'Ninahisi uchungu sana ninapoona wanyama wakubwa hivi wakianguka'

Iliyochapishwa

Vifo vya ndovu katika hifadhi ya kitaifa ya wanyamapori ya Amboseli Kusini mwa Kenya,

Vimeipa wasi wasi watu wa jamii ya Wamaasai ambao wanachukulia vifo hivyo kama tahadhari ya hali mbaya kwa mifugo wao.

Athari za kiangazi ni wazi huku wanyama wakipata tabu kupata lishe- ardhi ni kavu  na jua halina huruma katika eneo hili.

Wanahabari wa BBC Ann Ngugi na Judith Wambare walitembelea mbuga hiyo na kupata

mizoga ya wanyamapori waliokufa kwa  ajili ya hali ngumu iliyosababishwa na kiangazi hiki.