'Mwanangu hupigwa na kifafa zaidi ya mara 200 kwa siku'

'Mwanangu hupigwa na kifafa zaidi ya mara 200 kwa siku'
Iliyochapishwa

Tarehe 13 Februari Ulimwengu huadhimisha Siku ya Kifafa Duniani.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO, ugonjwa wa kifafa huathiri watu milioni 50 kote duniani, asilimia 80 wakiwa katika nchi zinazoendelea.

Hata hivyo asilimia 75 ya watu hao hukosa matibabu ya ugonjwa huu.

Fides Uiso @tanzaniaepilepsy kutoka nchini Tanzania ambaye ana mtoto wa miaka sita anayepata degedege zaidi ya mara 200 kwa siku.

Ameamua kuchukua hatua na kuanza kutokomeza dhana potofu juu ya ugonjwa huu kwa kutoa elimu kupitia mitandao ya kijamii ili kukuza uelewa katika jamii.

Video: @frankmavura