Arsenal dhidi ya Man City - Nani atashinda EPL?

Iliyochapishwa

Kinyang'anyiro cha kuwania taji la Ligi Kuu kinakaribia mwisho wa ajabu tunapoingia katika miezi miwili ya mwisho.

Arsenal waliendeleza uongozi wao kileleni hadi pointi nane kwa kuwalaza Crystal Palace 4-1 Jumapili na wamebakia na michezo 10 huku wakitarajia kutamatisha miaka 19 ya kungoja ubingwa.

Manchester City wana mchezo mkononi lakini pia bado wako kwenye Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa, kumaanisha kuwa wanaweza kucheza mechi saba zaidi ya Arsenal.

Timu hizo mbili zitakutana katika mechi ambayo huenda ikawa muhimu katika Uwanja wa Etihad tarehe 26 Aprili.

Kwa hivyo ni nani anayependelewa kuchukua taji?

BBC Sport imepunguza namba na kuchambua orodha ya mechi ili kujaribu kujua kitakachojiri...

Je Arsenal na City wamesalia kucheza na nani?

Hebu tuanze na ratiba.

Mtazamo wa Arsenal ni rahisi: wanahitaji pointi 26 kutoka kwa mechi hizo 10 ili kutwaa ubingwa, ikizingatiwa kuwa City ni kushinda mechi zao zote zilizosalia.

Mechi ya mwisho ya Arsenal itakuwa nyumbani dhidi ya Wolves tarehe 28 Mei.

City inayonolewa na Pep Guardiola imesalia na mechi 11 lakini pia inakabiliwa na robo fainali ya Ligi ya Mabingwa mikondo miwili dhidi ya Bayern Munich na nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Sheffield United kwenye Uwanja wa Wembley.

Iwapo City watashinda zote mbili, fainali ya Kombe la FA itafanyika Juni 3 na nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa imepangwa kuchezwa 9/10 na 16/17 Mei, kabla ya fainali mjini Istanbul tarehe 10 Juni.

'Hiki ni kinyanganyiro cha ubingwa ambacho ni vigumu sana kutabiri'

Kulingana na utafiti na mifano ya kampuni ya Gracenote, Arsenal ya Mikel Arteta ina nafasi ya 53% ya kunyakua taji la Ligi ya Premia, wakati nafasi ya City kuhifadhi taji lao ni 47%.

"Licha ya Arsenal kuongoza kwa pointi nane, bado inakaribia asilimia 50/50 kwa sababu The Gunners wamecheza mchezo zaidi ya Manchester City na bado wanapaswa kucheza ugenini katika timu tatu kati ya sita bora: City, Newcastle United na Liverpool," Alisema Simon Gleave, mkuu wa uchambuzi wa michezo, Gracenote.

"Safari ngumu zaidi iliyosalia kwa City katika Ligi ya Premia ni kwenda kwa Brighton mwezi ujao.

"Ikiwa tutatumia uwezekano kutoka kipimo cha Klabu ya Euro kwa kila mechi iliyosalia kuhesabu pointi zinazotarajiwa kwa Arsenal na Manchester City mwishoni mwa msimu, Arsenal itamaliza na pointi 87 na City na pointi 86.

"Ikiwa tutatenga ushindi, sare au kushindwa kwa kila moja kati ya mechi zilizosalia zikiongozwa na uwezekano wa kipimo cha Klabu ya Euro, timu zote zitamaliza kwa pointi 88.

Vyovyote vile, hiki ni kinyang’anyiro kikali sana cha ubingwa kutabiri.

"Mechi kati ya wawili hao mnamo Aprili 26 itakuwa dhahiri kuwa mechi muhimu katika kuamua hatima ya Kombe la Ligi Kuu.

"Kwa msingi wa wastani wa asilimia 66 ya nafasi ya ushindi kwa City kulingana na kipimo cha Klabu ya Euro, tumeipa City pointi tatu.

Ikiwa Arsenal itaepuka kushindwa, au hata kushinda, hii itakuwa na athari kubwa kwenye kutafuta ubingwa."

Arsenal upande wao wana historia

Mashabiki wa Arsenal ambao wana ndoto ya kunyakua taji la kwanza tangu 2003-04 wanaweza kupata faraja kutokana na historia.

Kwa mujibu wa Opta, ni timu tatu pekee kwenye Ligi ya Primia ambazo zimeongoza kwa pointi nane au zaidi baada ya mechi 28 na hazijashinda taji hilo.

Msimu wa 1997-98 Manchester United iliiongoza Arsenal kwa pointi tisa baada ya kucheza michezo 30 lakini The Gunners, waliokuwa na michezo mitatu mkononi, waliziba pengo hilo na kufanikiwa kutwaa taji lao la kwanza la Premier League.

Miaka mitano baadaye Manchester United ililipiza kisasi kwa kufukuzia uongozi wa Arsenal kwa pointi nane baada ya michezo 29.

Lakini United walikuwa kwenye nafasi ya pili msimu wa 2011-12 wakati City ilipofuta kilichokuwa kinawaweka kifua mbele yaani pointi nane kabla ya kutwaa kombe siku ya mwisho kutokana na bao la Sergio Aguero.

Ukiangalia nyuma zaidi, kati ya timu 12 zilizo na pointi zaidi ya 69 baada ya kucheza mechi 30 za Ligi Daraja la Kwanza au Ligi Kuu (kubadilisha pointi tatu ili kupata ushindi) ni timu moja tu iliyoshindwa kutwaa ubingwa - Liverpool msimu wa 2018-19.

Kinyang’anyiro cha taji kinakwenda vizuri."

Beki wa zamani wa Arsenal Martin Keown kwenye MOTD 2: "Itakuwa ya kuvutia kuona jinsi kinyang’anyiro cha ubingwa kinavyokwenda kutoka sasa, lakini naweza kusema Arsenal wamefanya yote wanayoweza kufanya hadi sasa.

"Bado kuna kazi nyingi iliyosalia, lakini wametia pointi kibindoni kuendeleza uongozi huu na City italazimika kukabiliana na msongamano wa mechi ili kuwashika huku wakijaribu kushinda Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA pia."

Mlinzi wa zamani wa Wales Danny Gabbidon kwenye BBC Radio 5 Live: "Ni uwiano ambao timu hii ya Arsenal sasa inao. Ni mashine iliyo na mafuta vizuri. Kuna michezo mikubwa zaidi inayokuja, lakini wanaonekana wakiwa katika hali nzuri na mimi sifikirii kama wanaenda popote. Kinyang’anyiro cha taji kinakwenda vizuri."

Mwandishi wa habari Luke Edwards kwenye podcast ya kils siku ya BBC Radio 5 Live: "Arsenal inaonekana kama washindi wa taji na hio litakuwa matokeo mazuri kwa Ligi Kuu kwa sababu ni moja ya vilabu ambavyo havijashinda ligi kwa muda mrefu. "

Kiungo wa zamani wa Premier League, Nigel Reo-Coker kwenye Football Daily: "Kuitazama Arsenal hivi sasa ni kama kutazama Man City ya Pep miaka michache iliyopita wakati ilikuwa ya kuburudisha sana, ilikuwa inakuvutia kutaka kuitazama kwa sababu soka na mtindo kutoka mbele hadi nyuma ulikuwa wa kustaajabisha tu."