Afcon 2023: Ratiba, tarehe na droo za wachezaji wakiwemo Mohamed Salah na Andre Onana

Iliyochapishwa

Timu zinazoelekea Ivory Coast kwa fainali zimeshathibitishwa, lakini je unafahamu ni lini kombe la mataifa bingwa Afrika litachezwa na namna zinavyowaathiri wachezaji na vilabu katika ligi kuu ya England na kote duniani?

Kwa karibu mwezi mzima Januari na Februari, baadhi ya wachezaji nyota katika soka wanatarajia kushinda mashindano hayo yanayofanyika baada ya kila miaka miwili yanayoandaliwa na shirikisho la soka Afrika (Caf).

Mabingwa watetezi Senegal wanaweza kurudi na nguvu mpya kupitia wachezaji kama Sadio mane wa klabu ya Al-Nassr na mchezaji mpya wa Chelsea Nicolas Jackson, huku nayo Misri, ambayo timu iliyowahi kupata ufanisi zaidi katika historia ya Afcon, ikijinyakulia mataji saba, wanaongozwa na kapteni Mohamed Salah.

Haya ndio unayohitaji kuyajua kuhusu ratiba ikiwemo pia droo na lini wachezaji wanaweza kuondoka katika mashindano ya nyumbani.

Afcon 2023 itachezwa lini?

Awamu ya 34 ya mashindano ya Afcon titachezwa kuanzia Januari 13 hadi Februari 11 mwakani 2024.

Hii ni mara ya pili Ivory Coast inakuwa mwenyeji wa fainali hii baada ya kuzikaribisha tiu za Afrika mnamo 1984.

Mashindano haya yalipangwa awali kuchezwa Juni-Julai 2023, hatahivyo masihndano haya yalisukumwa mbele kutokana na hofu ya msimu wa mvua.

Licha ya kwamba yatachezwa mwakani 2024 bado jina la mashindano ni Afcon 2023.

Wenyeji watacheza mechi ya ufunguzi dhidi ya mpinzani kutoka kundi A atakayepambanishwa dhidi yao.

Timu mbili za juu na nne zitakazoichukua nafasi ya tatu kutoka makundi sita ya awali zitafuzu katika awamu ya mtoani, huku robo na nusu fainali zikifuata katika kutafuta mshindi wa nafasi ya tatu na baada yah apo fainali itafuta.

Fainali itachezwa Februari 11 katika uwanja wa Alassane Ouattara katika mji mkuu Abidjan.

Mechi za kufuzu

Mashindano haya yanajumuisha mataifa 24 kwa mara ya tatu baada kupanuliwa mnamo 2019.

Licha ya kwamba Ivory Coast ni wenyeji, bado walishiriki mechi za kufuzu na kumaliza katika nafasi ya pili baada ya Zambia katika kundi H.

Mataifa hayo mawili yanaungana na timu nyingine 22 zilizomaliza katika nafasi mbili za juu za mechi hizo za kufuzu kwenye makundi yao.

Timu zote zinazoshiriki zimecheza angalau mechi moja kati ya mbili zilizopita isipokuwa Zambia mabingwa wa 2012 wanaoshiriki kwa mara ya kwanza tangu 2015 na Msumbiji wanaoshiriki kwa mara ya tano na mara ya kwanza tangu 2010.

Jamhuri ya Afrika ya kati ilikosa fursa ya kushiriki mashindano hayo baada yakushindwa na Ghana.

Droo ya Afcon na inavyofanyika?

Droo ya mashindano haya itafanyika Abidjan Oktoba 12 saa moja usiku saa Uingereza sawa na saa nne usiku saa za Afrika Mashariki.

Kulingana na orodha ya dunia ya Fifa ya hivi karibuni timu hizo 24 zimegawanywa katika vyungu vinne. Licha ya Ivory Coast kuorodheshwa katika nafasi ya tisa bora Afrika, imejumuishwa kwenye chungu cha kwanza.

CHUNGU CHA KWANZA - Ivory Coast (*50), Morocco (13), Senegal (20), Tunisia (29), Algeria (34), Misri (35)

CHUNGU CHA PILI - Nigeria (40), Cameroon (41), Mali (49), Burkina Faso (58), Ghana (60), DR Congo (64)

CHUNGU CHA TATU- Afrika kusini (65), Cape Verde (71), Guinea (81), Zambia (82), Guinea ya Ikweta (92), Mauritania (99)

CHUNGU CHA NNE - Guinea-Bissau (106), Msumbiji (113), Namibia (114), Angola (117), Gambia (118), Tanzania (122)

(*Nafasi kwenye orodha ya Fifa kwenye mabano)

Timu hizo zitagawanywa kwenye makundi sita. Kabla ya droo hiyo mechi katika kila kundi itatengewa sehemu ya kuchezwa licha ya kwamba maelezo haya bado yanathibitishwa.

Viwanja sita katika miji mitano vitatumika:

  • Uwanja wa Alassane Ouattara, Abidjan (mashabiki 60,000)
  • Uwanja wa Felix Houphouet Boigny, Abidjan (mashabiki 33,000)
  • Stade de la Paix, Bouake (mashabiki 40,000)
  • Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly, Korhogo (mashabiki 20,000)
  • Uwanja wa Laurent Pokou, San Pedro (mashabiki 20,000)
  • Uwanja wa Charles Konan Banny, Yamoussoukro (mashabiki 20,000)

Shirikisho la soka Afrika Caf kwa kawaida huhakikisha inawakaribisha miamba ya soka Afrika wa zamani n awa sasa katika droo hiyo inayohudhuriwa na watu mashuhuri.

Mabingwa wa Ivory Coast kama Kolo na Yaya Toure wanatarajiwa kuhudhuria, wote wakiwa wameichezea timu hiyo ya taifa inayofahamika kama Tembo walipoifunga Ghana na kulichukua taji kwa mara ya pili mnamo 2015.