Ndege ya Urusi ya II-22 iliodunguliwa na Wagner: Kipi cha kipekee kuihusu?

GGGG

Chanzo cha picha, MAXIM KUZOVKOV/TASS

Maelezo ya picha, Ndege aina ya IL-20
Iliyochapishwa

Uasi wa Wagner wa Juni 23 - 24, ulileta uharibifu katika kikosi cha anga cha Urusi. Kwa mujibu wa chanzo huru, helikopta mbili za kivita aina ya Ka-52 na Mi-35, helikopta tatu aina ya Mi-8MTPR, na gari moja la kijeshi la Mi-8, ya ulinzi aina ya II-22M imedunguliwa.

Taarifa hizi ziliripotiwa na wandishi habari wa Urusi na wana bloga. Kwa mujibu wa timu ya migogoro na intelejinsia, inawezekana kwamba helikopta nyingine aina ya Mi-8MTPR ilidunguliwa karibu na Ligansk Juni 23, ingawa hakuna taarifa za kutosha kuhusu tukio hili. Pia, haikuwa wazi ni watu wangapi walifariki.

Juni 24, video iliyochapishwa katika mtandao wa Telegram, ikidai ni tukio la ndege ikianguka na ikionesha eneo ilipoangukia. Ikiwa mabaki hayo ni kweli yanatokana na ndege iliyodondoshwa siku ya Jumamosi, picha moja inaonesha sehemu ya nyuma ya ndege ambayo ilidondoka wakati ikiwa angani.

Kwa kuzuitazama picha kutoka kutoka maeneo mbalimbali, ndege hiyo inaonekana ni kama ni ndege ya kambi ya Ivanovo-Severrny karibu na mji wa Ivanovo, pia ikaonekana Migalovo huko Tver. Ila haijulikani ni ndege inayomilikiwa na kikosi gani.

HDFJJSDHHS

Chanzo cha picha, TASS

Maelezo ya picha, Il-22 iliundwa kutoka ndege kongwe ya Il-18

IL-22 ilitengenezwa miaka ya 1970. Ili kusaidia kamandi ya kijeshi ya anga. IL-18, ni ndege yenye kuaminika iliyotengenezwa miaka ya 1958-1978. Mwaka 1970 aina hii ya ndege ilipangwa kuondoshwa katika matumizi ya kiraia na kutengenezwa kama ndege ya kijeshi.

Tangu wakati huo ndege kadhaa za kijeshi zimeundwa kutoka kwa mfumo wa II-18, ikiwemo ii-22M, pia ndege ya ulinzi dhidi ya nyambizi aina ya II-38. Ndege aina ya II-20 moja wapo ilidunguliwa na ulinzi wa anga wa Syria 2018.

wakati wa marekebisho eneo la abiria liliondoshwa kabisa, na vifaa maalumu viliwekwa. Pia, katika ii-22M kamandi ya rubani iliwekwa. Kwa jumla dazeni tatu ya ii-22 zimetengenezwa tangu 1970. Zimeboreshwa mara kwa mara.

Kwa mujibu Military Balance 2022, mwanzoni mwa vita vya Urusi na Ukraine, kulikuwa na ndege aina ya II-22M na 10 aina ya II-22. Ndege moja iliharibiwa wakati wa mapigano. Gazeti la Urusi la Moskovsky Komsomolets liliandika Oktoba 2022, kwamba II-22 ilipigwa na ulinzi wa anga wa Ukraine na kuharibiwa. Na haikuweza kurudi katika kambi.

Helikopta za vita

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Helikopta mbili zilizodondoshwa ni pigo kuwa kwa vita vya anga vya Urusi. Mi8MTPR-1 ni toleo la karibuni zaidi katika kiwanda cha uzalishaji wa helikopta za kivita. Helikopta hiyo imewekewa vifaa vya kieletroniki, ambavyo vimetengenezwa ili kwa mapambano ya chini na rada, ulinzi wa anga na silaha. Pia, helikopta hiyo hukusanya taarifa za kiintelejinsia.

Urusi kikawaida huzingatia sana vifaa vya kieletroniki, na helikopta hizi zimekuwa muhimu katika vita vya sasa. Military Balance inasema, helikopta za aina hiyo hazikuzidi 30 hadi 2022, ila inawezekana nyingine zilitengenezwa wakati vita vimeanza.

Helikopta mbili kudunguliwa na wanamgambo sio hasara ya kwanza kwa Urusi kwa helikopta ya aina hiyo. Mei, helikopta mbili za aina hiyo zilidunguliwa katika mkoa wa Bryansk. Mazingira ya tukio hilo hayako wazi. Kwa mujibu wa simulizi moja, ilidunguliwa ulinzi wa anga wa Ukraine na wengine wasema ilidunguliwa na Urusi kwa bahati mbaya.

Mashambulizi dhidi ya Ka-52 na Mi-35, na ndege ya ndege ya usafirishaji ya kijeshi Mi-8, zimeundwa kwa vifaa vyenye thamani kubwa. Lakini katika vita ndege za aina hiyo mara nyingi huwa mstari wa mbele na hupata hasara.

Katika video inayoelezwa kuchukuliwa karibua na Voronezh, Ka-52 ikipaa kwa umbali wa chini ilidunguliwa, kwa ulinzi wa anga unaodhani ni kutoka katika kombora la mkononi.

Mwandishi habari wa Chaneli One, Irina Kuksenkova aliandika katika akaunti yake ya Instagram kwamba, kombora la ulinzi wa anga la Wagner ndilo la kulaumiwa. Prigozhin alipoulizwa na makao makuu ya jeshi katika mkoa wa Kusini, alisema maofisi wa ulinzi wa anga walidungua kila kitu kinachopaa angani. Na hayo ndio maelezo yake.