Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 22,06.2024
Manchester United wamefanya mawasiliano ya awali na Lille kuhusu usajili wa beki wa Ufaransa Leny Yoro, 18. (Sky Sports)
Wolves wanataka hadi £45m kwa Max Kilman kufuatia ofa ya West Ham ya £25m kwa mlinzi huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27. (Guardian)
Manchester United na Tottenham wanamtaka Jonathan David wa Lille, Wolves wakitaka pauni milioni 45 kwa ajili ya Max Kilman, huku Douglas Luiz anakaribia kuondoka Aston Vila.
Manchester United na Tottenham ni vilabu viwili kati ya vilabu vinavyomhitaji mchezaji wa Canada mwenye umri wa miaka 24 na mshambuliaji wa Lille Jonathan David. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 26, anakaribia kuhama kutoka Aston Villa kwenda Juventus , huku Villa ikipokea winga Mwingereza Samuel Illing-Junior, 20, na kiungo wa kati wa Argentina Enzo Barrenechea, 23, pamoja na ada ya uhamisho ya £25m. (Mail)
Lazio wako tayari kumpa mlinda lango wa Ugiriki Christos Mandas, 22, pamoja na ada ya pauni milioni 15 katika jitihada zao za kumsajili mshambuliaji Muingereza Mason Greenwood, 22, kutoka Manchester United . (Il Messaggero - in Italian)
Southampton wanapanga kumnunua winga wa Jamaica na Fulham Bobby De Cordova-Reid, 31, ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu wa joto. (JSun)
Beki wa Manchester United na England Aaron Wan-Bissaka, 26, anakaribia kuhamia Galatasaray na atapewa mkataba wa miaka minne na timu hiyo ya Uturuki. (Bein Sports Turkey - in Turkish)
Chelsea na Bayern Munich zote zinaonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa Barcelona Mhispania Marc Guiu, 18 , ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro 6m (£5.08m). (Fabrizio Romano)
West Ham na Nottingham Forest wamewasiliana na Arsenal kuhusu uwezekano wa kumnunua winga wa Uingereza Reiss Nelson, 24 (Football Insider)
Manchester United wana wasiwasi kwamba hawataweza kumnasa Rennes mwenye umri wa miaka 19, Desire Doue kwenda Old Trafford, huku klabu hiyo ya Ufaransa ikiweka bei ya juu inayomtaka kiungo huyo. (Givemesport)
West Ham na Brentford wameonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa zamani wa Everton Dominic Calvert-Lewin, 27. (FootballTransfers)
Roma wako tayari kufanya mazungumzo na Manchester City huku wakitafuta njia za kumnunua mlinzi wa Uhispania Sergio Gomez, 23. (Caughtoffside).
AC Milan wanavutiwa na kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 28. (Corriere dello Sport via Football Italia.)
Everton wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Senegal Illian Ndiaye, 24, kutoka Marseille . (L'Equipe - in French)
Bayern Munich wako kwenye mazungumzo na Paris St-Germain kujaribu kumsajili kiungo wa kati wa Uholanzi Xavi Simons, 21. (Sky Sports Germany).
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi