Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 22.01.2024

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ivan Toney
Iliyochapishwa

Mshambuliaji wa Brentford na Uingereza Ivan Toney, ambaye amekuwa akihusishwa na uhamisho wa Arsenal na Chelsea, hatashinikiza kuhama Januari na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anapanga kusalia na The Bees hadi msimu wa joto. (Mirror)

Newcastle United haitawauza wachezaji wake wawili wa Uingereza, beki Kieran Trippier, 33, anayelengwa na Bayern Munich - au mshambuliaji Callum Wilson, 31, ambaye amekuwa akihusishwa na Atletico Madrid, mwezi huu. (Telegraph – Subscription Required)

Trippier na Wilson hawatasita kuhama lakini Bayern watajaribu dhamira ya Newcastle kwa kutuma ofa iliyoboreshwa ya kumnunua beki huyo baada ya ofa ya awali kukataliwa. (Guardian)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Trippier

Newcastle wanataka euro 15m (£12.9m) kutoka Bayern Munich kwa Trippier, wakati klabu hiyo ya Ujerumani inataka tu mkataba wa mkopo. (Bild in Sport - Deutsch)

Newcastle United italazimika kuwauza kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes, 26, na mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 24, ili kukidhi kanuni za uchezaji wa haki za kifedha. (Football Insider)

Jose Mourinho anapendelea kusalia Italia baada ya kutimuliwa na Roma na Mreno huyo anatazamiwa kufanya mazungumzo na rais wa Napoli Aurelio de Laurentiis kuhusu kuchukua mikoba ya mabingwa hao wa Serie A wanaotatizika. (Times – Subscription Required )

.

Chanzo cha picha, Getty images

Maelezo ya picha, Jose Mourinho

Crystal Palace wameanza kuandaa orodha fupi ya watu wanaowania kuchukua nafasi ya meneja Roy Hodgson, huku bosi wa zamani wa Nottingham Forest Steve Cooper, meneja wa zamani wa Wolves Julen Lopetegui, bosi wa Ipswich Kieran McKenna na bosi wa zamani wa Mainz Bo Svensson wakiwa miongoni mwa wagombea. (Mail)

Tottenham wamekataa ofa ya pauni milioni 20 kutoka kwa Al-Nassr kwa ajili ya mlinzi wa Brazil Emerson Royal, 25, huku timu hiyo ya Saudi Pro League ikifikiria kuongeza ofa yao. (Sport)

Juventus bado wanavutiwa na kiungo wa kati wa Tottenham Pierre-Emile Hojbjerg, 28, lakini Spurs watazingatia tu mauzo ya kudumu au mkopo na wajibu wa kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark. (Sky Sports Germany)

.

Chanzo cha picha, getty Images

Maelezo ya picha, Ben Godfrey

Beki wa Everton Ben Godfrey anaweza kuwa chaguo kwa AC Milan, wakati Sheffield United na Leeds United pia wanavutiwa na Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 26. (Calciomercato – in Italy)

Aston Villa wamekataa ofa ya West Ham ya kumsajili mshambuliaji wa Colombia Jhon Duran, 20, kwa mkopo na chaguo la kumnunua. (Guardian)

Liverpool wanataka pauni milioni 20 kumnunua mlinda mlango wa Jamhuri ya Ireland Caoimhin Kelleher, 25, ambaye amekuwa akihusishwa na Celtic. (Football Insider)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kipa Kelleher

PAOK ya Ugiriki iko kwenye mazungumzo ya kutaka kumsajili beki wa Wolves Jonny Castro Otto, 29. Mhispania huyo amepigwa marufuku kushiriki katika kikosi cha kwanza kufuatia tukio la uwanja wa mazoezi mwezi Novemba. (THE STAR in Shropshire)

Klabu ya Ujerumani Eintracht Frankfurt imefikia makubaliano ya mdomo na mshambuliaji wa Paris St-Germain Mfaransa Hugo Ekitike, 21, kuhusu kuhama na wanatazamiwa kuongeza mazungumzo. (Sky Sports Germany)

Vilabu vya La Liga Cadiz na Getafe vimetoa ofa kwa kiungo wa Sporting Gijon Mfaransa Jonathan Varane, kaka wa kambo wa beki wa Manchester United Raphael Varane. Timu za Norwich na QPR pia zina zabuni za kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (L'Equipe – in French}