Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Treni ya kustaajabisha ya safari ya kilomita 80 Zimbabwe
Katika njia yake kati ya Dete na Ngamo, "Tembo Express" huwapa wageni uzoefu wa kipekee kabisa wakati wa safari.
Tulitoka nje ya Kituo cha Dete kuelekea mpaka wa kaskazini-mashariki wa Mbuga ya Kitaifa ya Hwange ya Zimbabwe, wakiwa na shauku kweli - watalii tisa, wahandisi wawili na mwongoza safari mmoja - tukiwa njiani kutoka Maporomoko ya Maji ya Victoria hadi eneo tambarare wla Ngamo, eneo lililosheheni nyasi penye tembo ambapo misitu ya michongoma inayotoweka hukutana na eneo kame la mchanga wa Kalahari.
Nilitazama jua la adhuhuri na kupata kinywaji kidogo, nikijitahidi kusimama kwa mguu mmoja na kuegemea upande wa gari letu la kibinafsi, lililojengwa kwa kusudi la kuona vizuri ndege mchangamfu aliyesimama juu ya waya.
Abiria mwenzao kamera yake ilikuwa inatimika kutazama na kupiga icha kila upande.
Tuliona kidogo rangi ya buluu ya umeme, mdomo mrefu, kichwa kikubwa, lakini mwanga ulifanya utambuzi fulani kuwa mgumu.
Treni ilipozidi kushika kasi, tukiacha shabaha yetu nyuma, tuliendelea na mjadala.
Je, alikuwa mdiria? Aina fulani ya kigogota?
Aliposikia tukizungumza, mmoja wa wahandisi wa reli alimtambua ndege huyo kuwa ‘lilac-breasted roller’ yaani Kambu kifua-buluu-nyekundu-nyeupe.
Nikiwa nimefarijika kupata jibu, niliongeza ndege huyo kwenye orodha yangu na kutulia kwenye kiti changu.
Treni yenye behewa moja ambayo huchukua hadi watu 22, Elephant Express inaonekana kuwa gari la kipekee la safari, lakini inatoa uzoefu wa kipekee kabisa wa safari.
Badala ya kutafuta wanyama wakubwa katika gari ya 4x4 au kwa miguu, abiria huwatokea kutoka kila upande, na kuongeza hisia ya utulivu kwa ajabu.
Hilo lilifanya maofisa wa kikoloni wa Uingereza na wataalamu wa wanyamapori watilie shaka hekima ya kujenga eneo la hifadhi kwa ajili ya wanyama ambalo lingezungukwa na treni iliyokuwa ikifanya kazi. Hatukuwa mbali na Kituo cha Dete wakati wahandisi walipunguza kasi na kuelekeza upande wa kulia.
Kundi la nyani lililokuwa likiingia kwenye lango la mbuga hiyo.
Lazima kulikuwa na 100 - wanaume wakubwa waliokuwa wakitazama mabega yao kwa mashaka, vijana waliobalehe wakirukaruka na miili yao kupigana, akina mama wakiwa na watoto wachanga wenye velcro yaani aina ya kishikizo cha kubandika na kubandua shingoni mwao.
Katika muda uliosalia wa safari ya takriban kilomita 80, tulipunguza mwendo mara kadhaa kwa familia za tembo na makundi ya tandala wakivuka njia.
Tulisimama ili kupeleleza twiga waliokuwa wakichunga huku pundamilia na dondoro wakitafuna.
Tuliona ndege hawa ‘lilac-breasted rollers’ pamoja na kundi kubwa la ndege wa kusini hondohondo yaani hornbills, mdiria na tukasikia kilio cha ndege wa kijivu na kumwona kwa wakati.
Wakati Mark "Butch" Butcher - mkurugenzi mkuu wa Imvelo Safari Lodges - alifikiria kwa mara ya kwanza kuzindua treni ya utalii katika miaka ya 1980 na kujitolea kwa miaka mingi kuendesha urasimu wa Zimbabwe ili kufanikisha jambo hilo, maono yake hayakuwa tu kuhusu ukuu wa wanyamapori wa Hwange.
Badala yake, alilenga kuelekeza historia ya mbuga hiyo, na kwa kufanya hivyo, kuangazia umuhimu wa kukua kwa utalii unaozingatia jamii na juhudi za uhifadhi.
Njia za reli zimekuwa sehemu ya hadithi ya hifadhi hiyo tangu kuanzishwa kwake.
Njia za reli za Zimbabwe hapo awali zilijengwa ili kuunganisha maeneo ya uchimbaji madini na kilimo karibu na maeneo ya bandari za pwani katika nchi jirani za Msumbiji na Afrika Kusini.
Njia hii iliundwa mnamo 1904, miaka 24 kabla ya Hifadhi ya Wankie.
Lakini mpango huo uliendelea na licha ya njia hizo, Hifadhi ya Wankie ilianzishwa mwaka wa 1928 chini ya usimamizi wa mlinzi wa wanyamapori Ted Davison.
Leo hii, hakuna mnyama katika sehemu hii ya Hwange ambaye anakumbuka mandhari hiyo bila treni.
Si jambo la ajabu kuwakuta simba wakilala kwenye reli zilizochomwa na jua au kuwatumia kujificha wanapowinda kwenye uwanda.
Kwa hivyo, shirika la Elephant Express lilipoanzishwa mwaka wa 2015, kupeleka watu kwenye nyumba za kulala wageni za Imvelo, Butcher alijua kuwa ingewapa wageni uzoefu maalum wa safari.
"Wahifadhi wa mbuga wamepanda treni hizo kwenye njia hizi kwa miaka," mlinzi wa zamani wa mbuga ya Hwange aliniambia.
Wakati Butcher ilipoanza kama mlinzi wa mbuga zaidi ya miaka 40 iliyopita, mvutano kati ya mbuga na jamii ulikuwa dhahiri.
Hii ni sehemu ya sababu ya jinsi majeshi ya kikoloni ya Uingereza yalivyochagua ardhi kwa ajili ya uhifadhi, na jinsi jambo hili lilivyojitokeza katika juhudi za utalii zilizofuata.
Wakati maofisa wa serikali wakati huo - Rhodesia walipoweka mipaka ya eneo ambalo sasa linaitwa Hwange, walidai hii ni kwa sababu kulikuwa na wakazi wachache binadamu ¬– kauli ambayo ilipuuza familia nyingi za kuhamahama za Wazimbabwe weusi ambao waliita eneo hilo nyumbani - na kusababisha mvutano kati ya wanyama na binadamu.
Kwa miaka mingi, kutokana na uamuzi wa Davison wa kuchimba visima ili kuunda chanzo cha kudumu cha maji na ulinzi unaotolewa na walinzi waliojitolea na walinzi wa mbuga, idadi ya wanyamapori huko Hwange iliongezeka.
Kuongezeka kwa idadi ya wanyama kuliwavutia wawindaji na watalii wanaolipa kutoka nje ya nchi, lakini wao na pesa zao walibaki kwenye mbuga badala ya kunufaisha jamii zinazoizunguka.
Kwa bahati mbaya, Butcher alielezea, kuongezeka kwa wanyama na idadi ya watu pia kumesababisha migogoro zaidi na wanakijiji wa eneo hilo, ambao wanaogopa tembo wanaweza kula mazao yao na simba kuwinda ng’ombe wao.
Wakati Butcher anawasili Hwange, alibainisha kuwa "kijiji kilichukulia wanyama hao kuwa mali ya mbuga".
Wakazi wa kijiji hawakuona mapato kutoka kwa wanyama hawa ambao walitishia maisha yao wenyewe.
Na nchini Zimbabwe, ambako wengi wanategemea kilimo cha kujikimu na asilimia 60 ya watu wanakabiliwa na njaa, Butcher alisema, "wanyamapori lazima wagharamike kwa wao kuishi".
Kwa wengine, ujangili na uwindaji haramu hujaza pengo hili.
Ghafla, gari-moshi letu dogo lilisimama.
Tulichungulia kwa kutazamia nje ya pande zilizo wazi za gari la reli kwa ajili ya kuona wanyama, lakini Vusa Ncube, mwanakijiji wa Ngamo na kiongozi wetu mkuu wa safari, alituomba tukusanyike.
Upande wa kushoto wa treni, bamba la mbao lililosomeka "Mti wa Cecil" liliwekwa kwenye mti.
Ncube alisimulia kwa dhati kisa cha mauaji ya kusikitisha na haramu ya mmoja wa simba kipenzi wa eneo hilo.
Ujangili pia umepunguza idadi ya vifaru huko Hwange.
Ni vifaru wachache tu weusi wanaodhaniwa kusalia katika eneo hilo, na vifaru weupe wametoweka ndani kwa zaidi ya miaka 15.
Katika kukabiliana na hali hiyo, vijiji vya Tsholotsho kwenye mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Hwange vinafanya kazi na Butcher na Imvelo Safari Lodges ili kuhakikisha wakazi wanaweza kufaidika na uhifadhi wa wanyamapori na utalii.
Elephant Express inaunganisha abiria wake na miradi miwili kama hii: Imvelo’s Camelthorn Lodge, iliyojengwa kwenye ardhi inayomilikiwa na jamii;na Jumuiya ya Uhifadhi wa Faru ya Rhino Conservation Initiative (CRCI), mradi ambao utahamisha vifaru kutoka sehemu nyingine za Zimbabwe hadi kwenye msururu wa hifadhi kwenye ardhi za jumuiya ambazo hatimaye zitafunguliwa kwenye mbuga hiyo.
Ziara yangu ilikuwa mwezi wa Mei mwaka huu, wakati kampuni ya utalii ya Wilderness Travel yenye makao yake nchini Marekani iliposhirikiana na Imvelo kuleta kikundi kidogo cha wasafiri kushuhudia kuwasili kwa faru wa kwanza wa CRCI, Thuza na Kusasa.
Baada ya kufika Camelthorn Lodge, tulikaribishwa na Siboe Sibanda, meneja wa nyumba ya kulala wageni na mzaliwa wa Tsholotsho ambaye huhakikisha kila kitu kinaende sawa kwa wageni wa Camelthorn.
Na kwa sababu nyumba ya kulala wageni iko kwenye ardhi ya jamii, badala ya ndani kabisa ya mbuga ya kitaifa, anaweza kurudi nyumbani jioni ili kutumia wakati na familia yake.
"Nataka kufanya kazi ya utalii," Sibanda aliniambia.
"Lakini kwa kawaida, unakaa mbali na familia kwa siku nyingi. Kwa njia hii ninaweza kwenda nyumbani kwa familia yangu usiku."
Vile vile, mradi wa CRCI unatokana na dhana kwamba ili kufanikiwa, uhifadhi nchini Zimbabwe lazima uendane na maisha na vipaumbele vya wanajamii.
Tulipofika nyumbani kwa Johnson na Dorothy Ncube, mkuu wa kijiji cha Ngamo na mkewe walitusalimia wakiwa
Tulipoketi kwenye duara tukinywa chai na kahawa, Ncube alikumbuka furaha yake ya kuwaona vifaru akiwa mtoto.
"Watoto wengi katika kijiji hiki hawajawahi kuona faru, " alisema akitikisa kichwa.
"Lakini hilo litabadilika. Hawa ni vifaru wao. Vifaru wetu."
Hakika, kutoka kwa boma la Ncube, tulielekea katika shule ya eneo hilo, ambapo wanafunzi walikuwa wakichora picha za faru na kuandaa hotuba fupi kuhusu umuhimu wa wanyama hao kwa jamii yao.
Patricia ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita alijitolea kuongea.
"Lazima tuokoe faru kwa sababu ni spishi iliyo hatarini kutoweka. Lazima tuifanye salama," alisema.
Hotuba hiyo fupi ilimletea heshima ya kuwa mmoja wa watoto wa kwanza kuwatembelea vifaru ana kwa ana.
Kiwango hiki cha umiliki ni tofauti ya moja kwa moja na jinsi utalii wa hifadhi ulivyofanya kazi kihistoria katika Hifadhi ya Kitaifa ya Hwange na Zimbabwe kwa mapana zaidi.
Na, kulingana na viongozi kama Ncube na Butcher, ni njia bora ya kuwahudumia wanyamapori wa eneo hilo na watu wake.
Shirika la Elephant Express lilipofunga safari ya kurejea Dete Station, nilifurahia kukutana na wanyamapori tele wa Hwange.
Lakini nilishindwa kujizuia kuuliza: wakati mwingine nitakapokuwa hapa, je, ninaweza kuona faru akivuka njia.