Kombe la Dunia 2022: Kile ambacho takwimu zinasema kinaweza kutokea Qatar mnamo Novemba na Desemba

Iliyochapishwa

Je, Kombe la Dunia lililopita linaweza kutuambia nini kuhusu nini cha kutarajia nchini Qatar?

 

Je, Kombe la Dunia la mwaka huu ni kali zaidi? Je, timu zilizofuzu kupitia mchujo ziondolewe sasa? Je, kucheza barani Asia kunafaidisha nchi fulani?

 

Tunaangazia mambo haya - pamoja na mengine mengi - ili kuona ni timu gani zinaweza kuwa katika nafasi nzuri katika Kombe la Dunia lenye mafanikio.

 

Kumekuwa na mashindano sita ya hapo awali yakiwa na muundo sawa wa timu 32 zilizopangwa katika vikundi nane vya timu nne kila mojawapo na ni mashindano haya sita ambayo yametoa mechi 384 kutazama na kuona ikiwa mifumo yoyote itaibuka.

 

Katika uchanganuzi ulio hapa chini tutaangazia mashindano haya sita - kutoka 1998-2018

Je, eneo lina athari kiasi gani kwenye utendakazi wa timu zinazosafiri?

Katika michuano mitatu iliyopita iliyochezwa Ulaya, kulikuwa na mataifa ya Ulaya yaliojaza nafasi 10 kati ya 16 za mtoano. Wakati fainali zimefanyika nje ya Ulaya takwimu hii inashuka hadi wastani wa saba.

Timu za Amerika Kusini zinanufaika zaidi kutokana na kushuka huku, huku mara mbili ya timu za Asia zikifika hatua ya mtoano wakati fainali hazipo Ulaya.

Je, kuna uhusiano kati ya kufuzu na jinsi timu zinavyosonga mbele katika fainali?

Washindi watano kati ya sita katika  Kombe la Dunia walitoka Ulaya - na isipokuwa mabingwa wa 1998 Ufaransa, ambao walishiriki michuano hiyo moja kwa moja kama wenyeji, wote walikuwa na kampeni nzuri za kufuzu.

 

Mabingwa wengine wnne  - Italia mnamo 2006, Uhispania 2010, Ujerumani mnamo 2014 na Ufaransa mnamo 2018 - aidha walicheza bila ushindwa au walipoteza mara moja tu katika mechi 10 za kufuzu. Asilimia hizi za ushindi (huku sare zikihesabiwa kuwa nusu ushindi) zilikuwa 80% na zaidi.

 

Ili kufuzu kwa hafla ya mwaka huu, mataifa mengi ya Ulaya yamefikia kiwango cha 80%: Denmark (95%), Uingereza na Ujerumani (90%), Serbia na Ubelgiji (87.5%), Uhispania, Uswizi na Ufaransa (zote 81.3). %) na Croatia na Uholanzi (zote 80%).

Je, orodha ya mwaka huu ni 'imara' kiasi gani kulingana na viwango vya dunia ikilinganishwa na mashindano ya awali?

Kwa kutumia viwango vya kimataifa vya Fifa vya timu mwanzoni mwa mashindano, tunaweza kuhisi jinsi mashindano yanavyoweza kuwa na ushindani.

Kwa sababu ya sheria za Fifa kuelekeza idadi ya timu kutoka kila bara, kuna timu ambazo hazipo kwenye fainali ambazo ziko juu kuliko zingine.

 

Timu ambayo haitashiriki katika kombe hili ni Italia – ikiwa katika nafasi ya  sita duniani - lakini Colombia (17), Peru (23), Sweden (25), Ukraine (27), Chile (29) na Nigeria (32) zote zingehusika ikiwa orodha ya duniani ingetumika katika kufuzu katika fainali bila kujali eneo.

 

Ingawa timu saba za daraja la chini zinazoshiriki wakati huu zinaweza kuonekana kama sehemu kubwa, kwa hakika ndiyo idadi ya chini zaidi wakati wa enzi ya timu 32. Baadhi ya fainali zimekuwa na timu 11 kutoka nje ya 32 bora.

 

Kwa hivyo wakati huu kutakuwa na mchuano mgumu zaidi.

 

Na viwango vilivyojumuishwa vinaonesha kwamba  England na Wales ziko kwenye kundi gumu zaidi nchini Qatar - ni kundi pekee ambapo kila timu iko kwenye 20 bora duniani kufikia 30 Oktoba.

Makundi ya Kombe la Dunia la 2022 na orodha za dunia (kufikia 30 Oktoba)

A - Netherlands (8), Senegal (18), Ecuador (44), Qatar (50)

B - England (5), USA (16), Wales (19), Iran (20)

C - Argentina (3), Mexico (13), Poland (26), Saudi Arabia (51)

D - France (4), Denmark (10), Tunisia (30), Australia (38)

E - Spain (7), Germany (11), Japan (24), Costa Rica (31)

F - Belgium (2), Croatia (12), Morocco (22), Canada (41)

G - Brazil (1), Switzerland (15), Serbia (21), Cameroon (43)

H - Portugal (9), Uruguay (14), South Korea (28), Ghana (61)

Je, washindi wa mchujo huwa na matokeo mazuri kiasi gani?

Wales, katika mchuano wao wa kwanza kwa miaka 64, ilifuzu kupitia mchujo wa Ulaya pamoja na Poland na Ureno.

 

Kwa mtazamo wa kwanza inaweza kuonekana kama njia ya mlango wa nyuma - lakini historia ya hivi majuzi inaonyesha timu zinazofuzu kwa njia hiyo zinaweza kuleta athari kubwa.

 

Ukilinganisha timu za Ulaya, asilimia 67 ya waliofuzu katika hatua ya mtoano hufika hatua ya mtoano, ikilinganishwa na asilimia 57 pekee ya timu zinazofuzu moja kwa moja.

 

Fainali mbili kati ya sita zilizopita za Kombe la Dunia zimeshirikisha timu za Ulaya ambazo ziliingia kwa njia ya mchujo -Ujerumani mwaka 2002 na Croatia mwaka 2018. Aidha, Croatia (1998) na Uturuki (2002) walitinga fainali na tatu zaidi katika upande wa  timu za mchujo zilifika robo fainali.

Kwa nini mabingwa watetezi uhangaika?

Tangu miaka ya 1990, washindi wa Kombe la Dunia wameshinda jumla ya mechi moja ya mtoano katika michuano mitano, Brazil ilipoifunga Ghana mwaka wa 2006. Kwa hakika kombe hilo halijatetewa tangu 1962 na katika michuano 14 tangu hapo, ni washindi wawili pekee ambao wamepita raundi ya robo fainali.

 

Shida za washindi mara nyingi huanza na mechi ya kwanza. Katika michuano 12 ambayo Uingereza ilishinda mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Romania mwaka 1970, ni mabingwa watatu tu watetezi ambao walifungua kwa ushindi. Na mabingwa wanne kati ya watano waliopita hata hawajatoka kwenye makundi yao.

 

Kwa nini? Naam, miaka minne ni muda mrefu katika soka. Kwa wastani, ni asilimia 50 pekee ya wachezaji wanaoanza fainali wataanza mchezo wa kwanza wa kundi la mashindano yanayofuata.

 

Italia ilichezesha wachezaji watatu pekee katika kikosi chao cha kwanza kutoka fainali ya 2006 walipoanza mechi  yao ya utetezi kwa sare dhidi ya Paraguay mwaka 2010.

Je, ni mara ngapi timu ya daraja la chini hushangaza?

Ikiwa unatarajia timu mbili zinazoorosheshwa juu kuibuka mshindi kila mara kutoka kwa kila kundi, utashangaa.

Ni kawaida kwa nafasi sita kati ya 16 za mtoano kuchukuliwa na timu zilizoshika nafasi ya tatu na nne katika makundi yao. Hiyo ni kiwango cha kushangaza cha 32%. Katika mashindano haya sita, michezo ya mtoano imeshindwa kwa 34% na timu za daraja la chini.

Matokeo ya kushangaza zaidi katika mechi za mtoano za Kombe la Dunia - kulingana na viwango vya Fifa

Year  Winner (rank)     Loser (rank)         Difference

2002 South Korea (40)         Italy (6)      34 places

2002 Senegal (42)        Sweden (19)       23 places

2002 South Korea (40)         Spain (8)    32 places

2018 Russia (70) Spain (10)  60 places

Matokeo matatu ya kushangaza kati ya manne makubwa yamesababishwa na wenyeji - mara mbili kupitia penalti na mara moja kwa bao la dhahabu.

Chochote kitakachotokea katika wiki tano zijazo, kuna uwezekano wa kuwa na mishtuko mingi zaidi, drama na mabishano mbeleni.