Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Frank Lampard: Kipi kimemuendea kombo kocha huyu aliyetimuliwa Everton?
Klabu ya Everton imemfukuza kazi kocha wake Frank Lampard baada ya kuwa na klabu hiyo inayotumiwa uwanja wa Goodison Park kwa muda usiozidi mwaka mmoja. Kichapo kutoka West Ham United Jumamosi kilikuwa kipigo cha tisa kwa Everton katika mechi 12 za Ligi kuu England.
Kwa sasa Everton iko nafasi ya pili kutoka mkiani wakiwa na alama 15 katika mechi 20, juu ya Southampton kwa tofauti ya mabao.
Kiungo wa kati wa zamani wa Uingereza Lampard, 44, alichukua nafasi ya Rafael Benitez mnamo Januari 2022 akikuta timu ikiwa katika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi na kusaidia Everton kuepuka kushushwa daraja.
Everton sasa wanatafuta meneja wao wa sita wa kudumu katika kipindi cha miaka mitano. Klabu hiyo ilimshukuru Lampard na wakufunzi wake "kwa huduma yao katika kipindi ambacho kimekuwa cha changamoto kwa miezi 12". "Kujitolea na kujitoa kwa Frank na wasaidizi wake kumekuwa mfano wa kuigwa katika muda wote wa klabu, lakini matokeo ya hivi karibuni na msimamo wa sasa wa ligi unasukumua uamuzi huu mgumu kuchukuliwa," iliongeza taarifa ya klabu.
Makocha wasaidizi Joe Edwards, Paul Clement, Ashley Cole na Chris Jones pia wameondoka Everton, lakini Alan Kelly anaendelea kuwa kocha wa makipa.
Everton walisema "wameanza mchakato wa kupata meneja mpya". Meneja wa zamani wa Leeds United Marcelo Bielsa yuko kwenye orodha ya wanaowania kumrithi Lampard.
Kipi kilichokwenda kombo kwa Lampard?
Ni matokeo mabaya tu aliyoyapata akiwa na Everton. Baada ya sare ya 1-1 na mabingwa watetezi Manchester City, Disemba 31 Everton walifungwa 4-1 na Brighton katika uwanja wa Goodison Park, wakatupwa nje ya Kombe la FA kwa kuchapwa mabao 3-1 na Manchester United na kisha kufungwa na Southampton licha ya kwamba walitangulia kufunga wakachapwa 1-2. Pia wakachapwa 2-0 mwishoni mwa wiki na West Ham.
Wamefanikiwa kushinda mara tatu pekee msimu mzima. Kumekuwa na makelele kutoka kwa mashabiki dhidi ya bodi katika michezo ya hivi karibuni, na walionekana kutaka kuonesha hasira zao kama wangefungwa na Southampton.
Bodi ya wakurugenzi ya Everton ilikosa mchezo huo kwa sababu ya kile klabu ilidai kuwa "tishio la kweli na la kuaminika kwa usalama wao".
Polisi wa Merseyside walisema hakuna vitisho au matukio yoyote yaliyoripotiwa kwa maafisa wao kabla ya mechi na kabla ya Everton kutangaza "taratibu zilizoimarishwa za usalama" zitawekwa.
Hilo pia lilikuwa ni jibu kwa baadhi ya mashabiki waliokuwa waliomvaa beki Yerry Mina na kiungo Anthony Gordon walipokuwa wakiondoka Goodison Park wakiwa kwenye magari yao mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mmiliki wa Everton, Farhad Moshiri alihudhuria mchezo wake wa kwanza baada ya miezi 14 huko West Ham, pamoja na mwenyekiti wa muda mrefu Bill Kenwright. Moshiri alipoulizwa na Sky Sports kwenye mchezo huo, alisema kwamba haikuwa chini yake kuamua juu ya mustakabali wa Lampard.
Klabu hiyo bado haijasajili mchezaji yeyote katika dirisha la Januari lakini ilitumia zaidi ya pauni milioni 80 msimu wa joto, ikiwa ni pamoja na kumsajili Amadou Onana kutoka Lille kwa pauni milioni 33 na kumnunua Dwight McNeil kutoka Burnley kwa pauni milioni 20, baada ya kupokea pauni milioni 60 kutoka Tottenham, kwa kuwazuia mshambuliaji wa Brazil Richarlison.
Rekodi isiyofurahisha ni msumari mwingine kwa Lampard
Lampard alianza ukocha akiwa na Derby mnamo 2018. Katika msimu wake mmoja wa kuinoa timu hiyo, walifika fainali ya mchujo wa kuwania kupanda ligi kuu, ambapo walipoteza kwa Aston Villa.
Baadaye akaenda kuchukua nafasi ya Maurizio Sarri kama meneja wa Chelsea mnamo Julai 2019, lakini alifutwa kazi baada ya miezi 18.
Lampard apata nafasi Goodison huku Everton ikiwa nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi, alama sita kutoka mstari wa kushushwa daraja. Everton walipoteza mechi 10 katika mechi 18 zilizosalia za msimu huo, lakini walijihakikishia kunusurika kushuka daraja kufuatia ushindi wa 3-2 dhidi ya Crystal Palace kwenye kile Lampard alichoita "moja ya usiku mkubwa" wa maisha yake.
Lampard ameshinda mechi 12 pekee kati ya 44 katika mashindano yote akiwa na Everton, asilimia ya ushindi ya 27.27 ambayo ni mbaya zaidi kuliko rekodi yake huko Derby (42.1%) na Chelsea (52.4%)
Nani kumrithi na nini kinachofuata kwa Lampard?
Baada ya kuucheza mechi nane za ligi kuu bila ushindi Frank Lampard aanaondoka na kuwaacha The Toffees wakitafuta meneja wa saba wa kudumu tangu kuanza kwa msimu wa 2016.
Meneja wa zamani wa Leeds United Marcelo Bielsa anaongoza orodha ya makocha wanaojadiliwa kumrithi Lampard.
Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 67, ambaye anavutiwa na mmiliki wa Everton Farhad Moshiri, hajafanya kazi tangu atimuliwe na Leeds Februari mwaka jana, ingawa anasalia kuwa shujaa Elland Road kwa kuirudisha klabu hiyo kwenye Ligi kuu.
Inabakia kuonekana kama Bielsa atachukua kazi katikati ya msimu huku bosi wa zamani wa Burnley Sean Dyche akiwa pia kwenye orodha hiyo ya kujadiliwa.
Meneja wa zamani wa Southampton Ralph Hasenhuttl alijadiliwa na bodi ya Everton kabla ya kuteuliwa kwa Lampard mwaka mmoja uliopita naye anaweza kuchukua nafasi ya Lampard baada ya kuondoka St Mary's mnamo Novemba.
Mwingine anayevutia mashabiki wanaomvutia Goodison Park ni meneja wa West Bromwich Albion Carlos Corberan, ambaye ameleta mabadiliko The Hawthorns tangu kuteuliwa kwake Oktoba.
Wayne Rooney pia anapigiwa chapuo kuchukua nafasi ya Lampard pale Evertona ambayo kwa sasa Paul Tait na Leighton Baines watasimamia timu hadi meneja mpya atakapoteuliwa.