Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 13.05.2024

Iliyochapishwa

Liverpool wanavutiwa na winga wa Newcastle mwenye umri wa miaka 23 Anthony Gordon, ambaye alianza kucheza soka katika klabu ya Everton. (Star)

Mkataba wowote kwa Gordon unaweza kukatiza matumaini ya Arsenal ya kumsajili mshambuliaji wa Newcastle mwenye umri wa miaka 24 raia wa Uswidi Alexander Isak msimu huu wa joto. (Express)

Mshambuliaji wa Colombia Luis Diaz, 27, amepuuza tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa kwenda Paris St-Germain, akisema "mambo mazuri yanakuja" Liverpool. (Mirror)

Sheffield United iko tayari kutoa ofa ya pauni milioni nane kwa mlinda mlango wa Sunderland Muingereza Anthony Patterson, 23. (Sun)

Manchester City wanavutiwa na mlinda mlango wa chuo cha mafunzo ya soka ya Everton mwenye umri wa miaka 16 Douglas Lukjanciks na wanaweza kulipa hadi pauni milioni 10 kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza wa chini ya miaka -17. (Sun)

Newcastle wanapigiwa upatu kumsajili mlinzi Tosin Adarabioyo mwenye umri wa miaka 26 kwa uhamisho wa bure mkataba wake wa Fulham utakapokamilika msimu huu wa joto. (Mail)

Crystal Palace haitamruhusu meneja wa Austria Oliver Glasner, 49, kuondoka msimu wa joto, licha ya tetesi zinazomhusisha na nafasi ya ukocha mkuu katika klabu ya Bayern Munich. (Fabrizio Romano)

Mustakabali wa Luka Modric utawekwa wazi "wiki ijayo", asema wakala wake, huku kandarasi ya kiungo huyo wa kati wa Croatia mwenye umri wa miaka 38 katika klabu ya Real Madrid ikikamilika msimu huu wa joto. (Goal)

Eintracht Frankfurt haitaanzisha mchakato wa pauni milioni 13 wa kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Uholanzi aliyeko kwa mkopo Donny van de Beek, 27. (Fabrizio Romano)

Everton, Brighton, Inter Milan na Wolfsburg wanapania kumnunua beki wa wa AZ Alkmaar wa Japan Yukinari Sugawara, 23. (Florian Plettenberg)

Mkufunzi wa Everton Sean Dyche ana matumaini ya kuchunguza mpango wa kubadilisha mkopo wa winga wa Uingereza Jack Harrison kutoka Leeds kuwa uhamisho wa kudumu (Liverpool Echo)

West Ham wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Sevilla raia wa Morocco, 26, Youssef En-Nesyri msimu wa joto. (Football Insider)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi