Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 26.12.2022

Iliyochapishwa

Cristiano Ronaldo huenda asiwe supastaa pekee anayeelekea Saudi Arabia katika mwaka mpya kwani Al Nassr pia wanataka kumleta kiungo wa kati wa Chelsea N'Golo Kante, kwa mujibu wa Foot Mercato. Mkataba wa sasa wa Mfaransa huyo unamalizika mwishoni mwa msimu huu na anaweza kusaini makubaliano ya awali na klabu ya kigeni mwezi Januari. Kante amekuwa akisumbuliwa na majeraha katika kipindi cha miaka michache iliyopita na kwa sasa yuko nje ya uwanja kutokana na kuwa na tatizo la msuli wa paja kwa muda mrefu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 bado atahitajika sana msimu ujao lakini Al Nassr wanataka kujenga timu karibu naye na Ronaldo (mirror).

Gabriel Martinelli "anakaribia" kukabidhi mustakabali wake Arsenal, kulingana na mtaalam wa uhamisho Fabrizio Romano. Mkataba wa sasa wa fowadi huyo mwenye umri wa miaka 21 unamalizika hadi 2024, lakini Arsenal imekuwa ikizungumza na wawakilishi wa Martinelli kuhusu kuongeza muda wake wa kukaa London Kaskazini. Romano anasema mazungumzo hayo sasa yako katika "hatua za mwisho" ingawa hakuna kilichokubaliwa kikamilifu au kutiwa saini. Akizungumza na Sky Sports mwezi Novemba, Martinelli alisema: "Nina furaha sana Arsenal, nimesema mara nyingi. Hii ni klabu yangu. Ninapenda kuwa hapa. (Skysport)

Newcastle, Juventus na Borussia Dortmund ni miongoni mwa vilabu kadhaa vinavyofikiria kumnunua beki wa kulia wa Real Valladolid wa Uhispania chini ya umri wa miaka 19 Ivan Fresneda, 18. (Fabrizio Romano).

Wolves wanalenga mlinda mlango mpya mwezi Januari ili kutoa ushindani kwa mchezaji wa kimataifa wa Ureno Jose Sa, 29. (Express na Star)

Liverpool inawahitaji Sofyan Amrabat na Enzo Fernandes wakati dirisha la Januari linakaribia kwa kasi, ripoti ya AS. Amrabat na Fernandes walikuwa wawili kati ya safu ya kiungo iliyoanza Kombe la Dunia.

AS inasema mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anawalenga wawili hao iwapo Reds watamkosa Borussia Dortmund na nyota wa Uingereza Jude Bellingham msimu wa joto. (Skysport).

Aston Villa wameanza mazungumzo na Villarreal kuhusu mpango wa kumnunua winga wa Uholanzi Arnaut Danjuma, 25. (Todofichajes)

Inter Milan wanafikiria kumnunua mlinzi wa Roma Muingereza Chris Smalling, 33 msimu wa joto. (Calciomercato - in Italian) Newcastle wameanza mazungumzo na Flamengo kuhusu kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Matheus Franca, 18. (Globo)

Tottenham wana nia ya kumsajili beki wa kulia wa Uhispania Pedro Porro, 23, kutoka Sporting Lisbon. (Football London)

Wolves wamethibitisha kumsajili kwa mkopo Matheus Cunha kutoka Atletico Madrid. Mshambuliaji huyo mpya alisema: "Nimefurahi sana kuwa sehemu ya kundi hili na kuwa sehemu ya klabu hii - ni klabu kubwa. Nina furaha kucheza Ligi ya Premia, kucheza Wolverhampton, na nadhani jambo muhimu zaidi ni kwamba nina furaha kama mtoto." Mkataba wa Cunha na Wolverhampton utakuwa halali hadi Juni 2027.(Mirror)

Kipa wa England Jordan Pickford, 28, ana furaha kuongeza muda wake wa kusalia Everton huku mazungumzo yakiendelea kuhusu kandarasi mpya na klabu hiyo ya Merseyside. (Liverpool Echo)

Chelsea wako sokoni kutafuta beki wa kati na wamepanga mbadala wa Josko Gvardiol, kwa mujibu wa ripoti. Beki huyo wa Croatia amekuwa akihusishwa pakubwa na kuhamia Stamford Bridge lakini baada ya Kombe la Dunia la kuvutia, thamani yake imepanda. Na hii imeiweka Chelsea mbali kutokana na thamani ya juu, Kwa hivyo, Benoit Badiashile, Piero Hincapie na Evan Ndicka wote wanachukuliwa kuwa walengwa wanaotarajiwa Januari kwani Graham Potter bado anataka beki wa upande wa kushoto.(The sun)