Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumapili: Napoli tayari kumnunua Rashford
Napoli wako tayari kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, PSG wanakaribia kumnunua winga wa Napoli Khvicha Kvaratskhelia na Barcelona wanamtaka mshambuliaji wa Newcastle United Alexander Isak.
Napoli wanatarajiwa kuwasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Muingereza Marcus Rashford, 27, huku winga wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia akitarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Italia. (Mirror)
Paris St-Germain wanakaribia kumsajili Kvaratskhelia kutoka Napoli, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 tayari ameshakubali mkataba na timu hiyo ya Ufaransa. (Foot Mercato - kwa Kifaransa)
PSG wanaamini kuwa wanaweza kuwashawishi Aston Villa kuwauzia mshambuliaji wa Colombia Jhon Duran, 21, na klabu hiyo ya Ligue 1 ina nia ya kumjumuisha mshambuliaji wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 26, katika mazungumzo yoyote. (Mail)
Kiungo mshambulizi wa Uhispania Marco Asensio, 28, anatarajiwa kuhama PSG, huku Aston Villa, Juventus na Real Sociedad wakitarajiwa kuwa mojawapo wa klabu anazoweza kujiunga nazo. (Foot Mercato - kwa Kifaransa)
Barcelona wanamtaka mshambuliaji wa Newcastle United Alexander Isak na wanaweza kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 mwezi Januari au msimu wa joto, kulingana na hali yao ya kifedha. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
AC Milan wana nia ya kumsajili beki wa Uingereza Kyle Walker, huku meneja wa Manchester City Pep Guardiola akisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 aliomba kuondoka katika klabu hiyo ya Uingereza. (Guardian)
Matumaini ya Chelsea ya kumsajili mlinzi wa Uingereza Marc Guehi, 24, kutoka Crystal Palace huenda yakatibuka kwa sababu ya mfumo mkali wa mshahara wa klabu hiyo ya Stamford Bridge. (Mirror)
Mkurugenzi wa michezo wa Eintracht Frankfurt Markus Krosche amethibitisha kuwa kuna klabu ambayo imewasiliana nao kuhusu usajili mshambuliaji wa Misri Omar Marmoush. Manchester City walikuwa wamefikia mkataba na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Sky Sports Germany)
Barcelona wamekataa ombi la Juventus la kumnunua beki wa Uruguay Ronald Araujo na wanataka kusalia na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Uhispania unamalizika 2026. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
Borussia Dortmund wanafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Carney Chukwuemeka, 21, kwa mkopo kutoka Chelsea. (Sky Sports Ujerumani)
Chukwuemeka pia yuko kwenye rada za Lazio ya Italia huku wakipania kuimarisha kikosi chao. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi