Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 07.09.2024
Newcastle wanaweza kutazama upya mpango wa kumnunua fowadi wa Nottingham Forest wa Uswidi Anthony Elanga, 22, mwezi Januari. (Football Insider)
Corinthians wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay, 30, ambaye ni mchezaji huru. (Globo - in Portuguese)
Liverpool wana nia ya kumpa mkataba mpya mlinzi wa Uholanzi Virgil van Dijk, 33, ili kuongeza muda wake wa kusalia Anfield zaidi ya msimu wa joto. (Football Insider)
Meneja msaidizi wa Stockport County Andy Mangan anatazamiwa kuwa mkufunzi wa Carlo Ancelotti katika klabu ya Real Madrid . (Athletic - subscription required)
Barcelona wanatazamiwa kufufua azama yao ya kumnunua mshambuliaji wa Athletic Bilbao Nico Williams, 22, raia wa Uhispania. (Sport - in Spanish)
Fenerbahce ya Jose Mourinho imekubali kumsajili kiungo wa kati wa Argentina Cristian Medina, 22, kutoka Boca Juniors mwezi Januari. (Fabrizio Romano)
Manchester United wanataka kuchukua nafasi ya kiungo Casemiro mwenye umri wa miaka 32 na Christian Eriksen, ambao wanachezea Brazil na Denmark mtawalia. (Givemesport)
Mshambulizi wa Nigeria na Southampton Paul Onuachu, 30, amekataa kuhamia Goztepe ya Uturuki. (Sabah - in Turkish)
Kiungo wa kati wa Croatia Mateo Kovacic, 30, anafikiria mustakabali wake Manchester City kufuatia kurejea kwa Mjerumani Ilkay Gundogan, 33, katika nafasi hiyo hiyo. (Football Insider)
Wadau wakuu wa Chelsea , Clearlake Capital na mfanyabiashara wa Marekani Todd Boehly, wanatathmini kama wanaweza kununuana. (Bloomberg - subscription required)
Clearlake Capital hawana nia ya kufanya chochote zaidi ya kuongeza dau lao kwa Chelsea . (Telegraph - subscription required)
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi