Tetesi za Soka Ulaya: Arsenal iko mstari wa mbele kumfukuzia Hinshelwood

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wanaongoza mbio za kumsajili kiungo wa kati wa England, Jack Hinshelwood, mwenye umri wa miaka 21, kutoka Brighton. (Sun)
Barcelona wanajiandaa kuwasilisha ofa ya tatu ya takriban pauni milioni 60 kwa kiungo wa Uhispania, Rodri, mwenye miaka 30. Hata hivyo, ofa hiyo bado itakuwa pungufu kwa pauni milioni 10 ya thamani ambayo Manchester City imeweka kwa mchezaji huyo. (Independent)
Manchester United, Tottenham na Arsenal wamefanya mazungumzo ya ndani kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Nigeria, Victor Osimhen, mwenye miaka 27, kutoka Galatasaray. (Teamtalk)
Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi, Cody Gakpo, mwenye miaka 27, amefikia makubaliano ya awali kuhusu uhamisho wake kwenda Tottenham. (Voetbal International - in Dutch)
Crystal Palace wanatarajiwa kudai hadi pauni milioni 25 kwa beki wa kulia wa Colombia, Daniel Munoz, mwenye miaka 30, ambaye analengwa na Everton.(Football Insider)
Klabu ya Como imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa England, Liam Delap, mwenye miaka 23. Chelsea wanamthamini mchezaji huyo kwa pauni milioni 55.(Mail)
Kiungo wa Denmark, Pierre Emile Hojbjerg, mwenye miaka 31, ameondolewa unahodha wa Marseille baada ya kukataa uhamisho wa pauni milioni 15 kwenda Newcastle. (Mail)
Newcastle wameweka macho yao kwa kiungo wa Brighton na timu ya taifa ya Cameroon, Carlos Baleba, mwenye miaka 22, huku klabu hiyo ikitafuta kuimarisha safu yake ya kiungo. (Talksport)
Coventry wanataka kumsajili beki wa England, Josh Acheampong, mwenye miaka 20, kutoka Chelsea. (Talksport)
Mshambuliaji wa Arsenal, Gabriel Jesus, yuko kwenye mazungumzo na Napoli, huku mchezaji huyo wa Brazil mwenye miaka 29 akitafakari kuondoka Arsenal wakati wa dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi. (Fichajes - in Spanish)
Tottenham wanaendelea kufanyia kazi mpango wa kumsajili winga wa Brazil, Savinho, mwenye miaka 22, ambaye anataka kuondoka Manchester City. (Standard)
Winga wa Ubelgiji, Mika Godts, anatarajiwa kujiunga na Paris Saint Germain, ambao wamekubaliana kumlipa Ajax euro milioni 55, sawa na takriban pauni milioni 47, kwa mchezaji huyo mwenye miaka 21. (L'Equipe - in French)
Leeds watalazimika kulipa angalau euro milioni 10, sawa na pauni milioni 8.5, iwapo wanataka kumsajili beki wa Uswisi, Nico Elvedi, mwenye miaka 29, kutoka Borussia Monchengladbach.(Kicker - in German)















