Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 30.01.2023
Chelsea wamefufua tena mazungumzo na Benfica ili kujaribu kumsajili kiungo wa kati wa Argentina Enzo Fernandez, 22, kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa Jumanne. (Telegraph - usajili unahitajika)
Tottenham wamewasilisha ofa ya maneno ya euro 25m (£22m) kwa Bayer Leverkusen kwa ajili ya uhamisho wa beki wa kati wa Ecuador Piero Hincapie, 21. (Bild - kwa Kijerumani).
Nottingham Forest wako mbioni kumsajili kiungo wa kati wa Newcastle United Muingereza Jonjo Shelvey, 30. (Telegraph - usajili unahitajika)
Barcelona wanamfuatilia mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ureno Joao Felix, 23, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Chelsea. (Sport - kwa Kihispania)
Inter Milan wanamtaka mlinzi wa Manchester United na Uswidi Victor Lindelof, 28, kama mbadala wa Milan Skriniar ikiwa beki huyo wa Slovakia mwenye umri wa miaka 27 atahamia Paris St-Germain. (Fabrizio Romano)
Tottenham wanashughulikia mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Birmingham City Muingereza Jobe Bellingham, 17, kakake kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham, 19. (Football Insider)
Galatasaray wanaongoza katika harakati za kumsajili beki wa Liverpool Muingereza Nat Phillips, 25, ambaye thamani yake ni £10m. (Athletic -Usajili unahitajika)
Everton wanapania kumsajili mshambuliaji na pia mlinzi wa Udinese kutoka Brazil mwenye umri wa miaka 27 Rodrigo Becao. (Mail)
Nottingham Forest wapo kwenye mazungumzo ya juu kumsajili kipa wa Paris St-Germain na Costa Rica Keylor Navas, 36. (Football Insider)
Sporting Lisbon wanakaribia kufikia kumsajili kwa mkopo wa beki wa Barcelona na Uhispania Hector Bellerin, 27, kama mbadala wa mlinzi wa Uhispania Pedro Porro, 23, ambaye Tottenham wanatarajia kumsajili. (Atheletic-Usajili unahitajika)
Manchester City itapambana na Barcelona katika kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa Girona na Uhispania mwenye umri wa chini ya miaka 21 Arnau Martinez, 19. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
Sevilla wako kwenye mazungumzo ya juu ya kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Bryan Gil, 21, kutoka Tottenham kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Fabrizio Romano)
Newcastle United wamekubali ada ya takriban £3m kwa ajili ya beki wa West Ham na Scotland aliye na umri wa chini ya miaka 21 Harrison Ashby, 21. (Times - usajili unahitajika)