Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya: United yamtolea macho Mateta
Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa wa Crystal Palace, Jean-Philippe Mateta, mwenye umri wa miaka 27. (Sun).
Real Madrid, Bayern Munich, Chelsea na Tottenham zote zina nia ya kumsajili beki wa Hispania chini ya miaka 21 wa Bournemouth, Dean Huijsen, mwenye umri wa miaka 19, ambaye thamani yake ni pauni milioni 50. (Mail)
West Ham na Crystal Palace ni miongoni mwa klabu zinazotaka kumsajili beki wa Uingereza anayekipiga Southampton, Taylor Harwood-Bellis, mwenye umri wa miaka 23, katika msimu huu wa joto. (Football Insider)
Atletico Madrid wanatarajiwa kutoa ofa ya takriban euro milioni 60 (pauni milioni 50) kumsajili mshambuliaji wa Marseille na Uingereza, Mason Greenwood, mwenye umri wa miaka 23, mwishoni mwa msimu. (Fichajes - in Spanish)
Kiungo wa Ujerumani, Joshua Kimmich, mwenye umri wa miaka 30, anaonekana atasalia Bayern Munich msimu huu wa joto licha ya kusakwa na vilabu vya Arsenal na Paris St-Germain. (Sky Germany).
Chelsea inamtaka winga wa Hispania chini ya miaka 19 anayechezea Real Betis, Jesus Rodriguez, mwenye umri wa miaka 19, ambaye ana kipengele katika mkataba wake cha kuuzwa kwa pauni milioni 42, huku Liverpool pia wakifuatilia maendeleo yake. (Mail)
Manchester United na Liverpool wameulizia kuhusu upatikanaji wa kiungo wa Brazil wa Atalanta, Ederson, 25, ingawa Manchester City pia inamtaa kwa udi na uvumba mchezaji huyo mwenye thamani ya pauni milioni 50. (Caught Offside)
Manchester United wanatumai kuuza baadgi ya wachezaji wake katika majira ya joto kabla ya kuamilisha usajiliwa euro milioni 80 (pauni milioni 67) wa mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia, Benjamin Sesko, mwenye umri wa miaka 21. (Caught Offside).
Liverpool pia inataka kumfanya Sesko kuwa sehemu ya kikosi chao watakachokitengeneza katika majira ya joto. (Give Me Sport).
Liverpool inaweza kumuuza kwa mkopo kiungo wa Uingereza chini ya miaka 21, Harvey Elliott, mwenye umri wa miaka 21, msimu ujao ili aweza kupata muda mwingi wa kucheza katika kikosi cha kwanza (Football Insider).
Barcelona inataka kumbana kwa mkataba mpya na kiungo wa Uholanzi, Frenkie de Jong, mwenye umri wa miaka 27 ili asalie klabuni hapo, baada ya Arsenal kuonyesha nia ya kumsajili. (Sport - in Spanish)