Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Rashford huenda asicheze tena Man Utd

Chanzo cha picha, Getty Images
Marcus Rashford huenda asicheze tena Manchester United, Newcastle United inaweza kumsajili Justin Kluivert, na Nico Williams anawaniwa na Arsenal.
Mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, ambaye amejiunga na klabu ya Aston Villa kwa mkopo, huenda asicheze tena Man United kwa vile uhusiano kati ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 na timu hiyo ya Old Trafford umesambaratika. (Guardian)
Newcastle United inajiandaa kumsajili msahambuliaji wa Bournemouth na Uholanzi Justin Kluivert, 25, ikimkosa mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, msimu wa joto. (Sun)
Newcastle na Tottenham huenda zikafufua nia ya kumsajili mlinzi wa Crystal Palace Marc Guehi, 24, msimu wa joto atakapoingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake, baada ya Spurs kukataliwa ofa mwishoni mwa dirisha la Januari. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kocha wa Napoli Antonio Conte amesikitishwa na hatua ya klabu hiyo kutomsajili winga wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho, 20, au mshambuliaji wa Ujerumani Karim Adeyemi, 23, kutoka Borussia Dortmund mwezi Januari baada ya kumuuza winga wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 23, kwa Paris St-Germain. (Sky Sports Italia, kupitia Football Italia)
Klabu za Manchester United na Bayern Munich wote zilimtaka mshambuliaji wa Ufaransa Christopher Nkunku mwezi Januari lakini zilisitisha mpango huo kwa sababu Chelsea ilimthamini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Mail)
Arsenal hawakumsajili mchezaji yeyote katika uhamisho wa Januari, lakini mikataba ya mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 21, na kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi, 26, huenda ikaongezwa. (Football.London)
Winga wa Athletic Bilbao wa Uhispania Nico Williams, 22, ni kipaumbele wa cha usajili wa mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta. (Football transfer)
Kiungo wa Arsenal na timu ya taifa ya Italia Jorginho, 33, ametia saini makubaliano ya awali ya mkataba wa kujiunga na Flamengo ya Brazil msimu ujao wakati mkataba wake na The Gunners utakapokamilika. (Mirror)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












