Zifahamu faida za maziwa ya ngamia zisizojulikana
Na Mohamed-Rashid Dirie

Chanzo cha picha, Getty Images
Wasomali na ngamia na huwezi kuwatenganisha au kutenganishwa kwa njia yoyote, kuanzia watoto mpaka wazazi wao.
Katika fasihi yake, Somalia inawataja ngamia na kuwahesabu kwa mashairi au nyimbo za kuwasifu. Pia, huwapa majina mazuri sana yanayotafsiriwa katika uhusiano kati ya ngamia na mmiliki ama msimamizi.
Dunia ya kisasa sasa inaboreshwa kwa faida ya ngamia, maziwa yake na bidhaa nyingine zinazotengenezwa kutokana na maziwa ya ngamia.
Wakati wa kutafiti maziwa ya ngamia na faida zake niligundua kuwa kuna baadhi ya maeneo nchini Ethiopia ambako maziwa ya ngamia yanaaminika kuwa na manufaa maalum kwa wanaume na wanawake walio katika ndoa. Nitafafanua hoja hii katika sehemu zifuatazo.
Je, zipi ni faida za maziwa ya ngamia?
Nilimuuliza Khadar Abdullah, daktari mkuu wa magonjwa na mchambuzi wa binadamu, anayefanya kazi huko Hargeisa kuhusu faida za maziwa ya ngamia. Nilimuuliza kuhusu faida halisi za maziwa ya ngamia, akasema. ''Maziwa ya ngamia mara nyingi yana virutubisho ambavyo ni bora kwa ukuaji wa mwili, ikiwepo 'calcium, thiamine na pottasium ambazo zote ni nzuri na muhimu kwa ukuaji wa mwili.
Pia niliuliza kuhusu faida za maziwa ya ngamia, Diktor Usman ambaye anafanya kazi Mogadishu. Naye alisema ''Maziwa ya ngamia yanapokuwa mapya yana vitamini muhimu kwa mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na calcium ambayo ni nzuri kwa mifupa na vimeng'enya muhimu vinavyoimarisha mfumo wa kinga''.
''Maziwa ya ngamia hudhibiti utamu wa mwili, pia ni tiba ya mzio mbalimbali wa magonjwa kama vile pumu, nimonia, mzio wa chakula na kadhalika.'' Haya yameandikwa na Abdullahi Mahdi anayeendesha shughuli zake katika hospitali ya Eastend mjini Nairobi, Kenya na pia ni mwandishi anayechapisha taarifa za matibabu kwenye SomaliDoc.
Mambo ya kushangaza yaliyomo kwenye maziwa ya ngamia

Chanzo cha picha, Getty Images
Sisay na Awoke, ambao ni walimu wa Chuo Kikuu cha Jijiga nchini Ethiopia, walichapisha makala katika Jarida la Uvuvi na Uzalishaji wa Mifugo (Journal of Fisheries & Livestock Production) na kueleza masuala yanayohusiana na maziwa ya ngamia na ukitafakari zaidi itakuvutia kutokana uwezo wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu.
Maaajabu ya maziwa ya ngamia
- Ni kwamba ngamia hutoa maziwa zaidi wakati wa ukame, na hilo ni tofauti na wanyama wengine kama vile ng'ombe.
- Maziwa anayotoa wakati wa ukame wakati hakuna maji ya kunywa, maziwa yake yana maji mengi, na wakati wa msimu wa kawaida usio wa ukame maziwa yanayotolewa ni kidogo akiwa na maji kiduchu.
Hekima hii ya Mungu ni kwamba wakati wa ukame, wakati kuna maji kidogo, maziwa ya ngamia huhifadhi ili watoto wa binadamu na watoto wake wayatumia. Faida za maziwa ya ngamia ni zaidi ya maziwa, kuna mpaka bidhaa zinazoengenezwa kutokana na maziwa ya ngamia.
Mfano wa bidhaa hizi ni sabuni, mafuta ya krimu kwa ajili ya kulinda ngozi, dawa za binadamu, chokoleti, Ice cream na pia siagi iliyotengenezwa kwa maziwa ya ngamia ni moja ya bidhaa maarufu zaidi.
Fursa ya kibiashara

Chanzo cha picha, Getty Images
Somalia inakadiriwa kuwa na ngamia zaidi ya milioni 6, ingawa hakuna takwimu rasmi, na inasemekana kuwa ndiyo nchi yenye ngamia wengi zaidi duniani.
Kwa hiyo, kama Somalia ina ngamia wa aina hiyo, ni lazima pia imiliki au iongoze kila kitu kuhusu ngamia. Iwe ni sayansi ya ngamia, uchumi na biashara ya ngamia, maziwa ya ngamia na kila chenye chembe ya ngamia kinapaswa kuwa cha juu zaidi nchini Somalia.
Nilipokuwa nikichunguza maziwa ya ngamia na faida zake, siku zote ilikuwa ikija kichwani mwangu kuhusu nafasi za kazi ambazo zingeweza kutengenezwa na ni vijana wangapi wangeweza kufaidika na kazi ambazo zingeweza kuzalishwa kutokana na ngamia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ni nini kinachoweza kutuzuia kutengeneza, kufanyia kazi hili, ili kufanikiwa kupiti maziwa ya ngamia na kuyatumia kwa njia tofauti.
Ukosefu mkubwa wa ajira nchini unatokana na ukosefu wa fursa za ajira kwa kuzingatia ukosefu wa tija nchini. Iwapo viwanda vidogo vinavyotengeneza bidhaa tajwa hapo juu vitaanzishwa, itapelekea tija ya nchi kuanza taratibu, kuzalisha ajira, na kuinua uchumi wa wananchi na nchi kwa ujumla.
Kila nchi inayofanya maendeleo huanza kwa maafikiano, na kuuza nje zaidi kuliko nchi nyingine duniani. Ili Somalia iingie kwenye njia hii, ni lazima ianze kuzalisha ndani ya nchi, na pia itakuwa kazi ya ubunifu ambayo itawawezesha vijana wa Somalia kubadili mawazo yao kuhusu nchi yao.
Inasemekana kwamba tuna ngamia wengi zaidi, ni rahisi kwetu kupata maziwa mengi zaidi ya ngamia duniani, tunaweza kupata ujuzi na misuli ya kufanya kazi yoyote. Mara tu tunaweza kupata hii pamoja, swali ambalo linastahili kuulizwa ni jinsi gani tunaweza kuongoza katika kila kitu kuhusu ngamia?
Mohamed-Rashid Dirie ni mwandishi na mtafiti anayejitegemea. Maoni yake hayatafsiri kuwa maoni ya BBC.














