Tetesi za soka Ulaya: Man City inamtaka Florian Wirtz

t

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Florian Wirtz
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester City inamfukuzia kiungo Mjerumani wa Bayer Leverkusen Florian Wirtz, 21, huku kuna uswezekano mkubwa kiungo Muingereza James McAtee, 22, kuelekea upande wa pili (Mail).

Mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak anaweza kuruhusiwa kuondoka kama Newcastle haitafuzu klabu bingwa Ulaya msimu ujao, huku vilabu vya Liverpool na Arsenal vikimtaka nyota huyo mwenye miaka 25 (Mirror)

Mshambuliaji wa Ademola Lookman, 27, ataondoka Atalanta baada ya kuzozana na kocha Gian Piero Gasperini (Sky Sports Switzerland - in French).

Newcastle inafkiria kumsajili Lookman katika dirisha lijalo na inaweza kukutana na ushindani kutoka Manchester United, inayomtaka pia (Teamtalk).

Paul Pogba

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Paul Pogba

Kiungo wa Ufaransa Paul Pogba, 31, ambaye yuko huru baada ya kuondoka Juventus mwezi Novemba, anaweza kujiunga na Inter Miami wakati adhabu yake ya kutumia dawa za kusisimua misuli itakapomalizika mwezi ujao. Hiyo ni baada ya kukutana na mmiliki wa klabu hiyo David Beckham. (Manchester Evening News).

Kiungo Mbelgiji Kevin de Bruyne anasubiri kuona kama bado Manchester City itamuhitaji msimu ujao, huku mkongwe huyo akikubalia wazo la kucheza muda mchache kama atasaini mkataba mpya (Mirror), external.

Kiungo wa Croatia Luka Modric, 39, anaweza kusalia Real Madrid kwa muda mrefu atakavyotaka, hiyo ni kwa mujibu wa kocha Carlo Ancelotti. (Fabrizio Romano), external

Dijk

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Dijk

Real Madrid haiko kwenye mazungumzo na mlinzi Mholanzi Virgil van Dijk, 33, ambaye mkataba wake na Liverpool unamalizika msimu huu (Marca - in Spanish).

Manchester City ina matumaini ya kuibwaga Arsenal katika mbio za kumsajili kiungo kinda wa Norway, Sverre Nypan, 18, kutoka Rosenborg. (TBR Football)

Tottenham imeanza mazungumzo na kiungo wa Uruguay Rodrigo Bentancur kuhusu mkataba mpya, ambapo mkataba wake wa sasa unamalizka mwishoni mwa msimu ujao (Mail).

Kocha wa England Thomas Tuchel amefanya mazungumzo na beki wa kulia Arsenal Ben White kuhusu kurejea timu ya taifa ambapo mlinzi huyo kwa mara ya mwisho kuichezea england ilikuwa mwaka 2022 (Sun).