Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 18.07.2024
Aston Villa wanakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Amadou Onana kutoka Everton, kocha wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwa kocha wa England, Nani yuko tayari kumsubiri Pep Guardiola kuondoka Manchester City.
Kiungo wa Everton Mbelgiji Amadou Onana anatarajiwa kukamilisha uhamisho wa kwenda Aston Villa kufikia wikendi hii. (Sky Sports)
Shirikisho la soka la England liko tayari kumsubiri Pep Guardiola kuondoka Manchester City ili kumteua kama mrithi wa kudumu wa Gareth Southgate kama kocha wa England. (Independent)
Kocha wa zamani wa Liverpool Jurgen Klopp hana nia ya kugombea nafasi ya ukufunzi wa timu ya taifa ya England . (Sky Germany)
Kocha wa Tottenham Ange Postecoglou pia ni miongoni mwa makocha wanaowania kuziba pengo lililoachwa wazi na Southgate. (Telegraph - usajili unahitajika)
Al Nassr wamesitisha azma yao ya kumsajili mlinda mlango wa Juventus mwenye umri wa miaka 34 kutoka Poland Wojciech Szczesny. (Athletic - usajili unahitajika)
Paris St-Germain wameongeza juhudi za kumsaka mshambuliaji wa Napoli Victor Osimhen, 25, jambo ambalo linaweza kuathiri mpango wa Chelsea wa kumnunua mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Nigeria. (Talksport)
Liverpool wamejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kumnunua mlinzi wa Manchester United Leny Yoro, 18, kutoka Lille kwa sababu walihisi anavutiwa zaidi na klabu ya Real Madrid. (Mirror)
Birmingham City wanamnyatia mshambuliaji wa Aston Villa Mwingereza Louie Barry, 21. (Football Insider)
Villa bado wanadaiwa na Bayer Leverkusen zaidi ya nusu ya pesa walizomlipa winga wa Ufaransa Moussa Diaby, 25, ambaye anakaribia kujiunga na klabu ya Al Ittihad ya Saudia. (Football Insider)
West Ham wako kifua mbele katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Reiss Nelson, 24, huku The Gunners wakikadiria thamani ya mchezaji huyo kuwa pauni milioni 25. (Talksports)
Huddersfield Town wako kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Wolves Joe Hodge, 21, baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa timu ya Jamhuri ya Ireland ya chini ya miaka 21 kuchezea Queens Park Rangers kwa mkopo msimu uliopita. (Football Insider)
Barcelona wamewasilisha pendekezo lao kwa winga wa Athletic Bilbao Nico Williams, 22, katika juhudi ya kuafikiana na Mhispania huyo kabla ya klabu yoyote ya Ligi Kuu ya England kufanya hivyo. (Fabrizio Romano)
West Ham wamepiga hatua katika mazungumzo ya kumsajili Aaron Wan-Bissaka, 26, kutoka Manchester United. (Teamtalk)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi na kuhaririwa na Yusuf Jumah