Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Bruno Fernandes na wachezaji wengine 5 kuondoka Man United
Nahodha Bruno Fernandes, mshambuliaji wa Ureno mwenye umri wa miaka 30, ni mmoja wa wachezaji sita wa kikosi cha kwanza wanaotarajiwa kuondoka Manchester United msimu huu wa joto. (Football Insider)
Bayern Munich wanamlenga Eberechi Eze kama mbadala wa Florian Wirtz, Liverpool na Newcastle wanavutiwa na Joao Pedro na Manchester United tayari kuuza idadi kuu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza.
Bayern Munich wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Crystal Palace na England Eberechi Eze, 26, baada ya kumkosa mshambuliaji wa Ujerumani anayekwenda Liverpool Florian Wirtz, 22. (Mirror),
Liverpool wamempa Wirtz wa Bayer Leverkusen kandarasi yenye thamani ya zaidi ya pauni 320,000 kwa wiki huku wakitarajia kukamilisha dili la mchezaji huyo. (Sky Sports Switzerland – in French), nje
Mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich pia wanavutiwa na winga wa Brighton na Japan Kaoru Mitoma, 28, na mshambuliaji wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, 25. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin de Bruyne, 33, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wa kwenda kujiunga na mabingwa wa Serie A Napoli wiki mbili zijazo. (Mail)
Liverpool na Newcastle wanatazamia kumenyana na mshambuliaji wa Brighton na Brazil Joao Pedro, 23. (Sportsport)
Hatima ya winga wa Uingereza Jack Grealish katika klabu ya Manchester City imetiliwa shaka zaidi baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kuachwa nje ya kikosi chao kwa mechi ya mwisho ya msimu huu huko Fulham.
(Telegraph – Subscription Required)
Kocha wa Manchester United Ruben Amorim amewajulisha wachezaji wake kuwa atasalia Old Trafford. (Athletic – Subscription Required)
Mshambulizi wa Denmark Rasmus Hojlund, 22, ni mtu mwingine anayetarajiwa kuondoka huku Manchester United ikiwa tayari kupokea ofa. (GiveMeSport)
Inter Milan wanataka kumsajili Luka Modric mwenye umri wa miaka 39 baada ya kiungo huyo wa kati wa Croatia kuthibitisha kuwa ataondoka Real Madrid msimu huu wa joto. (Fichajes – In Spanish)
Nottingham Forest wanafikiria kumnunua beki wa Liverpool mwenye umri wa miaka 22, Jarell Quansah. (Football Insider)
Beki wa kati wa Manchester United, Victor Lindelof ataondoka katika klabu hiyo kama mchezaji huru mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu. (Fabrizio Romano)
Newcastle wanatarajiwa kushindana na Napoli, Juventus na Roma kumsajili beki wa kulia wa Atletico Madrid na Argentina Nahuel Molina, 27. (Marca, via Sportwitness)
Galatasaray wametoa ofa kwa winga wa Ujerumani Leroy Sane, 29, ambaye mkataba wake na Bayern Munich unamalizika msimu huu wa joto, huku pia klabu za Napoli na Ligi ya Premia zikiwa na nia ya kutaka kumnunua. (Sky Germany – In Deutsch)
Imetfasririwa na Seif Abdalla