya vifungu vitatu.
Kwa msingi wa mashahidi tisa na ushahidi wa maandishi katika kesi hii, korti ilisema mshtakiwa alitumia cheti cha kughushi kujiunga na kozi ya udaktari.
Daktari alishtakiwa akiwa na umri wa miaka 61, yaani miaka 43 baada ya kuanza kufanya kazi. Hakimu Mkuu wa Metropolitan Pawan, Kumar M. Naveen alimhukumu Utpal katika kesi hii.
Kifungo na Faini

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
“Mwanafunzi mwingine anayestahili amenyimwa fursa kutokana na vitendo vya mshtakiwa. Ni lazima adhabu kali itolewe" hoja kali ziliwasilishwa na serikali.
“Wakati mshitakiwa hana sifa, kitendo chake kimechukua nafasi ya mtu mwingine mwenye sifa, kitendo hicho ni kinyume na jamii. Ni jukumu la korti kuhakikisha kuwa kesi kama hizo hazijirudii tena,” mahakama ilisema katika uamuzi wake.
Akizungumza na BBC kuhusu maelezo ya kesi hii, Mwendesha Mashtaka wa Umma Prajapati alisema, "Utpal Patel amepata alama za asilimia 48 pekee katika mtihani wa sayansi. Baada ya hapo, alighushi cheti kingine cha alama ili ajiunge na chuo cha matibabu. Hukumu hiyo inategemea mashahidi na hati 39 zilizowasilishwa katika kesi hiyo."
Akizungumzia hoja nyingine zilizowasilishwa mahakamani hapo, alisema, “tumebishana kuwa nafasi ya daktari ina thamani katika jamii. Kwa hivyo hatua za mfano zichukuliwe katika kesi hii na adhabu ya juu itolewe. Mshtakiwa hawezi kuachiliwa kwa sababu ni mzee.”
Mahakama ilimhukumu Utpal Patel faini ya rupia 10,000 kwa kila kosa na kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuandikisha kozi ya matibabu kwa kutoa cheti bandia.















