Tetesi za soka Ulaya Jumapili 05.05.2024

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Meneja wa Man United Eric ten Hag
Iliyochapishwa

Meneja wa Manchester United Erik ten Hag ndiye anayetarajiwa kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel anayeondoka Bayern Munich. (Falk Christian)

Mshambuliaji wa Liverpool na Uruguay Darwin Nunez, 24, analengwa na Barcelona msimu huu kama mbadala wa mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 35. (Sun).

Man United wanasubiri ofa kwa winga wa Brazil Antony, 24, huku wakitafuta nafasi katika kikosi chao kumnunua kiungo wa kati wa kimataifa wa Ufaransa na Crystal Palace aliyezaliwa Uingereza Michael Olise, 22. (Rudy Galetti).

Arsenal wana makubaliano ya mazungumzo na Brentford kukamilisha usajili wa kudumu wa mlinda lango wa Uhispania David Raya, 28, msimu huu kwa pauni milioni 27. (Fabrizio Romano)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Harry Maguire

Liverpool wana matumaini kuwa meneja msaidizi Pep Lijnders, ambaye anatazamiwa kuondoka msimu huu pamoja na meneja Jurgen Klopp, watarejea Anfield siku zijazo. (Mirror)

Manchester United inanuia kumtumia mlinzi wa Uingereza Harry Maguire, 31, kama chambo cha kuwashawishi Everton kumuuza mlinzi wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 21, msimu huu. (Star)

Mkufunzi wa Palmeiras Abel Ferreira anataka rais wa klabu Leila Pereira kuzuia kuuzwa kwa winga wa Brazil Estevao Willian mwenye umri wa miaka 17 kwa Chelsea, ambao wameweka mezani ofa ya euro 55m (£47m). (Goal)

Kocha wa zamani wa Chelsea Graham Potter yuko katika kinyang'anyiro cha kuwa meneja wa Ajax baada ya mabingwa hao mara nne wa Uropa kukata tamaa ya kurejea tena kwa Ten Hag wa Manchester United. (De Telegraaf)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Graham Potter

Getafe wameanza mazungumzo na Manchester United kuhusu uwezekano wa kusaini mkataba mwingine wa mkopo kwa mshambuliaji wa Uingereza Mason Greenwood, 22. (Subscription Required)

Mshambulizi wa Juventus na Serbia Dusan Vlahovic, 24, anavutiwa na Arsenal huku Mikel Arteta akijaribu kuimarisha safu yake ya ushambuliaji. (Tuttosport – In Itali)

Beki wa Uingereza Jarell Quansah, 21, yuko mbioni kupata kandarasi mpya ya muda mrefu baada ya kuonyesha kiwango kizuri msimu wake akiwa Liverpool. (Mirror)

Inter Milan wako tayari kumenyana na Manchester United na Arsenal katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Bologna Mholanzi Joshua Zirkzee, 22. ( 90 min)