Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 01.03.2024

Luis Diaz

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Colombia Luis Diaz
Iliyochapishwa

Liverpool watakuwa tayari kupokea ofa ya kumuuza mshambuliaji wa Colombia Luis Diaz, 27, msimu wa joto - ikiwa mashambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 31, atakubali mkataba mpya. (Sun)

Liverpool wangedai ada ya zaidi ya pauni milioni 100 ili kumuuza Salah kwa Ligi Kuu ya Saudi msimu huu kwa hivyo wanaamini watakuwa na pesa zinazohitajika za kujaza nafasi yake. (Football Insider)

Tottenham Hotspur wanaendelea kufuatilia hali ya kiungo wa Uingereza Conor Gallagher huko Chelsea na wako tayari kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 msimu wa joto. (Daily Mail)

Arsenal wanajiandaa kuanza mazungumzo na kiungo wa kati wa Italia Jorginho, 32, kuhusu kandarasi mpya. (Evening Standard)

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Kocha wa Brighton Roberto de Zerbi ni mshindani mkubwa katika mbio za kuwania nafasi ya mkukufunzi wa ajaye wa Manchester United. (Football Insider)

Getafe wako tayari kuanzisha mazungumzo na Manchester United kuhusu kuongeza muda wa kusalia kwa Mason Greenwood katika klabu hiyo, kwa kuafikiana mkataba mwingine wa mkopo na mshambuliaji huyo Mwingereza mwenye umri wa miaka 22 au uhamisho wa kudumu. (Times- usajili unahitajika)

Barcelona wanataka kuwabakisha wachezaji wa Ureno waliocheza kwa mkopo Joao Cancelo na Joao Felix msimu ujao, na wako tayari kulipa Manchester City kati ya euro milioni 15 na 20 (£13-£17m) kumpata Cancelo, 29, na kumchukua mshambuliaji Felix, 24, kwa mkataba mwingine wa mkopo kutoka Atletico Madrid. (Sport - kwa Kihispania)

Joao Cancelo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mchezaji wa Manchester City Joao Cancelo

Chelsea wanaweza kumnunua mlinda mlango wa Arsenal Muingereza Aaron Ramsdale, 25, wakati wa usajili wa majira ya kiangazi. (Football Insider)

Beki wa Uingereza Trevoh Chalobah, 24, anataka kusalia Chelsea na amesikitishwa na klabu hiyo kufikiria kumuuza msimu huu wa joto. (Teamtalk)

Beki wa Uingereza Eric Dier, 30, ametimiza masharti ya kimkataba yanayohitajika kubadilisha uhamisho wake wa mkopo wa Bayern Munich kutoka Tottenham kuwa uhamisho wa kudumu mwishoni mwa msimu. (Athletic)

Manchester United na Aston Villa wametuma maskauti kumfuatilia beki wa Torino Mtaliano Raoul Bellanova, 23, msimu huu. (Tuttosport - kwa Kiitaliano)

Aaron Ramsdale

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Chelsea wanaweza kumnunua mlinda mlango wa Arsenal Muingereza Aaron Ramsdale

Roma wana nia ya kumteua Richard Hughes, mkurugenzi wa ufundi wa Bournemouth, kuhudumu katika klabu hiyo ya Serie A msimu ujao. (Telegraph - usajili unahitajika)

Bayern Munich wako tayari kulipa hadi euro 100m (£85.6m) kumsajili beki wa kati wa Ureno Antonio Silva, 20, kutoka Benfica. (Sport - kwa Kihispania)

AC Milan na Juventus wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Morocco Youssef En-Nesyri, 26, wakati mchezaji anayelengwa na West Ham anaingia mwaka wa mwisho wa kandarasi yake na Sevilla msimu huu wa joto. (Il Corriere dello Sport, via Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi