Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi: Je, Harry Kane kumrithi Lewandowski Barcelona?

Chanzo cha picha, Getty Images
Klabu ya Barcelona inamtaka nahodha wa Uingereza Harry Kane, 32, ambaye ameifungia Bayern Munich mara 95 katika mechi 102 za ligi. Kane anaonekana kama mbadala wa mshambuliaji wa Poland na Barcelon Robert Lewandowski. (El Nacional - kwa Kihispania)
Mkufunzi wa Manchester United Ruben Amorim atapewa fedha za kumsajili kiungo i wa Nottingham Forest na Uingereza Elliot Anderson, 22, mwezi Januari. (Team talk)
Klabu za Chelsea, Manchester United na Newcastle United zina nia ya kumsajili kumnunua kiungo wa kati wa Real Madrid na Ufaransa Eduardo Camavinga, 22, ambaye thamani yake ni euro 80m (£69.7m). (CaughtOffside)
Real Marid inavutiwa na kiungo wa Liverpool na Uholanzi Ryan Gravenberch, 23, ambaye thamani yake ni euro 75m (£65.3m). (Fichajes - kwa Kihispania)
Klabu ya Arsenal ina imani kuwa beki wa Ufaransa William Saliba, 24, atatia saini kandarasi mpya ya muda mrefu huku Real Madrid ikimfuatilia mchezaji huyo. (Football Insider)
Manchester United ilishindwa kumsajili kipa wa Italia Gianluigi Donnarumma, 26, kabla mchezaji huyo kuhamia Manchester City kutoka Paris St-Germain kwani jumla ya ada ya uhamisho na malipo ya mshahara yangekuwa takriban £130m. (Telegraph - usajili unahitajika)

Chanzo cha picha, Getty Images
Maafisa wa West Ham wamemkosoa mkufunzi wa Ureno Nuno Espirito Santo, 51, ambaye alifutwa kazi na Nottingham Forest mapema mwezi huu, kama mbadala wa Graham Potter baada ya kuanza vibaya msimu huu. (Sportsport)
The Hammers wamekataa kutoa mbinu rasmi kwa mchezaji wao wa zamani Frank Lampard, 47, ambaye sasa ni meneja wa klabu ya Coventry City. (Football Insider)
Kocha wa zamani wa Liverpool Rafael Benitez, 65, anasema anataka kuinoa Uingereza tena. (Telegraph - usajili unahitajika)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












