Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 29.06.2024

Iliyochapishwa

Bayern Munich wamewasilisha ofa ya mwisho ya kati ya pauni milioni 38-39 kwa ajili ya kiungo wa kati wa Fulham na Ureno Joao Palhinha, 28, ambaye tayari amefikia makubaliano ya kibinafsi na klabu hiyo ya Ujerumani. (Sky Sports Ujerumani)

West Ham wako tayari kulipa pauni milioni 35 kumnunua mlinzi wa Wolves Muingereza Max Kilman lakini wako tayari kutafuta mabeki wengine, huku klabu hiyo ya Midlands ikikataa kubadilisha dau lao la pauni milioni 45 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Guardian)

Fulham wanajiandaa kufanyia kazi mikataba ya kuwabakisha mshambuliaji wa Brazil Willian, 35, na winga wa Jamaica Bobby De Cordova-Reid, 31, hata baada ya kandarasi zao na klabu hiyo kuisha Jumatatu. (Standard)

Mazungumzo kati ya klabu ya Manchester United na mkufunzi Erik ten Hag kuhusu mkataba mpya yamekuwa mazuri na yamepiga hatua wiki hii. (Sky Sports)

Chelsea wanataka pauni milioni 37 kwa ajili ya mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, lakini AC Milan na Napoli wanatumai kwamba bei ya mchezaji huyo wa miaka 31 itashuka msimu wa joto. (Gianluca di Marzio)

Barcelona na Paris St-Germain wanatumai kumshawishi mashambuliaji wa Argentina Julian Alvarez, 24, kuondoka Manchester City msimu huu. (Caught Offside)

AC Milan pia wanavutiwa na mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham, 26, ambaye ana mkataba hadi 2026 na Roma. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Juventus wanamnyatia mshambuliaji wa Atalanta Ademola Lookman, huku Bayern Munich wakimfanya mchezaji huyo kimataifa wa Nigeria mwenye umri wa miaka 26 kuwaniwa na klabu kadhaa za Ligi Kuu ya England. (Mail)

Bayern Munich wako kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa Ujerumani Jonathan Tah kutoka Bayer Leverkusen na klabu hizo mbili zinakaribia kufikia makubaliano ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake. (Sky Sports Ujerumani)

Newcastle United wana imani kwamba mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 24, atasaini mkataba mpya msimu huu wa joto, huku Chelsea wakionyesha nia ya kutaka kumsajili. (Givemesport)

Barcelona huenda wasimnunue beki wa Bayern Munich Mjerumani Joshua Kimmich, huku mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji na Everton Amadou Onana, 22, na mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Mikel Merino, 28, anayechezea Real Sociedad, wakionekana kuwa chaguo bora zaidi katika safu yao ya kati.(Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Tottenham wanamwinda Archie Gray, 18, wa Leeds, huku kiungo huyo wa kati wa Uingereza akiwa kwenye rada za vilabu vya Uhispania na Ujerumani. (Talksport)

Everton ndio klabu ya hivi punde zaidi kutangaza nia ya kumnunua winga wa Hull Muingereza Jaden Philogene mwenye umri wa miaka 22. (Echo)

Southampton wanajadiliana na kocha Russell Martin kuhusu kurefusha kandarasi yake baada ya kuwaongoza kurejea tena katika Ligi ya Premia. (Usajili unahitajika)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi