Tetesi za Soka Ulaya Jumapili: Guehi ataka kuhamia Madrid

Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa Crystal Palace Marc Guehi, 25, amewafahamisha washauri wake kwamba anapendelea kujiunga na Real Madrid baada ya uhamisho wake wa kujiunga na Liverpool kugonga mwamba. (Mirror)
Barcelona wamemtambua mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland, 25, kama mbadala wa muda mrefu wa mshambuliaji Robert Lewandowski. (Football Insider)
Mabingwa wa Ligi ya Primea, Liverpool wanamfuatilia kiungo wa Brighton Carlos Baleba. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon mwenye umri wa miaka 21 pia bado analengwa na Manchester United. (Team Talk)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham Hotspur na Arsenal ni miongoni mwa timu kadhaa za Ligi ya Primea zinazomfuatilia kiungo wa kati wa Athletic Club na Uhispania Oihan Sancet, 25. (Fichajes)
Manchester United wako tayari kumtoa kwa ofa kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 20, pamoja na pesa taslimu ili kumsajili Federico Valverde wa Real Madrid. Hata hivyo, Real hawana mpango wa kumuuza kiungo huyo wa kati wa Uruguay, 27 (Goal)
Bayern Munich na Manchester United wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona Frenkie de Jong, 28, huku mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi ukitarajiwa kuisha msimu ujao wa joto. (Fichajes)

Chanzo cha picha, Getty Images
Matumaini ya Marcus Rashford kuhamia Barcelona yamezimwa na vikwazo vya mishahara vya La Liga. Mshambuliaji huyo wa Manchester United na England, 27, kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu hiyo ya Uhispania lakini sheria za kifedha zinaweza kuathiri mkataba wowote wa kudumu. (Daily Mail)
Senne Lammens alikataa kuhamia Aston Villa msimu wa joto ili kujiunga na Manchester United. Mlinda lango huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 23 alitambuliwa kama mbadala wa Emiliano Martinez ikiwa angeondoka katika klabu hiyo. (Birmingham Live)
Wakala wa kiungo wa kati wa Spurs Xavi Simons anasema mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi " hana masikitiko" baada ya uhamisho wake kwenda Chelsea msimu wa joto kugonga mwamba. (Metro)















