Slap Kabaddi: Ni mchezo gani huu wa kuzabana makofi?

Slap Kabaddi: Ni mchezo gani huu wa kuzabana makofi?
Iliyochapishwa

Slap Kabaddi, mchezo unaofanana na mieleka unaohusisha kupiga makofi, unazidi kuwa maarufu huko Punjab, Pakistan.

Kabaddi ni mchezo maarufu wa mawasiliano huko Asia Kusini.

Wachezaji hupata alama kwa kuvamia uwanja wa wapinzani na kuwagusa wapinzani wengi iwezekanavyo bila kuishiwa na pumzi.

Mtindo mpya, Slap Kabaddi, pia unajulikana kama Thappad Kabaddi unahusisha kuwazaba makofi wachezaji wa timu pinzani na kwa kawaida huchezwa katika sherehe katika mkoa wa Punjab.