Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 18.10.2024

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anaweza kusaini nyongeza ya kandarasi yake hata kama klabu hiyo itashindwa katika vita vyake vya kisheria dhidi ya madai 115 ya ukiukaji wa sheria za kifedha. (Athletics)

Mkufunzi wa Sporting Ruben Amorim, 39, na kocha mkuu wa Bayer Leverkusen Mhispania Xabi Alonso, 42, wanaongoza kwenye orodha ya Manchester City kuchukua nafasi ya Guardiola iwapo ataamua kuondoka. (mail),

Barcelona ilikataa ofa ya euro 250m kutoka kwa Paris St-Germain msimu wa joto kwa winga wao wa miaka 17 raia wa Uhispania Lamine Yamal. (Goal),

Arsenal na Manchester City ni miongoni mwa mashabiki wa kiungo wa kati wa Atalanta na Ubelgiji Charles de Ketelaere, 23. (Caught Offside),

Mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag ana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 27, mwezi Januari anapojaribu kujenga upya safu yake ya kati (Sport – In Spanish),

Manchester United wanavutiwa na mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 21, ambaye anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Bundesliga msimu ujao. (Barua – Subscription Required)

Beki wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Jonathan Tah, 28, na mlinzi wa kushoto wa Bayern Munich Alphonso Davies, 23, na fowadi wa Lille na Canada Jonathan David, 24, wanafuatiliwa na Barcelona. (Mundo Deportivo – In Spanish)

Kiungo wa kati wa Chelsea Cesare Casadei, 21, ameshauriwa na mkufunzi wa Italia wa wachezaji walio chini ya umri wa miaka 21 Carmine Nunziata kuzingatia mustakabali wake wa Blues mwezi Januari ikiwa hatapata muda wa kucheza. (Radio Rai 1 via Metro)

Mkufunzi mpya wa England Thomas Tuchel anaweza kutafuta ushauri kwa wafanyikazi katika klabu yake ya zamani Chelsea, huku Mjerumani huyo, 51, akitamani kuunda timu mpya ya wahudumu ambayo anaiamini. (Mail)

imetafsiriwa na Seif Abdalla