Kundi la Wagner bado linasajili wapiganaji licha ya uasi - Utafiti wa BBC

ggg

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Ofisi za Wagner za kuajiri zinafanya kazi kama kawaida
Iliyochapishwa

Kundi la Wagner bado linasajili wapiganaji kote Urusi, ikiwa ni siku chache baada ya kufanya uasi ambao ulisababisha Vladimir Putin kupata hofu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kwa kutumia namba ya simu ya Urusi, BBC ilipiga simu kwenye vituo zaidi ya kumi na mbili vya kuandikisha watu kuajiriwa tukisema kuwa tunaulizia kwa niaba ya ndugu.

Wale wote waliojibu walithibitisha kuwa utaratibu unaendelea kama kawaida.

Kutoka Kaliningrad upande wa magharibi hadi Krasnodar kusini, hakuna mtu aliyeamini kuwa kikundi hicho kilikuwa kinasambaratishwa.

Katika jiji la Arctic la Murmansk, mwanamke mmoja katika klabu ya michezo ya Viking alithibitisha kwamba bado alikuwa akisajili wapiganaji wa Ukraine.

"Hapo ndipo tunaandikisha watu, ndio. Mtu akitaka kwenda lazima anipigie tu na tutapanga siku."

Orodha ndefu ya vituo vya Wagner vya mawasiliano hutegemea zaidi klabu za mapigano, ikijumuisha shule za karate na vilabu vya ngumi.

Watu kadhaa ambao walipokea simu walisisitiza kwamba wanachama wapya walikuwa wakisaini mikataba na kundi la mamluki lenyewe, sio wizara ya ulinzi ya Urusi.

WAGNER GROUP

Chanzo cha picha, WAGNER GROUP

Maelezo ya picha, Mawasiliano ya ofisi za Wagner za kuajiri bado ziko mtandaoni na kusisitiza kuwa biashara inaendelea kama kawaida

"Haihusiani kabisa na wizara ya ulinzi," mwanamume mmoja katika klabu ya michezo wa Sparta huko Volgograd alisisitiza. "Hakuna kitu kimesimama, bado tunasajili."

Takwa la mamluki hao kuhamishwa hadi wizara ya ulinzi, na hivyo kuwafanya Wagner Group na bosi wake Yevgeny Prigozhin kupigwa chini, ilikuwa mzizi wa mabishano makali ambayo yalizuka katika ghasia za mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ilikuwa changamoto kubwa zaidi kwa mamlaka ya Rais Putin katika utawala wake wa zaidi ya miaka 20, licha ya Kremlin kuhangaika tangu wakati huo kufafanua upya jibu lake kama mwenye nguvu na maamuzi.

Na bado kesi ya jinai dhidi ya waasi imetupiliwa mbali, katika nchi ambayo wanaharakati wengi wa upinzani wanatumikia vifungo virefu kwa sababu tu ya kuzungumza dhidi ya vita vya Urusi dhidi ya Ukraine

ggg

Chanzo cha picha, Matthew Goddard

Maelezo ya picha, Sarah Rainsford alipiga simu zaidi ya ofisi kumi na mbili za kuajiri Wagner (picha: Matthew Goddard)
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hata kiongozi wa Wagner ameruhusiwa kuondoka, akielekea Belarusi - ingawa ndege ya binafsi ya Prigozhin ilifuatiliwa ikirejea Urusi Jumanne usiku.

Na jeshi lake, ambalo lilienda Moscow na kushambulia helikopta na ndege kutoka angani, bado halijavunjwa.

"Tunafanya kazi. Ikiwa kitu kingebadilika, wangetuambia. Lakini hakuna chochote," mwajiri wa kike huko Krasnodar, kusini mwa Urusi, aliweka wazi.

Mshahara wa mpiganaji wa Wagner unasalia kuwa pesa ya Urusi rubles 240,000 (£2,175) kwa mwezi; mikataba ni ya miezi sita.

Siku ya Alhamisi, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi katika bunge la Urusi alisema kuwa Prigozhin alionywa mapema kwamba tarehe ya mwisho ya Wagner uliyopitishwa na wizara ya ulinzi haiwezi kujadiliwa.

"Wizara ya ulinzi ilisema makundi yote…lazima yatie saini mikataba, na wote wakaanza kufanya hivyo. Kila mtu isipokuwa Bw Prigozhin," Andrei Kartapolov alitoa maoni, akimaanisha uasi wake kama kitendo cha uhaini.

"Alifahamishwa kwamba Wagner hatashiriki katika Operesheni Maalum ya Kijeshi," alitumia usemi wa Urusi kwa vita vyake dhidi ya Ukraine. "Pia haitapata fedha au rasilimali."

Vladimir Putin, ambaye ametumia miaka mingi kukataa uhusiano wowote rasmi na Wagner, alibadilisha ghafla kufuatia uasi huo. Inaonekana akijaribu kupunguza ukubwa wa Yevgeny Prigozhin, aliyedai kuwa kikundi hicho kilifadhiliwa na serikali ya Urusi kwa 100%.

Utendaji wa kuishi kwa Wagner, basi, hauko wazi.

Siku ya Jumamosi, Putin alitia saini sheria ambayo inamaanisha ni wizara ya ulinzi pekee ambayo sasa inaweza kuajiri katika magereza ya Urusi, ambayo hapo awali yalikuwa chanzo kikuu cha wapiganaji wa Ukraine kwa Wagner.

Lakini mpango kikundi hiko kuajiri bado unaendelea.

Huko Volgograd, mtu tuliyezungumza naye alisema kwamba ikiwa mtu amejiandikisha leo, "Ninaweza kumpeleka kesho," na akathibitisha kwamba Belarusi sasa ndio linalowezekana.

Mapema wiki hii, kiongozi wa muda mrefu wa Belarus Alexander Lukashenko - ambaye amefurahi kuelezea jukumu lake la upatanishi na kumalizika kwa uasi wa Jumamosi - alisema kuwa wapiganaji wa Wagner wanakaribishwa huko.

Alipendekeza jeshi la Belarusi lilikuwa na mengi ya kujifunza kutoka kwao.

ggg

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Alexander Lukashenko alitoa maelezo ya kina wiki hii jinsi alivyomshawishi Prigozhin kukomesha uasi wake.

Mwanachama wa Kibelarusi wa Wagner ambaye alijulikana kwa jina alilosaini kama "Brest" alidokeza kwamba kundi hilo litakuwa ulinzi mzuri kwa Bw Lukashenko kabla ya uchaguzi wa bunge mwaka ujao, kama kutakuwa na maandamano makubwa zaidi katika utawala wake wa kimabavu.

Katika video iliyowekwa kwenye Telegramu na kurekodiwa katika eneo lisilojulikana, "Brest" pia iliwakumbusha waliojiandikisha kuwa mpaka wa Belarusi ulikuwa "chini ya 300km kutoka Kyiv". Ilikuwa ni tishio jembamba.

Bado hakuna dalili kwamba wapiganaji wa Wagner wanahamia Belarusi.

"Kila kitu ni sawa na hapo awali, kwa sasa. Hakuna kilichobadilika," alisema mwanamke mmoja huko Saratov, katikati mwa Urusi, akithibitisha kwamba bado alikuwa akiandikisha wanaume kupigana nchini Ukraine.

"Kila mtu huenda kwa Molkino, kama kawaida. Katika kituo cha mafunzo. Wanapata taarifa zote huko," aliongeza, akimaanisha safu ya ufyatuaji risasi iliyohusishwa hapo awali na Wagner kusini mwa Urusi.

Kwa hivyo chochote kitabadilika baada ya 1 Julai, nilijiuliza? "Sina matumaini. Sijui. Lakini watu bado wanawasiliana nasi, bila shaka."