Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 29.02.2024

tt

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Winga wa Wolves wa Ureno Pedro Neto
Iliyochapishwa

Tottenham wanamsaka kiungo mshambuliaji wao mkuu katika usajili wa majira ya kiangazi, huku winga wa Wolves wa Ureno Pedro Neto, 23, na winga wa Crystal Palace wa Uingereza Eberechi Eze, 25, wakiangaziwa kwa sasa. (Independent)

Liverpool wamewasilisha ombi la awali la kuzungumza na mkufunzi wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso wakitafuta mbadala wa Jurgen Klopp anayeondoka. (Bild - kwa Kijerumani)

Manchester United itafanya uamuzi kuhusu mustakabali wa mshambuliaji wa Uingereza Mason Greenwood, 22, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Getafe, ifikapo mwisho wa Mei. (Sun)

Arsenal, Manchester United na Chelsea wana nia ya kumsajili kipa wa Ujerumani Diant Ramaj, 22, wa Ajax. (Bild)

Mshambulizi wa Manchester United Mason Greenwood

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Manchester United kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wa mshambuliaji wa Uingereza Mason Greenwood

Maisha ya Dele Alli Everton yanaweza kuwa mazuri baadaye mwaka huu kwa vile The Toffees wako tayari kumpa kiungo huyo wa zamani wa England, 27, mkataba mpya. (Express, via Athletic)

Mshambulizi wa Korea Kusini Son Heung-min, 31, anameridhika Tottenham na mazungumzo rasmi kuhusu kandarasi mpya ambayo yamepangwa kuanza. (Football Insider)

Mshambulizi wa Ureno Rafael Leao, 24, amekuwa akihusishwa na Barcelona lakini anasema "hawezi kuondoka" AC Milan. (Sport - kwa Kihispania)

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Everton wako tayari kumpa Dele Alli mkataba mpya

Kiungo wa kati wa Italia Jorginho, 32, anaweza kurejea Serie A mkataba wake Arsenal utakapokamilika msimu huu wa joto. (Goal)

Klabu za Ligi kuu ya Saudi Pro zinawanyatia nyota kadhaa wa Ligi ya Premia katika usajili wa majira ya kiangazi, wakiwemo wachezaji wachanga kama vile mshambuliaji wa Argentina Matias Soule, 20, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Frosinone kutoka Juventus. (ESPN)

Timu ya daraja la pili ya Saudia Al Qadsiah ilitoa ofa nono kwa kiungo wa zamani wa Uhispania Sergi Roberto lakini nahodha huyo wa Barcelona, ​​32, angependelea kuhamia MLS. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jorginho, anaweza kurejea Serie A mkataba wake Arsenal utakapokamilika.

Brighton atapokea kitita kikubwa kwa ajili ya kinda wa miaka 14 baada ya mahakama kuamua kwamba Chelsea lazima walipe hadi pauni milioni 4.25 kumnunua mshambuliaji wa England wa chini ya miaka -17 Shumaira Mheuka, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 16 lakini alisajiliwa 2022. (Football Insider)

Michael Edwards angetaka udhibiti kamili kabla ya kurejea kama mkurugenzi wa michezo wa Liverpool, hatua ambayo huenda ikachangia uhamisho wa mkurugenzi wa kiufundi wa Bournemouth Richard Hughes. (Mirror)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi